CCM na Mgogoro wa Kidini Tanzania

CCM na Mgogoro wa Kidini Tanzania

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Wiki kadhaa zilizopita, invisible alileta uzi ulio hoji iwapo Rais Kikwete na Serikali yake wanahusika katika mgogoro wa kidini unaoendelea nchini hivi sasa; Katika uzi huo, invisible alini ‘tag’ lakini kwa bahati mbaya sikuweza kushiriki kutokana na majukumu; Kwa vile muda umeshapita sana, nimeona nije na uzi mpya, ili kutoa fursa tena kwa wale wenye ambao bado wana interest na mada husika ili kwa pamoja tubadilishane mawazo “kwa hoja” zenye maslahi kwa taifa, na sio kwa hoja zenye kulenga kutugawa na kupandikiza chuki miongoni mwetu kama watanzania;

Taifa letu lipo katika mgogoro mkubwa wa kidini baina ya waumini wa kikristo na kiislamu. Kutokana na tatizo hili, kumekuwa na malalamiko mengi kutoka pande zote mbili, huku serikali, viongozi na taasisi mbali mbali za kidini zikizidi kunyoshewa vidole vya lawama kwamba aidha wanahusika au wanachangia katika mgogoro huu kwa njia moja au nyingine. Nia ya mjadala mada hii kujaribu kuliangalia suala hili kwa kina zaidi, kwa matarajio kwamba mwisho wa siku tutapata majibu kwa maswali makuu muhimu matatu yafuatayo:

Kwanza - Je, nini ni chanzo cha misuguano ya kidini nchini Tanzania?
Pili - Kwanini misuguano hii imezidi kushamiri katika miaka ya hivi karibuni tofauti na huko nyuma?
Na Tatu – Je, nini kifanyike kutatua tatizo hili kabla ya taifa halijasambaratika?

Tupende, tusipende, itakuwa ni vigumu kuelewa kiini cha mgogoro husika pamoja na ufumbuzi wake iwapo tutapuuzia mjadala unaohusisha sera na itikadi ya Ujamaa; Pamoja na mapungufu mengi ya Ujamaa, lengo la itikadi hii miaka michache baada ya uhuru ilikuwa ni pamoja na kuwaunganisha watanganyika waliotapakaa nchi nzima katika mgawanyiko wa imani kuu tatu za kidini – uislam, ukristo na imani za kienyeji (traditional beliefs), tukiachilia mbali diversity kubwa ya makabila. Katika mazingira haya, ili kujenga taifa lenye umoja na mshikamano, TANU (chini ya Mwalimu Nyerere) iliona kwamba njia bora ilikuwa ni kuondokana na market oriented liberalism na badala yake kufuata state centred socialism (UJAMAA) kama ndio itikadi na dira mpya ya taifa – kisiasa, kiuchumi, na kijamii; ili kusakafia lengo husika, ilionekana ni vyema kwa mfumo wa kisiasa nao ugeuzwe na kuwa mfumo wa chama kimoja – TANU na baadae CCM). Hivyo ndivyo TANU/CCM ilivyofanikiwa kupata legitimacy kwa muda mrefu, kwani taifa lilikuwa na mwelekeo na wananchi walijaa matumaini kupitia itikadi ya Ujamaa, ambayo ilihimiza umoja na undugu wa kitaifa, huku juhudi za maendeleo zikitekelezwa kupitia Sera ya kujitegemea na Sera ya Usawa chini ya Serikali ambayo haikuwa inafuata dini ya aina yoyote kwa mujibu wa Katiba (Secularization of the state);

Matokeo yake ikawa ni pamoja na – Ujamaa ku ‘encourage’ Secular Policies (sera zisizoegemea itikadi za udini bali utaifa), hasa Ujamaa sasa ukigeuka kuwa ni “DINI YA KIRAIA” (Civil Religion); Wananchi wengi waliitikia wito huu na kwa kiasi kikubwa sana wakawa ni waumini wakubwa wa Ujamaa mbele ya UMMA (Public) huku imani zao za kidini mbalimbali (Uislam, Ukristo na dini za Kienyeji) zikibakia kuwa ni suala BINAFSI (Private);

Juhudi Za Kujenga A Secular State na Changamoto Za Kidini Chini Ya Ujamaa

Ingawa Serikali ya TANU ilitamka rasmi kwamba dini ni suala binafsi, TANU iliendelea ku – encourage taasisi mbalimbali za kidini kusaidia kujenga umoja na maendeleo ya taifa huku ikihimiza uvumilivu wa kidini (religious tolerance); Kwa mtindo huu, ilikuwa ni rahisi kwa TANU kuunganisha itikadi yake ya Kisiasa (UJAMAA) na Values za Dini za uislam na ukristo na kufanya mchanganyiko huu kuwa sehemu muhimu ya national ethos (attribute), huku Ujamaa ukizidi kushika mizizi kama DINI YA KIRAIA na kuendelea kuungwa mkono na makundi mbalimbali ndani ya jamii, hasa yale ya waaumini wa kikristo na kiislam; Hivyo ndivyo serikali ya TANU ilifanikiwa kugeuza Tanzania kuwa ‘a Secular State’ – taifa lisilofungamana na itikadi ya dini yoyote, na kwa kiasi kikubwa, Taifa likaepuka misuguano ya kidini kwa muda mrefu;

Mradi huu uliolenga to secularize the state na kugeuza Ujamaa kuwa DINI YA KIRAIA ulichukua sura kuu mbili: Kwanza – Serikali ya TANU iliagiza taasisi zote za Kiislam kutochanganya dini na siasa; Lakini Pili, Serikali ya TANU pia ilihimiza baadhi ya taasisi za dini ya Kikristo kushiriki katika shughuli za maendeleo; Hili la pili lilikuwa ni kutengeneza bomu la kulipuka baadae, vinginevyo kwa ujumla wake, watanzania wengi waliendelea kuridhika na sera za TANU zilizolenga kujenga nchi katika mazingira ya usawa, umoja, udugu na mshikamano;

Kwa kumalizia sehemu hii ya kwanza, Serikali ya TANU ilifanikiwa sana kuifanya sehemu kubwa ya jamii kwa ‘part of the state’, hasa kufanikiwa kufanya the sphere of civil society na Ujamaa kuwa kitu kimoja; Kwa ku ‘promote’ haya mawili kama kitu kimoja, serikali ya TANU ikafanikiwa kusakafia vyema zaidi itikadi ya Ujamaa vichwani mwa watanzania wengi; Matokeo yake ikawa – Watanzania wengi wakawa wanaabudu UJAMAA openly and in public kuliko imani zao nyingine za kidini – hasa uislam na ukristo;

Je, nini kilichobadilika na kupelekea kukua kwa kasi la msuguano wa kidini nchini?

