Nasema hivo kutokana na ukweli kuwa chama cha mapinduzi 2015 wananchi walikuwa wameshakikataa kwa kuchoshwa na rushwa iliyokithiri ya utawala wa kipindi hicho!Ujio wa Magufuli ambaye tayari alikuwa ameshajipambanua kwa wananchi kwa uchapakazi wake kuliwafanya baadhi ya watanzania kurudisha moto! Hiyo hali ilipelekea kwa CCM kuheshimika tena kwa watanzania walio wengi na kupungua kama sio kuisha kabisa tabia ya kuwazomea watu waliokuwa wakivaa sare za CCM. Nimachokiona sasa mtaani ni hali ile ya 2015 na kibaya zaidi ndani ya CCM hii hakuna mtu kwenye ushawishi aliyejipambanua kwa wananchi kama iliyokuwa Magufuli ingawa wote tunakubaliana kuwa Magufuli alikuwa na mabaya na mema yake!. Kwa hiyo CCM hii ijiandae kisaikolojia si kwa kuwatisha ila kuwaambia ukweli wananchi hawa wanahiyaji mtu wa kuwatetea na anayeaminika kwa vitendo sio projo.Uchaguzi wenu wa ndani ya chama mwakani muwe makini kuna uwezekano mkawapoteza vijana wengi na kuweka wazee matajiri kupitia rushwa na hapo ndo mazishi rasmi ya CCM yatakapoanzia kabla ya 2025.Uwepo wa kikundi cha watu wanaojidai ndo wenye chama wakati walishashindwa kujipambanua kwa wananchi na wanafahamika kuwa ni mafisadi ni kuizika CCM. Kipindi cha nyuma hawa wazee wanaojiita ndo kwenye chama ndo walikuwa wamegawana mali za CCM wakila watakavyo huku wakichekelea na kujitwika uzalendo mfu uliojaa unafiki wa hali ya juu!