Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Baada ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Ndug John Heche kueleza jana kuwa CHADEMA wanaenda kuweka ushahidi na kuuelezea Umma namna taifa hili linavyoibiwa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo tenda za ununuzi za mradi wa SGR, chawa wa Samia na CCM amejitokeza kumtisha Heche eti atakamatwa na kushtakiwa aelezee amepata wapi nyaraka za Serikali ili kumtisha Heche na CHADEMA wasianike wazi wizi wanaoufanya CCM kwa taifa letu pendwa.
Nawaomba CCM mumueleze huyo Kigogo wenu, kuwa nchi hii kuna sheria maalum inayowalinda Watoa Taarifa za Ufisadi, Wizi na Uhalifu wote, hivyo ni vizuri ajifunze na asome mambo kabla ya kupost ujinga wake mitandaoni. Heche na CHADEMA wakitoa taarifa za Wizi unaofanyika huko Serikalini na CCM wanatakiwa kulindwa na sio kukamatwa na kushtakiwa.
Sheria hiyo inaitwa The Whisleblower and Witness Protection Act ( Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi).
Mwisho kwa CCM na machawa wenu. Napenda kuwaeleza kuwa nchi yetu lazima iokolewe sasa dhidi ya udhalimu na wizi wa kutisha mnaoufanya. Taifa hili Mungu analipenda na ndo mana kila siku ananyanyua watu kwa ajili ya kulitetea.
Lord denning,
Dubai