Kama nilivyojadili awali, katika kipindi kizima cha azimio la arusha (1967 – 1985), in public, watanzania waligeuka kuwa waumini wa dini ya Kiraia – UJAMAA, huku wakiendelea na imani zao mbalimbali katika maisha yao binafsi; na tumeshajadili japo kwa kiasi jinsi gani hili liliwezekana; Kilichogeuza hali yote hii ilikuwa ni ujio wa mageuzi ya kiuchumi baada ya Mwalimu kung’atuka mwaka 1985; Lakini kama tunavyoelewa, mageuzi ya Kisiasa yalichukua muda zaidi na hii ilikuwa ni kwa makusudi kwani hivyo ndivyo misingi iliyowekwa na ujamaa ingeweza kuwa sustained ili kuhakikisha kwamba transition ya nchi kutokea Ujamaa kwenda Ubepari na Soko Huria inatokea katika mazingira ya amani na utulivu; Swali la ku digest – je, Katiba ya Nchi (1977) na ya CCM kuendelea kutamka Ujamaa, lengo lake ni nini hasa?

Kufuatia Mageuzi ya kiuchumi na mageuzi ya kisiasa yanayozidi kushika kasi leo (hasa suala la katiba mpya), UJAMAA umebakia kuwa ni Nadharia (theory) zaidi huku kivitendo (practice), taifa likiendelea kukabiliwa na ombwe kubwa la Dira na Itikadi; Kutokana na ombwe hili, utulivu uliotokana na mafanikio ya Ujamaa kama DINI YA KIRAIA and a national expression ya watanzania, umepata mtikisiko mkubwa kwani matokeo ya ombwe hili ni publicly displayed religious expressions tofauti na enzi za Ujamaa; Kutokana na uwepo wa ombwe hili, leo, kila dini inajaribu to fill and dominate the re – opened public realm ambayo awali ilikuwa imefungwa na dini ya raia – UJAMAA; Ndio maana, leo hii it has become common practice kwa wakristo na waislam to challenge sera za serikali ya CCM waziwazi, hasa challenging mahusiano baina ya serikali and various sections of the society, kwani kila upande (ukristo na uislamu) unazidi kuamini kwamba wakizubaa, ombwe husika litajazwa na upande wa pili;

Baada ya Taifa kuhama kutoka state centred socialism to market oriented liberalism, leo hii kama taifa, tuna ‘ a multitude’ of religious expressions and institutions za kiislamu na kikristo, huku kila moja ikifanya kila linalowezekana kutafuta prominence and to challenge the state katika masuala mbalimbali hasa yalio socio – political and social-economic in nature; Ni muhimu tukaelewa kwamba - kutoweka kwa DINI YA URAIA – Ujamaa, kumeacha sio ombwe tu bali pia makovu mengi; ndio maana ni jambo la kawaida kwa dini hizi kuu mbili (uislamu na ukristo) kuwa na mivutano, sometimes violently; Kwa mfano, ni jambo la kawaida kwa waislamu kujadili jinsi gani historia ya nchi haijawatendea haki in terms of employment, leadership, education na political and economic opportunities kwa ujumla; Kuna hoja ya msingi katika mengi ya madai haya na kitendo cha kuyapuuzia ndio imekuwa ni moja ya key inputs za bomu ambalo limesha anza kutoa cheche;

Je, kumekuwa na juhudi gani za kutafuta ufumbuzi wa tatizo?

Kumekuwepo na juhudi mbalimbali ngazi ya taifa na kimataifa lakini kwa kiasi Fulani, juhudi hizi pia zimekuwa zinachangia kukua kwa tatizo kuliko kutatua tatizo; nitajitahidi kufafanua kama ifuatavyo

Moja ya interventions kubwa zenye nia ya kutafuta ufumbuzi juu ya suala hili ilikuwa ni initiative ya miaka kadhaa iliyopita iliyolenga to establish inter religious action and dialogue nchini Tanzania ambapo Taasisi kwa jina la Inter Religious Council of Peace in Tanzania (IRCPT) ilianzishwa na ina ofisi zake Mikocheni, Dar-es-salaam; Lengo la IRCPT ilikuwa ni kuwakilisha taasisi “zote” kubwa za dini Tanzania kama ifuatavyo: Muslims, Catholics, Protestants, African Traditional religions & minority religions of Asian origin; IRCPT ilikuwa na bado inaendelea kuwa the first and main official hub katio lengo husika; Kwa mujibu wa afisa mmoja wa IRCPT, taasisi hii ipo kwa ajili ya mambo yafuatayo:

  • To guard the peaceful societal relations and national unity attributed to Tanzania;
  • To play an advisory and advocacy role to the government of Tanzania on matters pertaining to societal interests, especially when religious expressions threatens the nation’s socio – political stability;

Kwa maana hii, IRCPT ni chombo cha kutuokoa kutoka kwenye janga linalotunyemelea, hivyo kuja kamati au tume mpya kila mara jambo linapotokea inaweza kuwa ni creation of unnecessary redundancy kwani tayari kuna chombo kilichoundwa kwa madhumuni hayo, tena chombo ambacho kinakaa meza moja na serikali kwa miaka mingi; Swali linalofuatia ni Je, kwanini chombo kama IRCPT kimeshindwa kuja na ufumbuzi wa kudumu?

