Uchaguzi 2020 CCM msimjibu Tundu Lissu mnazidi kuharibu. Je, Wananchi wana maisha magumu?

Uchaguzi 2020 CCM msimjibu Tundu Lissu mnazidi kuharibu. Je, Wananchi wana maisha magumu?

Mambo bado magumu

..Nashauri atangaze kuvifuta vitambulisho vya machinga.

..anatakiwa achukue hatua, aache kujibizana na Tundu Lissu.

..Lissu akisema wafanyakazi hawajaongezwa mishahara, Jpm anatakiwa aongeze mishahara.
 
Wanabodi, Mimi ni mwana ccm na nilitoa hapa ushauri kwenye uzi huu Uchaguzi 2020 - CCM msimjibu Tundu Lissu, Mnavyomjibu ndio anazidi kuongea mengi

Mkutano wa Tundu lissu Tunduma ni dhahiri jinsi viongozi wa CCM wanavyomjibu majukwaani ndivyo watu wanazidi kuhamasika na kumpenda zaidi Tundu lissu

Hoja nyingi za Tundu Lissu hazijibiki kirahisi na hata wanaojibu wanaacha maswali zaidi kuliko majibu mbele za wananchi

Majibu ya hoja za Tundu Lissu sasa yanasababisha watu wanaosikiliza kampeni za CCM kutafuta habari za upande wa Chadema, Kitendo cha viongozi kumuongelea Lissu imepelekea Wanaccm kuanza kumsikiliza Tundu Lissu na kujaa kwenye kampeni zake huko Tunduma

Mosi, Hoja ya uwanja wa ndege kujengwa Chato na Mbuga ya wanyama kuanzishwa huko ,Lisu anahoji mikataba na ni nani aliidhinisha bungeni uwanja kujengwa Chato na pesa hizo ni za nani? Tenda ya ujenzi ilitangazwa wapi na ni nani kapewa tenda hiyo, Kigezo gani kilitumika kumpa Tenda mkandarasi huyo,Huyo mkandarasi ana mahusiano gani na mamlaka?

Pili, Hoja ya mishahara ya watumishi wa Umma, Tundu Lissu anahoji ni sheria ipi imetumika kuwanyima nyongeza ya mishahara walimu na kada zingine,Anahoji majibu ya Mamlaka kuwa hawaongezi mishahara wapo bize na reli,stiglers gorge na barabara,Anahoji watu wa Jeshi la police nao wameumia hawajaongezewa pesa kwa miaka mitano.

Tatu, Anahoji TRA kama wakusanya mapato kupeleka Bank TRA notes za kuzitaka mabenki kufreeze au kumark account za wateja No debit (kuzuia akaunti za wateja pesa isitoke) bali wazitume TRA kiasi cha pesa chochote kilichopo na kinachoingia kwa wakati huo, Anahoji hali hii imepelekea wafanyabiashara kuwa maskini wa kutupwa na kushindwa kuajiri watu

Tundu Lissu anahoji, Maisha ya wakulima anaongelea mazao ya korosho na mahindi watu kuzuiwa kuuza nje kwa bei nzuri na kuambiwa walime kwa ajili ya chakula,Anahoji maisha magumu ya wakulima wa pamba na korosho kutolipwa pesa zao

Tundu Lissu anahoji sheria za utakatishaji pesa na uhujumu uchumi zinavyotumika kukandamiza watu na kutoa hofu kwa wananchi ambao ndio wenye nchi yao,Anahoji yeyote anayepinga serikali anafunguliwa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji pesa

Tundu Lissu anahoji mifumo ya elimu na ajira hasa maisha ya vijana waliomaliza vyuo kutoajirika

Nini kifanyike kujibu hoja hizi

Ni vyema CCM kama chama kikajikita kwenye sera zake na ilani ya chama,Majibu ya hoja hizi yamezidi kuzaa hasira kwa wananchi

CCM isijibu hoja hizi, Majibu ya hoja hizi kwa week moja hii yameongeza hasira kwa wananchi. Tundu Lissu anazidi kuwaelimisha wananchi hata mambo ambayo hawakuyajua

Tundu Lissu amegeuza kampeni zake kama darasa la kufundisha na kutoa elimu bure kwa wananchi kwa mambo yanayoendelea na wananchi wanamuelewa na kuwa na hasira juu ya CCM

Kwa sasa taarifa zake mitaani ndizo zinazoongeleka zaidi na kutafutwa na kila mwananchi ,Watu wanajadili hoja za lisu mitaani na kuzifurahia

Uchaguzi huu utufundishe wana ccm ni bora kuwaacha watu waongee ya moyoni kuliko kuwafungia,Mpaka sasa tangu mwaka waliofungiwa wangekuwa hawana hoja ya kuzungumza

Ccm ni wakati muafaka wa kujikita kwenye ilani na malengo yetu ya chama,Tuhubiri sera na ilani yetu,Yale tuliyokosea tukubali makosa na kujisahihisha
Sisi watumishi wa umma una jambo letu tarehe 28 October. Subirini tukiamka 29 ndio mtajua kama hii ni Tanzania mpya.
 
Nyerere mwingine kaibuka Tanzania.
If God say Yes no one can say No.

Viva Tundu lissu
 
Yani nikiona bongo fleva wanavyonyang'anyana peremende za CCM halafu kule Nigeria wasanii wana mahela lakini bado wanatumia ushawishi wao kuchochea mabadiliko kwenye jamii na mifumo ya nchi nasikia hasira mpka natamani kupiga ngumi ukuta…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata marekani na nchi za kiarabu nimmatajiri na maskini pia wapi acheni kutulisha matango pori
 
..Nashauri atangaze kuvifuta vitambulisho vya machinga.

..anatakiwa achukue hatua, aache kujibizana na Tundu Lissu.

..Lissu akisema wafanyakazi hawajaongezwa mishahara, Jpm anatakiwa aongeze mishahara.
Maisha hayana kanuni
 
Ilani yenu hamuiamin wenyewe mnaanza kuongelea Ilan za wengine... Nioneshe kwenye ilan yenu wapi mtatoa Bima buree.. japo mmetaja neno afya zaid ya mara ngapi uko
Bima inatolewa?
 
wananchi wana maisha ya kawaida: na ni ktu cha kawaida: and forever always lazima kue na matabaka ili maisha yasogee,
Maisha ya matabaka ndio unapendekeza eeeeh
 
Back
Top Bottom