Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu
Leo mimi kama mtanzania mwenye haki ya kutoa maoni, nimekuja kutoa maoni yangu na kuweka sawa historia kuhusiana na swala la michezo pamoja na siasa zetu hapa nchini. Kabla ya kuendelea na mada yangu, naomba nikiri tu kwamba kwa sasa michezo imekuwa ikipewa kipaumbele zaidi ya siasa hadi kupelekea baadhi ya watu kushindwa kujizuia hisia zao na kuanza kujitokeza kuzilaumu team zetu pamoja na vijana wetu wanaohamisha mawazo, fikra na akili zao katika michezo hususani kwa team za Yanga na Simba.
Sasa kabla ya kuendelea kuzilaumu Simba na Yanga naomba kwanza tuangalie historia ya michezo pamoja na siasa zetu.
Yanga na Simba zilianzishwa mnamo miaka ya 1930's huko kabla hata nchi zetu za Tanganyika na Zanzibar kupata uhuru wetu. Team hizi zimekuwa faraja na furaha kwetu miaka na miaka bila kujali utofauti wetu wa kidini, kikabila, rangi, Mikoa tunayotokea wala itikadi zetu za kisiasa kabla na baada ya uhuru. Kwa Sisi ambao tulianza kuzipenda na kuzikubali team hizi tangu miaka hiyo ya chama kimoja (CCM) tunafahamu fika jinsi vijana na wazee wa miaka hiyo walivyokuwa wanazipenda team zao hizi za Simba na Yanga hadi kupelekea sometimes kusikia vifo vya watu wanaojiua baada ya team yao ya Yanga au Simba kufungwa. Namaanisha kwamba swala la kupenda michezo haswa wa team za Simba na Yanga halikuanza leo, lipo miaka na miaka na huwa halibadiliki japo kuna kuna kipindi lilipungua kidogo (nitaeleza sababu hapo chini) lakini haimaanishi kwamba watu wanaweza kuacha kuzipenda na kuzishangilia team zao hizi bila kujali uvyama wala udini.
Miaka ya 90's wakati mchakato wa kuanzisha vyama vingi unafanyika, Simba na Yanga bado zilikuwa zikiendelea kutupa burudani na kukonga nyoyo za watanzania kama kawaida. Hilo liliendelea hata baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa. Naamaanisha kuwa watu walikuwa wanafuatilia siasa, lakini pia hawaachi kuendelea kufuatilia mchezo wa mpira haswa baada ya team nyingine kuibuka na kuongeza msisimko wa michezo nchini.
Mwaka 95's wakati wa uchaguzi mkuu watu walipiga kura na baada ya matokea ya uchaguzi kutangazwa watu waliendelea na Uyanga na Simba wao kama kawaida wakiwemo humo wana CCM, wana NCCR Mageuzi, wana CUF, wana TLP nk. Siasa ilibaki kama siasa, na michezo ilibaki kama michezo, hakuna mwanamichezo aliemlaumu mwanasiasa katika jukwaa la michezo, wala mwanasiasa aliemlaumu mwanamichezo katika jukwaa la siasa. Siasa ilibaki kuwa ni siasa, na michezo ilibaki kuwa ni michezo. Kila taasisi ilitafuta mbinu zake za kuvutia watu upande wake.
Mwaka 2000 pia uchaguzi mkuu ulifanyika na baada ya matokeo kutoka ambapo CCM ilishinda (inasemekana kwa kuiba kura) hakuna mwanasiasa yoyote au mwanachama wa CUF ambacho ndo kililalamika kuibiwa kura alijitokeza na kuanza eti Yanga na Simba zimesababisha washindwe, halikadhalika kwa upande wa michezo hakuna mwanamichezo aliejitokeza kuzungumzia siasa unless awe ameamua kusimama kama mwanasiasa (nje) ya michezo.
Mwaka 2005 baada ya uchaguzi mkuu ambao ulipelekea vijana wengi kutoka upinzani (Chadema) kushinda ubunge na uenyekiti wa serikali za mitaa, kisha kuja na hoja za kupambana na ufisadi.
Watu wengi haswa vijana waliokuwa wanafuatilia zaidi michezo, wakaamua kupunguza na wengine kuachana kabisa na michezo na badala yake wakahamishia nguvu kubwa katika siasa, wakiamini kwamba siasa ndio mfumo halisi wa maisha ya mtu. Hii ilipelekea mpaka michezo yetu na baadhi ya team zetu kukosa wadhamini kwa kuhofia kupata hasara pale wanapodhamini kitu ambacho hakina wafuatiliaji wengi. Mpaka hapo hakuna mwanamichezo au kada hata mmoja alieenda katika vyombo vya habari au mitandao ya kijamii na kuanza kuwalaumu vijana au vyama vya siasa kwa kuhamisha akili za watu kutoka katika michezo hadi katika siasa. Wanamichezo walipambana wenyewe kwa hali zao. Tuliokuwa vichwa ngumu wa michezo, japo tulikuwa nje lakini ufuatiliaji wetu wa michezo ulikuwa ni ule ule.
Hali iliendelea kiasi ya kwamba hadi watu hawakufikiria tena kwamba kuna mambo mengine ya kufuatilia nje ya siasa. Taarab ilikufa kifo cha mende, bongo fleva ikadorora, Yanga na Simba zikashuka viwango vya michezo kwa upande wa viwango vya club barani Africa na Dunia kwa ujumla. Ikawa kila kitu ni siasa.