Kwa utafiti wangu. Nimegundua tatizo kuu moja kuhusiana na IRCPT au any other initiative ambayo italenga kutafuta ufumbuzi juu ya mgogoro wa kidini Tanzania; IRCPT haipo representative kwani haitambui ALTERNATIVE MUSLISM AND CHRISTIAN ORGANIZATIONS AND INSTITUTIONS nchini; Kwa mfano, active members wa IRCPT ni Wakristo waliopo chini ya Tanzania Episcopal Conference (TEC) na Christian Council of Tanzania (CCT), na Waislamu waliopo chini ya BAKWATA, na pia minority religions of Asian origin; Alternative organizations and institutions za Wakristo na Waislamu ambao wana waumini wasiokuwa na mahusiano na CCT, TEC au BAKWATA na hata Dini nyingine za kienyeji (traditionally), wote hawa leo hii sio active members wa IRCPT; Na kuna kila dalili kwamba hali hii itaendelea kuwa hivi kila mara tume au kamati mpya zitakapoundwa kukabiliana na mgogoro wa kidini Tanzania; Wadau wa dini ambao wapo kwenye makundi haya wengi zaidi ya wale kwenye CCT, TEC na BAKWATA kwa pamoja, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwatambua na kuwahusisha katika majadiliano;

Tujadili kidogo the intra religious tensions ndani ya uislamu na ndani ya ukristo;

Ukristo

Kutokana na Ombwe katika public realm tulilojadili mapema ambalo liliachwa baada ya kutoweka kwa dini ya uraia i.e. UJAMAA kufuatia mageuzi ya kiuchumi miaka ya 1980s, kila kukicha kumekuwa na uibukaji wa taasisi mbalimbali za kikristo ambazo zimekuwa zinapigania wafuasi kutoka dini nyingine na zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika harakati hizo; Matokeo yake imekuwa ni mivutano ya chini kwa chini (kitaasisi) baina ya makundi makubwa ya wakristo hasa Wakatoliki na Protestants na alternative Christian organizations ambazo taasisi hizi kubwa mara nyingi imekuwa haizitambui rasmi; Lakini intra religious tensions ndani ya ukristo bado sio tatizo kubwa kama ndani ya uislaimu;

Uislamu

Ndani ya uislamu pia kuna intra religious tensions za muda mrefu sana ambazo tofauti na zile ndani ya ukristo, hizi za kiislamu zimeshakuwa public and in the open kwa muda mrefu; Tension kubwa iliyopo ni baina ya BAKWATA & BARAZA KUU; Tatizo lililopo ni kwamba enzi za Ujamaa, interest za waislamu wa Baraza Kuu zilikuwa catered ambapo walikuwa ni partners wa one party state kama taasisi nyingine za kikristo na kiislamu; Lakini since the demise of Ujamaa, ni Bakwata pekee ndio imekuwa inajulikana as the only legitimate organization that represents the interests of Muslims in Tanzania;

Matokeo yake ni kwamba Baraza Kuu kama taasisi ambayo ina wafuasi wengi, hoja na mawazo yao mengi yamekuwa yakipuuzwa na wamekuwa hawashirikishwi katika maamuzi mengi; Iwapo inatokea hivyo, kwani tushangae wanapoamua kufuata njia za ki-harakari? Na ni kawaida kusikia hoja kwamba BARAZA KUU lipo too political, hivyo kuwa kinyume na Katiba lakini pia national security interests wakati ukweli uliopo ni kwamba Bakwata is more political kwani iliundwa to fulfill political interests za TANU/CCM; Ni kwa bahati mbaya sana kwamba hoja za Baraza KUU huwa zinatazamwa kwa jicho la mashaka wakati wote; Kumekuwa na makosa makubwa ya kuita Baraza Kuu as extremists au fundamentalists, na kwamba wanachanganya dini na siasa kinyume na Katiba;

Ningependa kumalizia kwa hoja kuu tatu:

Kwanza, kama wadau wa IRCPT chombo ambacho ni mshauri mkuu wa serikali ya CCM katika masuala ya mahusiano mazuri ya kidini nchini, kitendo cha Tanzania Episcopal Conference (TEC) na Christian Council of Tanzania (CCT) na BAKWATA (kama wadau wakuu wa IRCPT) to marginalize, perceive and sometimes describes alternative Muslim organizations (e.g. Baraza Kuu) and Christian organizations in terms of religious extremists whose action threatens our socio – political stability, ni kosa kubwa sana na linachochea badala ya kutibu mgogoro wa kidini nchini; Kwa maana nyingine, taifa letu halipo katika mgogoro wa kidini kutokana na uwepo wa alternative Muslim and Christian religious organizations bali ni kwa sababu ya attitude ya large religious organizations za kiislam na kikristo (TEC, CCT, BAKWATA) towards alternative Muslim and Christian religious organizations in Tanzania; Tukumbuke pia kwamba Inter Religious Council of Peace in Tanzania (IRCPT) ndio the largest hub inayotambulika rasmi kuwakilisha waumini wa dini zote Tanzania na ndio mshauri mkuu wa Serikali ya CCM katika suala zima la kudumisha amani na utulivu katika mazingira ya diversity katika imani za kidini miongoni mwa watanzania;

Pili, kuna aina kuu mbili za migogoro ya kidini katika taifa letu, kwanza ni migogoro ndani ya madhehebu (yani islam na Christianity), na pili ni migogoro baina ya dini kuu mbili za kiislamu na kikristo; Ni ni muhimu tukaelewa hili vizuri iwapo kweli tuna ni aya kutafuta permanent solution ya mgogoro husika; Uwepo wa migogoro hii katika Tanzania ya leo ni ishara ya nini? Kwanza - ni ishara kwamba huu ni Mwanzo wa 'a renewed secularization process' kukidhi mahitaji ya mfumo mpya wa kiuchumi na kijamii yani market oriented liberalism tofauti na state centred socialism ambayo ilifanikiwa kujenga ujamaa kuwa dini ya raia; Swali linalofuatia ni je - Serikali ya CCM itasimamia vipi suala hili katika mchakato wa Katiba Mpya, ikizingatiwa kwamba hadi sasa (mwaka 2013), mfumo rasmi wa kiuchumi na kijamii kwa mujibu wa katiba ya Tanzania (1977) ni Ujamaa?

Na Tatu, kinachoendelea hivi sasa pia inaweza kutafsiriwa kama ni mchakato huu wa re-secularization of the state kutokana na ombwe lililoachwa na Dini ya Raia (Ujamaa); Hii ni changamoto kubwa sana on the whole issues of Power Relations in contemporary Tanzania, power ambayo kwa muda mrefu imekuwa mikononi mwa the Supreme Islamic Council of Tanzania (Bakwata), Tanzania Episcopal Conference (TEC) & Christian Council of Tanzania (CCT), chini ya ufundi, ustadi na uangalifu mkubwa wa CCM in the NAME and in the GAME of a SECULAR STATE; Itambulike kwamba ingawa wapo watu na taasisi zinazofaidika na power relations za sasa, ukweli unaendelea kubakia wazi kwamba tatizo la ombwe la itikadi na dira kutokana na kutoweka kwa dini ya raia (Ujamaa) linazidi kuwa kubwa na linakaribia kuipasua Tanzania vipande vipande; Hii ni kwa sababu, Ombwe hili kwa sasa linagombaniwa na taasisi zote za kidini (waislamu na wakristo), huku zile kubwa - Bakwata, Tanzania Episcopal Conference (TEC) na Christian Council of Tanzania (CCT), zikiendelea kuziminya na kuzi marginalize alternative religious organizations za Kislamu na Kikristo na kiislamu nchini; Swali linalobakia ni je – Serikali ya CCM itamudu vipi misuguano hii bila ya kuathiri mtaji wake wa kisiasa - in the name and game of a secular state?
 
Lugha gani hii? Andika kwa lugha moja ambayo unaridhika nayo, vinginevyo uchambuzi wako haueleweki.
 
Waliokandamizwa na kuzibwa midomo kwa muda mrefu sasa washajua wanakandamizwa na wameanza kudai haki zao.Ni muhimu kwa serikali kutoa haki sawa kwa wote.Serikali iache kukumbatia baadhi ya taasisi na kuziacha zingine.
 
Lugha gani hii? Andika kwa lugha moja ambayo unaridhika nayo, vinginevyo uchambuzi wako haueleweki.

Nazidi kujitahidi kuongeza uwezo wangu wa kuandika kwa lugha ya kiswahili kama kugha yangu ya taifa lakini yapo masuala ambayo kwa kweli kwangu binafsi huwa nashindwa kuya express kwa kiswahili kufikisha ujumbe naokusudia, hasa kutokana na uhaba wa literature katika masuala husika kwa kiswahili; Iwapo hauna tatizo na yaliyopo kwenye mada na imekuvutia na kwamba tatizo ni mtoa mada kutoeleweka vizuri kutokana na kuchanganya lugha ya kiingereza na kiswahili, una nafasi ya kuuliza maswali kwani maswali ni sehemu ya mjadala, na mimi au wengine wenye uelewa watatoa ufafanuzi, vinginevyo hutaki, unaacha;
 
Waliokandamizwa na kuzibwa midomo kwa muda mrefu sasa washajua wanakandamizwa na wameanza kudai haki zao.Ni muhimu kwa serikali kutoa haki sawa kwa wote.Serikali iache kukumbatia baadhi ya taasisi na kuziacha zingine.

Haswa, kwani hili ni moja ya sehemu kubwa sana za tatizo husika;
 
Mradi huu uliolenga to secularize the state na kugeuza Ujamaa kuwa DINI YA KIRAIA ulichukua sura kuu mbili: Kwanza – Serikali ya TANU iliagiza taasisi zote za Kiislam kutochanganya dini na siasa; Lakini Pili, Serikali ya TANU pia ilihimiza baadhi ya taasisi za dini ya Kikristo kushiriki katika shughuli za maendeleo; Hili la pili lilikuwa ni kutengeneza bomu la kulipuka baadae, vinginevyo kwa ujumla wake, watanzania wengi waliendelea kuridhika na sera za TANU zilizolenga kujenga nchi katika mazingira ya usawa, umoja, udugu na mshikamano;

hongera sana mchambuzi kwa uzalendo wako....

mimi ni hapo kwenye red........ je mhimizo wa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo haukuzihusu taasisi ambazo hazikuwa za kikristo?........ au ni habari za kuendekeza wali wa brauni ambao ndio unaotumika kwenye kura za maoni?
 
Ninamengi ya kujadili na mchambuzi sijamuelewa vema, kuna kutupoteza.

Ukisoma alivoanza kwa maana ya utanzania na kuweka pembeni ushabiki nadhani Mchambuzi

amepotea sehem nyingi na kuingiza ushabiki ngoja nipitie upya kisha nitakuja na yale nadhani ameyajadili kwa ushabiki

na kuiweka kweli pembeni.
 
Last edited by a moderator:
Kama wewe ni mwana CCM basi mmeshaanza kusema ukweli ambao hua mnajifanya hamuujui, CCM ndio maprofessor wa kuleta matatizo nchi hii!!!

Tena nasikia hua mnapelekwa ugaibuni kusomea jinsi ya kuhujumu watanzania kwa ustadi wa hali ya juu.
 
Una ujumbe muhimu sana lakini nadhani uzi huu utahamishiwa ktk room nyingine!
 
kwa hiyo ndo kusema hujui lugha yako ya taifa vizuri? au ndo usharubaro wa wabongo akiongea kingereza ataonekana amesoma wakati kingereza ni lugha tu kama lugha nyingine tuache utumwa wa kusamini zaidi vitu vya wenzetu badala ya vyakwetu ndio matokeo yake kila siku tunajiona hatuwezi na hatujui tunabaki kuamini kuwa hata kuzaliwa mwafrika ilikuwa ni makosa ulitakiwa kuzaliwa mzungu ndio ungekuwa umekamilika. Hivi neno kama literature ukisema ni machapisho kunaubaya gani? jirekebisheni bwana acheni kujizalilisha kwa kuongea kiswanglish kama unajua unajua tu si lazima ujishaue kujionyesha kuwa unajua
 