Baada ya list of shem kutolewa pale mwenyeyanga, ndo kabisa vijana wakawa hawaambiwi kitu, maandamano yaruhusiwe yasiruhusiwe wao wanaingia tu barabarani, wazazi wawakataze wasiwakataze wao wataenda tu maanamanoni, jeshi la polisi litumie mabomu ya machozi au risasi, wao hawajali yani walikuwa tayari kufa kwa ajili ya siasa. Baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 ndo kabisa vijana walitoboka roho, wapo waliotekwa na kwenda kunyofolewa kucha, wapo waliovunjwa viuno na miguu katika maandamano, wapo waliouwawa kwa kuripukiwa na bomu la Soweto huko Arusha, yote hayo hayakuweza kupunguza kasi ya watu walioamua kuwa upande wa siasa. Na haswa adui yao mkubwa alikuwa ni Lowasa ambae viongozi wao wa upinzani walisema ndio fisadi papa anaetakiwa kushughulikuwa mapema kabla ya ku deal na wengine. Mpaka hapo Simba na Yanga zilikuwa zimebaki majina tu na historia ya hapa na pale, lakini wanamichezo pamoja na kuona kwamba swala la michezo linapoteza ushawishi, wao hawakuingia mitandaoni kuandika upuuzi kuhusu siasa. Wa wakakubali kuishi katika hali walivyokuwa nayo kipindi hicho mpaka Burundi na Rwanda zikawa zinakuja nchini kujipigia tu na kukusanya point kuondoka.
Kimbembe kilianza mwaka 2015, baada ya viongozi wa vyama vya upinzani kupata tamaa ya pesa, na matokeo yake kumleta yule waliesema kuwa ni mwizi wa taifa aje awe mgombea wao wa uraisi. Hapo ndio kosa la watu kuachana na siasa na kurudi katika michezo lilipoanzia. Na haikuwa kurudi katika michezo tu, bali kuna wengine walipata hasira wakaamua kwenda CCM na wengine kuachana jumla na siasa, kwani waliekuwa wanampinga, wanamshutumu na kumzomea kwa ufisadi ndio huyo huyo wanaambiwa wamchague ili akamalizie na kile kidogo alichokuwa ameshindwa kukiiba.
Na hakika result na madhara ya kumleta fisadi kugombea uraisi ilianza kuonekana muda mfupi tu baada ya uchaguzi. Kwani kila yalipoitishwa maandamano watu hawakuwa tayari tena kuandamana, maana waliona kuwa wao waandamanaji wanatumiwa tu kama daraja kwa faida ya wajanja wachache wa chama. Mfano unaambiwa andamana ili spika wa bunge Dr Tulia atoke katika uspika. Unaingia kichwa kichwa kuandamana unachezea virungu, unavunjwa mguu au kiuno halaf kesho aliesababisha uvunjwe mguu au kiuno anapewa nafasi ya kugombea tena ubunge au uraisi kupitia chama kile kile kilichokushawishi uandamane ili yeye atoke katika kiti. Sasa katika hali kama hiyo ndomaana baada ya waliempinga kuwa kiongozi hata wa serikali ya mitaa kutokana na ufisadi alipopewa nafasi tena ya kugombea uraisi watu wengi wakaona kumbe wanasiasa hawapo serious na matatizo ya wananchi, wao wanachoangalia ni matumbo yao na faida zao. Hivyo vijana ambao ndio ilikuwa nguvu kubwa ya upinzani na siasa kwa ujumla ikaamua ihamishie mawazo, fikra na akili katika michezo ambayo hawatokuja kuambiwa waandamane halaf kesho waliomwaambia waandamane na kuvujwa miguu waitwe ikulu kunywa chai.
Ni ujinga kulalamikia Simba na Yanga kwa sababu team hizi zilianzishwa kabla ya CCM, Chadema, ACT wazalendo, CUF nk. Kukimbilia kuzilaumu Simba na Yanga ni kutafuta kichaka cha kuficha ule upuuzi uliotokea mwaka 2015 ambao ndio uliozirudisha Yanga na Simba na sasa Taifa Stars kwenye ramani.
Ingekuwa vizuri wale waliosababisha haya mwaka 2015 waje siku moja wakiri mbele ya taifa au wawaombe radhi wanachama wao na ikiwezekana wajiudhuru kabisa ili kuonesha kwamba wameguswa na makosa yao.
Simba na Yanga zilikuwepo lakini watu waliandamana na hadi wengine kuuwawa mwaka 2001
Simba na Yanga zilikuwepo lakini watu waliandamana hadi kina Prof Lipumba walivyunjwa mikono.
Simba na Yanga zilikuwepo hadi bomu la Soweto liliuwa watu katika maandamano yalioshindwa kuzuilika.
Sasa leo hii kudai kuwa Yanga na Simba zinasababisha vijana wasiandamane au kufuatilia siasa za Tanzania ni uongo wa kitoto sana. Wenye akili mchawi wanamjua, japo wanashindwa kumtaja live. Simba na Yanga zinafanya kuangushiwa jumba bovu tu ambalo lilitakiwa limuangukie jamaa yule.
Tangazeni sera zenu vizuri ili mpate wafuatiliaji wa siasa kama miaka ile. Simba na Yanga zilikuwepo, zipo na zitaendelea kuwepo tu miaka yote no matter who win the election.