uchambuzi wako ni mzuri ila kubwa ambalo waislamu wamekua wakilalamikia ni upendeleo wa serikali kwa wakristu huku ikiwaacha waislamu. angalieni mifano ifuatayo;
1- waislamu wamekua wakilalamikia serikali kutotambua siku ya ijumaa kama siku ya ibada. wakristo wana jumapili lkn waislamu waliyo wengi wamekua wakishindwa kufanya ibada kutokana na ijumaa kuwa siku ya kazi. wameomba pia kama inawezekana angalau saa 5 na nusu hadi saa nane uwe muda rasmi wa kuwaruhusu waislamu kwenda kufanya ibada siku za ijumaa. la ajabu hadi bunge huendelea na mijadala mida ya adhuhuri siku za ijumaa.
2- waislamu wamekua wakilalamikia upendeleo uliyofanywa na serikali kwa kuingia mkataba na TEC na CCT. mkataba huo unajulikana kama MEMORANDUM OF UNDERSTANDING. waislamu wanajiona kama mtoto ambaye anawekwa kando huku kaka yake akiendelezwa kwa kupewa mtaji wa biashara.
3- waislamu wamekua wakilalamikia kutopata fursa ya kuwa na mahakama za kadhi zinazotambulika rasmi kikatiba. wamefafanua kuwa mahakama a kadhi itahusu mirathi, ndoa, talaka na wakfu. mambo ya jinai hayamo kwenye mahakama ya kadhi. licha ya mambo haya kuwa IBADA kwa waislamu, wakristo wamekataa katakata uanzishwaji wa mahakama ya kadhi. waislamu kwa upande wao wameona kuwa wanaingiliwa katika ibada yao. wametoa mifano kuwa uganda. afrika ya kusini, uingereza nk... kuna mahakama za kadhi licha ya hizi nchi kuwa na idadi ndogo za waislamu.
4- waislamu waliwahi kushauri nchi yetu ijiunge na oic. walieleza faida za kujiunga na oic kiuchumi. wakristo wakamekataa suala la oic. wanasema nchi haina dini. haiwezi kusajiliwa kuwa ya kiislamu. uganda, msumbiji nk... ni wanachama wa oic.
5- waislamu wamelalamikia NECTA kuwa na viongozi wakristo watupu. hakuna muislamu pale. muislamu kama yupo atakua mfagiaji. mwaka juzi na jana, ilibainika kuwa watoto wa kiislamu walifelishwa mtihani wa islamic knowledge. NECTA walikira na kusema kuwa ni kosa la kikompyuta. hakuna akiejiuzulu!
6- waislamu wamelalamikia kuwekwa kando katika ajira ya umma. wanasema kuwa wakristo ni wengi maofisini. wanaendelea kubebana licha ya kuwepo waislamu wenye sifa. baadhi ya ofisi za serikali zinaonekana kama parokia. wameombwa pawe na mpango mkakati wa kuwachomeka kwenye ajira serikalini (wenye sifa) ili angalau nao washiriki katika matunda ya keki ya taifa.
7- waislamu wanasema wamekua kwa miaka mingi wakichukuliwa kama minority group. ktika sensa ya mwaka jana, waliomba kiwekwe kipengela cha sensa ili ukweli wa idadi ya watu kidini ujulikane. walitoa mfano kuwa inasemekana wakristo ni wengi. hivyo, inapopangwa mipango ya maendeleo kwa mfano ardhi kwa ajili ya nyumba za ibada na maziko, wakristo hupewa maeneo makubwa kwa madai kuwa ni wengi.
8- waislamu wamekuwa wakilalamika kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa mfumo kristo. wanasema kipindi cha sikukuu, ofisi za serikali hupambwa muda wa sikukuu za wakristo. sikukuu za waislamu hakuna kinachofanyika!
9- kama ulivyo sema, waislamu wanalalamika kuwa serikali imekua ikiikumbatia sana BAKWATA na kudharau taasisi nyingine za kiislamu. BARAZA KUU ni taasisi yenye waislamu wengi hapa nchini kuliko bakwata. serikali huwa haiipi taasisi ya baraza kuu uzito wowote.

MY TAKE
kundi katika jamii linaposononeka kwa muda mrefu, hukata tamaa. baada ya kukata tamaa kupoteza imani na serikali yao. waislamu wanaamini kuna urafiki mkubwa kati ya serikali na ukristo. hali hii inawafanya wawachukie wakristo wakiwaona kuwa wabaya wao. hoja ya kusema rais, makamu, rais na wakamu wawili wa znz, igp, jaji mkuu kuwa wote ni waislamu haina mashiko. hawa siyo watendaji mkoa, wilaya, kata hadi kijiji. mfumo wanasema ni wakikiristo. hata kama viongozi wa juu watakua waislamu, hilo ni kiini mamcho.

nashauri upande wa wakristo watambue na kutafakari madai ya waislamu kuliko kuwadhihaki kuwa "wala ubwabwa hao, wavaa kanzu hao, wavaa msuli hao..........". kuwadhihaki ni kungeza mpasuka ambao unafanya amani na umoja vizidi kutoweka.
 
Pia katika ujenzi wa secular state nchi ilishindwa kukwepa kitanzi cha udini na ukabila kwa kutokuondoa vipengele hivyo kwenye taarifa mbalimbali za kiofisi au kinamii. Hali hii imepelekea baadhi jamii kuanza kuhesabiana mwa lengo la kujua idadi yao.

Pia serikali haikujipanga juu ya matumizi ya majina ya kidini kwani nayo yanaongeza changamoto.
 
kwa hiyo ndo kusema hujui lugha yako ya taifa vizuri? au ndo usharubaro wa wabongo akiongea kingereza ataonekana amesoma wakati kingereza ni lugha tu kama lugha nyingine tuache utumwa wa kusamini zaidi vitu vya wenzetu badala ya vyakwetu ndio matokeo yake kila siku tunajiona hatuwezi na hatujui tunabaki kuamini kuwa hata kuzaliwa mwafrika ilikuwa ni makosa ulitakiwa kuzaliwa mzungu ndio ungekuwa umekamilika. Hivi neno kama literature ukisema ni machapisho kunaubaya gani? jirekebisheni bwana acheni kujizalilisha kwa kuongea kiswanglish kama unajua unajua tu si lazima ujishaue kujionyesha kuwa unajua

Hutaki, unaacha, hauna haja ya kuanza malumbano juu ya lugha ya kiingereza na usomi; Kwa maneno haya sina maana ya kukukatisha tamaa juu ya hoja yako kwani ukija na uzi mzuri juu ya mada ya kiingereza na usomi, wengi tutashiriki kwani hakika utakuwa ni mjadala wenye manufaa kwetu sote; Vinginevyo kama hauelewi yaliyomo kwenye uzi huu na hauoni haja ya kuliza ufafanuliwe na wadau wengine, lakini muhimu zaidi, iwapo yaliyomo hayakupi hamasa yoyote ya maana, kuna mada nyingine nyingi za kushiriki, pengine tutakutana huko;
 
kwa hiyo ndo kusema hujui lugha yako ya taifa vizuri? au ndo usharubaro wa wabongo akiongea kingereza ataonekana amesoma wakati kingereza ni lugha tu kama lugha nyingine tuache utumwa wa kusamini zaidi vitu vya wenzetu badala ya vyakwetu ndio matokeo yake kila siku tunajiona hatuwezi na hatujui tunabaki kuamini kuwa hata kuzaliwa mwafrika ilikuwa ni makosa ulitakiwa kuzaliwa mzungu ndio ungekuwa umekamilika. Hivi neno kama literature ukisema ni machapisho kunaubaya gani? jirekebisheni bwana acheni kujizalilisha kwa kuongea kiswanglish kama unajua unajua tu si lazima ujishaue kujionyesha kuwa unajua
Mkuu Mchmbuzi, nadhani unaeleweka kwa jinsi unavyoelezea mada zako.

Kama kuna mapungufu ni ya mtu binafsi. Labda ungemuuliza Kasuku hivi kiswahili cha '' Market oriented liberalism' inawekwaje kwa lugha yetu. Hata tukiandika kiswahili bado kuna malalamiko. Lazima watu watambue kuwa lugha yetu haijajitosheleza na wala hakuna lugha iliyojitosheleza duniani kwa asilimia 100.

Ukisema Bureau de change mtu atadhani hicho ni kiingereza kama atakavyodhani de facto au mutatis mutandis ni kiingereza.Hili lisitutoe katika mada na liachwe kwa kila mmoja.

Pili, mada ya Mchambuzi ipo katika analysis zaidi ya tuhuma au malalamiko. Hata kama mtu ataorodhesha tuhuma au malalamiko 1000 bado tutarudi kwenye analysis. Bila analysis ni ngumu sana kupata solution ya tatizo.

Niwaombe wanajamvi tukabiliane na hoja kwa kukubaliana au kupingana kwa mantiki na hekima.

Mchambuzi kuna sehemu nakubaliana nawe kama nisivyokubalina na nyingine.
Nitarajea kuziangalia hoja zako za kufikirisha.
 
Tofauti za kidini zitaendelea kuwepo katika mfumo wowote wa maisha yetu ya kisiasa na kiutawala. Hii ni kwa sababu dini hizi zenyewe zina uasili wa ushindani na tofauti za kimaono. Lakini kubwa ni kuwa dini hizi zote (uislamu na ukristu)zinaubiri jinsi ya kuishi hapa duniani Kama njia ya kufikia maisha ya kheri mbinguni. Jinsi gani ya kuishi hapa duniani na njia ya kueneza dini hizo ndipo tofauti zinapojitokeza.

Kwangu mimi si aina ya mfumo wa utawala wetu bali wasimamizi tuaowachagua kutuongoza wanapaswa kutuunganisha (katika tofauti zetu za kiimani) Kama taifa moja lenye Imani moja ya utaifa wetu. Tatizo tulilonalo ni kuwa watawala (Serkali na chama) wameshidwa na wana woga wa kuchukua hatua staiki zitakazohakikisha utaifa wetu unadumu. Sababu kubwa inatokana na woga wa kuodolewa katika utawala katika siasa hizi za ushindani. Lakini pia inatokana na watawala wenyewe (Kama watu binafsi) kuweka mbele Imani zao za dini kuliko ujenzi wa utaifa wetu.
 
uchambuzi wako ni mzuri ila kubwa ambalo waislamu wamekua wakilalamikia ni upendeleo wa serikali kwa wakristu huku ikiwaacha waislamu. angalieni mifano ifuatayo;
1- waislamu wamekua wakilalamikia serikali kutotambua siku ya ijumaa kama siku ya ibada. wakristo wana jumapili lkn waislamu waliyo wengi wamekua wakishindwa kufanya ibada kutokana na ijumaa kuwa siku ya kazi. wameomba pia kama inawezekana angalau saa 5 na nusu hadi saa nane uwe muda rasmi wa kuwaruhusu waislamu kwenda kufanya ibada siku za ijumaa. la ajabu hadi bunge huendelea na mijadala mida ya adhuhuri siku za ijumaa.
2- waislamu wamekua wakilalamikia upendeleo uliyofanywa na serikali kwa kuingia mkataba na TEC na CCT. mkataba huo unajulikana kama MEMORANDUM OF UNDERSTANDING. waislamu wanajiona kama mtoto ambaye anawekwa kando huku kaka yake akiendelezwa kwa kupewa mtaji wa biashara.
3- waislamu wamekua wakilalamikia kutopata fursa ya kuwa na mahakama za kadhi zinazotambulika rasmi kikatiba. wamefafanua kuwa mahakama a kadhi itahusu mirathi, ndoa, talaka na wakfu. mambo ya jinai hayamo kwenye mahakama ya kadhi. licha ya mambo haya kuwa IBADA kwa waislamu, wakristo wamekataa katakata uanzishwaji wa mahakama ya kadhi. waislamu kwa upande wao wameona kuwa wanaingiliwa katika ibada yao. wametoa mifano kuwa uganda. afrika ya kusini, uingereza nk... kuna mahakama za kadhi licha ya hizi nchi kuwa na idadi ndogo za waislamu.
4- waislamu waliwahi kushauri nchi yetu ijiunge na oic. walieleza faida za kujiunga na oic kiuchumi. wakristo wakamekataa suala la oic. wanasema nchi haina dini. haiwezi kusajiliwa kuwa ya kiislamu. uganda, msumbiji nk... ni wanachama wa oic.
5- waislamu wamelalamikia NECTA kuwa na viongozi wakristo watupu. hakuna muislamu pale. muislamu kama yupo atakua mfagiaji. mwaka juzi na jana, ilibainika kuwa watoto wa kiislamu walifelishwa mtihani wa islamic knowledge. NECTA walikira na kusema kuwa ni kosa la kikompyuta. hakuna akiejiuzulu!
6- waislamu wamelalamikia kuwekwa kando katika ajira ya umma. wanasema kuwa wakristo ni wengi maofisini. wanaendelea kubebana licha ya kuwepo waislamu wenye sifa. baadhi ya ofisi za serikali zinaonekana kama parokia. wameombwa pawe na mpango mkakati wa kuwachomeka kwenye ajira serikalini (wenye sifa) ili angalau nao washiriki katika matunda ya keki ya taifa.
7- waislamu wanasema wamekua kwa miaka mingi wakichukuliwa kama minority group. ktika sensa ya mwaka jana, waliomba kiwekwe kipengela cha sensa ili ukweli wa idadi ya watu kidini ujulikane. walitoa mfano kuwa inasemekana wakristo ni wengi. hivyo, inapopangwa mipango ya maendeleo kwa mfano ardhi kwa ajili ya nyumba za ibada na maziko, wakristo hupewa maeneo makubwa kwa madai kuwa ni wengi.
8- waislamu wamekuwa wakilalamika kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa mfumo kristo. wanasema kipindi cha sikukuu, ofisi za serikali hupambwa muda wa sikukuu za wakristo. sikukuu za waislamu hakuna kinachofanyika!
9- kama ulivyo sema, waislamu wanalalamika kuwa serikali imekua ikiikumbatia sana BAKWATA na kudharau taasisi nyingine za kiislamu. BARAZA KUU ni taasisi yenye waislamu wengi hapa nchini kuliko bakwata. serikali huwa haiipi taasisi ya baraza kuu uzito wowote.

MY TAKE
kundi katika jamii linaposononeka kwa muda mrefu, hukata tamaa. baada ya kukata tamaa kupoteza imani na serikali yao. waislamu wanaamini kuna urafiki mkubwa kati ya serikali na ukristo. hali hii inawafanya wawachukie wakristo wakiwaona kuwa wabaya wao. hoja ya kusema rais, makamu, rais na wakamu wawili wa znz, igp, jaji mkuu kuwa wote ni waislamu haina mashiko. hawa siyo watendaji mkoa, wilaya, kata hadi kijiji. mfumo wanasema ni wakikiristo. hata kama viongozi wa juu watakua waislamu, hilo ni kiini mamcho.

nashauri upande wa wakristo watambue na kutafakari madai ya waislamu kuliko kuwadhihaki kuwa "wala ubwabwa hao, wavaa kanzu hao, wavaa msuli hao..........". kuwadhihaki ni kungeza mpasuka ambao unafanya amani na umoja vizidi kutoweka.

Hayo masuala yaliyokuwa raised hapo juu.......kwa namna fulani ninaomba yawekwe kama "sticky" as FQA i.e. frequent asked questions........kw akumbukumbu zangu maswali hayo yote yalishatolewa majibu.........

Kuhusu NECTA kwa mfano....kuna mtu kaelezea kuwa kuwa na Viongozi wakuu wa Serikali wote ni Wailsam....ni kiini macho.......in the same way mwingine anaweza kusema kuwa na viongozi wakristo watupu NECTA ni kiini macho........

The point is......binafsi nimepitia elimu iliyodaiwa waislamu walihujumiwa kwani yalitumika majina na wala si namba......hilo nikalikanusha.......nikaambiwa wewe ulipita/penya kwenye ufa!!......nilipata kazi...wala sikushikwa mkono wala nini.....na yenyewe nikaambiwa nilipenya kwenye ufa......

Pale NECTA kuna marafiki zangu.......kama hamujui ni jinsi gani NECTA inafanya kazi ni bora kuuliza......kuna watendaji wa dini zote pale........na nilishawahi kupita pale.....kwenye kamati kadha wa kadha.......hizi assumptions kuwa eti kuna upendeleo si kweli....HAKUNA!.....tuache kusikiliza uzushi wa Mohamed Said et al ............ni UONGO MTUPU......nilimuambia Mohamed Said kwamba kuhusu suala la mitihani na madai yake kuhus Wizara ya Elimu na Baraza la mitihani ni UONGO........kwani mimi nimepitia sehemu hizo........na aliyokuwa akiyadai.....si KWELI.......
 
Mkuu Mchambuzi,
Umeeleza mengi na muhimu.
Mimi nichangie kwa uchache sana ya kuwa tatizo tulilo nalo sasa hivi linatokana na mambo kadha wa kadha na wala si sababu moja.

1. Kuhusu dhana nzima ya siasa nakubaliana na hoja zako na naongezea kuwa tulipoacha mifumo yetu tukaamua kuingia katika soko huria hili lililonekana wazi.

Mfumo wa soko huria si katika biashara tu bali kila kitu. Kwamba tunatakiwa tufuate masharti ikiwa ni pamoja na yale ya haki za binadamu ambayo sisi tulikuwa nazo lakini zinatakiwa zile kutoka nje.

Uhuru wa kuabudu ulikuwepo hata kabla ya ukoloni lakini tunaambiwa lazima tutoe uhuru huo hata kwa wendawazimu kwasababu wao ni sehemu ya jamii na tusipofanya hivyo basi hatutafikia ''true market oriented state''

2. Kutokana na hilo hapo juu, tulijikuta tunakumbatia mfumo wa soko huria kwa mtindo wa soko holela.
Hapo ndipo vikazuka vikundi vya dini ambavyo vingine vimethibitika kutokuwa vya dini bali vya kitapeli the least to say
Serikali haikujiandaa kukabiliana na hali hiyo na hapa ndipo tulipo, tunatafuta band aid badala ya dawa.

3. Udhaifu wa serikali. Tatizo hili halikuzuka siku moja. Tumeona tension kati ya dini mbili ikikua siku hadi siku.
Haii haina maana hakukuwepo na tension siku za nyuma, la hasha! ilikuwepo lakini kulikuwepo na willing ya kukabiliana nayo. Na hiyo ilifanywa na viongozi walioweka masilahi ya taifa mbele na wala si yao.

Viongozi wa serikali iliyopo walijua kuwa kuna uchochezi, vurugu n.k. Kwa bahati mbaya wao waliweka masilahi yao mbele masilahi ya umma nyuma.
Haiwezekani video au vyombo vya habari vipalilie chuki na serikali ikae kimya. Walijua lakini nani athubutu.

3.Nani athubutu ikiwa uwepo wake madarakani ulitegemea sana hoja za kufurahisha wanadini na si Watanzania?
Ni kwasababu kama hizo wanasiasa wakachukua fursa ya udhaifu huo kutafuta ulaji wao.
Angalia ndani ya bunge hoja za kitaifa zinajadiliwa tena katika ''cauccus'' za vyama.

Kuna nyakati hata wabunge wa CCM walitishiwa kufukuzwa kama hawakubaliani na maagizo ya serikali.
Leo wabunge hao hao wamegawanyika kidini na siyo chama tawala au vya upinzani vilivyofanya caucuss kujalili msimamo wa pamoja. Hii maana yake ni kuwa ndani ya chama kama CCM tayari kuna ufa, na ufa huo upo serikalini sasa nani wa kulikabili tatizo. Yote haya ni matatizo ya udhaifu wa uongozi.

4.Kuhusu tume ya pamoja ya ushirikiano, nalo pia nakubaliana nawe kuwa badala ya kuwa na tume kila uchao, basi interfaith ingepewa nguvu zaidi ili tujue tunadili na makundi mawili au matatu kuliko utitiri wa vikundi.

5. Hili la waislam kuwa na mzozo na BAKWATA, nadhani ili kuondoa simtofahamu na vurugu ni vema serikali ikavunja BAKWATA na kuwaachia waislam waunde baraza lao moja kutoka katika vikundi tofauti. Ni kwa kupitia hapo tutakuwa na uwezo wa kuwa na viongozi responsible na watakaobeba dhamana na wala si kukimbizana na mtu mmoja mmoja.

6. Kwamba, kiongozo wa taifa atakayeshindwa kukemea achilia mbali kuchukua hatua za kukabiliana na vikundi vya dini basi yeye abebe dhamana kwanza kabla ya mtu mwingine.
 
Mkuu ngurivi3,

Asante kwa mchango wako bandiko namba 18; Kimsingi nakubaliana na hoja zako zote katika bandiko husika, na baada ya kuzi digest, kuna suala moja ambalo limejitokeza at least ndani mawazo yangu, nalo ni kwamba: Ni ya Ujamaa ilikuwa ni kutibu the inequalities na injustices zilizotokana na mfumo wa kikoloni ambao msingi wake ni ubepari na elements zake zote; Kuanzia mwaka 1967 (Azimio la Arusha), kilichojiri ni political will ya uongozi wa nchi pamoja na commitment ya uongozi pamoja na resources za nchi katika ku address tatizo la injustices and inequalities ndani ya jamii ya Tanzania, lakini haina maana kwamba Ujamaa ulitatua tatizo husika; Kinachokosekana leo ni hiyo political will and commitment ambayo kama ingekuwepo, misuguano hii ingepungua sana hata kama injustices and inequalities zingeendelea kuwepo;

Tofauti na zamani ambapo injustices and inequalities zilikuwa zinaangaliwa na jicho la Ujamaa, leo hii the same injustices and inequalities zinaangaliwa kwa jicho la udini na ukabila katika kila nyanja na pia sehemu nyingi za vyombo vya maamuzi kama vile bunge, vyama vya siasa, ikulu n.k; Hii ni kutokana na ujio wa itikadi ya uliberali ambayo kama ulivyojadili imeachia karibia kila kitu kiwe determined na nguvu ya soko; Kutoweka kwa ujamaa kama itikadi imeleta ombwe kubwa la kiitikadi ambalo itikadi mpya ya uliberali imeshindwa kuliziba ipasavyo, hasa kutokana na ukweli kwamba itikadi hii haina interest to address inequalities and injustices ndani ya jamii; Matokeo yake ni kwamba sio bunge, ikulu, wala vyama vya siasa vina interest ya kujenga na kusimamia national value system ambayo ingelenga to address such issues kwa vitendo; isitoshe, hakuna a common answer kutoka kwa taasisi hizi juu ya nini ni value system yetu kama taifa zaidi ya porojo za amani na utulivu ambazo in principle, ni value system iliyojengwa na itikadi ambayo has been abandoned miaka mingi iliyopita; ni uulimbukeni kwa viongozi kuzungumzia amani na utilivu na jinsi gani tuvitunze as if vitu hivi vimejengwa na itikadi ya uliberali wakati ukweli ni kwamba vilijengwa na ujamaa ambao viongozi hawa wanaukwepa kama ukoma, na uongozi na mapenzi yao yasio na mipaka juu ya itikadi ya uliberali umekuwa unaendelea kuyabomoa haya tena kwa usimamizi mahiri sana wa viongozi hawa hawa wa CCM;
 
Scramble, kwa mujibu wa bandiko lako namba 11, nakubaliana na wewe kwamba sasa ni wakati wa kuyachukulia seriously madai husika badala ya kuendelea kuyapuuzia, lakini ningependa kujua msimamo wako juu ya madai gani unaunga mkono na kuona yana mashiko na madai yepi hauyaungi mkono na kwa hoja zipi;

Ogah amejadili suala la NECTA katika bandiko lake namba 16 lakini ukweli ni kwamba mgogoro husika ni mpana zaidi ya hoja hizi za NECTA; Ni muhimu tukajerea kwenye historia ya nchi yetu ili tuone ni wapi tuliteleza; Ningependa kuuliza maswali yafuatayo ili kwa pamoja tuyajadili:

Kwanza - Je, nini ni kiini cha mgogoro huu (kihistoria) - je ni educational inequality baina ya waumini kwa kislamu na kikristo au kuna mengine ya msingi zaidi?

Pili - lawama kwa historia pamoja na mipaka yake ni katika yepi zaidi kati ya haya mawili - je ni Ukoloni and western civilization au Ujamaa? Kwa hoja zipi?

Tatu - je - iwapo taifa lingefuata mfumo wa kibepari na soko huria kuanzia uhuru hadi leo (bila kupitia ujamaa), hali ingekuwaje? kungekuwa na unafuu katika tatizo husika?

cc: nguruvi3
 
Back
Top Bottom