Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mkuu Mchambuzi,
Nilipendelea sana kuiangalia mada yako kwa mtazamo mpana, hata hivyo ikibidi nitakuwa naingiza specifics pengine kuleta maana zaidi ya kile nilichokusudia.
Siku za nyuma mtu alikuwa akiitwa mdini ni tusi na kosa. Tuliona viongozi wa dini wakiweka mipaka ya ndimi zao, mafundisho na vitendo katika ulingano. Na kama ulivyosema ujaama ulijaribu sana kuweka hali ikaonekana kuwa sote tulikuwa na adui wakubwa akina ujinga, maradhi na umasikini. Hili umelieleza vema na nisingependa kulirejea.
Uliberali unatoa fursa ya kila kitu kuwa huru na kuamuliwa na soko. Ni nguvu hiyo ambayo tumeipokea bila matayarisho imetufikisha hapa tulipo. Tukakurupuka kuondoa miiko ya uongozi ambayo ilisaidia sana katika vetting ya viongozi bora.
Tukaruhusu kila mtu kuanzisha dhehebu au dini yake kwasababu huo ndio msingi wa uliberali na kwamba nguvu ya soko ndiyo inayoamua.
Kwa kuondoa miiko ya uongozi na maadili ambazo zilikuwa ni thamani zetu '' value'' nguvu ya mfumo wa kiliberali ikachukua mkondo wake. Kwa vile nguvu hiyo huamuliwa na soko, ni soko hilo hilo likawavuta viongozi wa kisiasa. Kwamba, ili wapate uongozi ni lazima waiitike nguvu ya soko ambayo tayari imeshachafuliwa na wajinga wachache.
Ndipo viongozi wakafuata msemo'' if you can't beat them join them.
Viongozi wanaopatikana kwa njia hiyo hawawezi kusimama na kukemea udini kwasababu udini ndiyo nguvu ya soko iliyowapa ulaji. Hapa ndipo tunaona sehemu muhimu kama bunge ikigawanyika kwa misingi ya udini.
Huwezi kuwa na serikali imara ukishakuwa na bunge la hovyo.
Lakini si bungeni, hata kwenye vyama kila mtu anaangalia nguvu ya soko. Ni kwa msingi huo hata chama tawala kimebaki kutoa statement ambazo hazionyeshi suluhu bali kutaka kupendeza kila mmoja.
Yote haya ninaweza 'wrap up'' kwa hoja kuwa uongozi uliopo ni dhaifu sana na umeacha mianya mingi ikiwa ni pamoja na kutupa thamani za taifa.
Leo ukiwauliza sisi kama taifa ni thamani zipi zinatuweka pamoja, wote watakimbia amani na utulivu.
Na kama ulivyosema hawajui kuwa hivyo viliundwa havikuremeka kama mvua. Hawajishughulishi kujiuliza tatizo liko wapi wamebaki kupiga porojo. Hakuna, si ndani ya chama tawala, serikali au bunge. Ikifika hapo ujue kuna tatizo tena kubwa.
Kuhusu maswali yako kwa scramble labda tumpe nafasi ayajibu ili pengine tuone mtazamo wake tofauti.
Kitu kimoja ninachotaka kusema ni kuwa suluhu ya tatizo iangaliwe kuanzia mzizi yake na wala si dalili.
Scramble ameorodhesha mambo mengi, moja ya hoja zake ni ile ya 6 kuhusu ajira za umma.
Scramble anasahau kuwa ajira za umma katika mfumo wa free market ni kitu kidogo sana.
Katika mfumo wa uliberali ni nguvu ya soko tu itakayoamua. Itafika siku kutakuwa na malalamiko makampuni yanaajiri wakristo wengi. Watu watakuwa wamesahau kuwa ni nguvu ya soko inayoamua si watu kama ilivyokuwa nyakati za ujamaa. Tena nguvu hiyo inaweza kuamua ajira apewe Mkenya, Mmalawi n.k.
Nikidokoa hoja moja ya Mchambuzi, kiini cha tatizo ni historia ya ukoloni kuanzia kwa mwarabu hadi mwingereza.
Kila ukoloni ulikuja na mizigo yake na kutuacha na faida au matatizo.
Athari za ukoloni zimekuwa katika nyakati tofauti zikiathiri jamii fulani kwa nyakati fulani.
Elimu inatumika kama kisingizio kwasababu tunajua kuwa kuna jamii zilifanikiwa sana siku za nyuma kwa mambo mengine hata kama si elimu.
Kwahiyo naweza kusema kiini cha mzozo siyo elimu, NECTA n.k. pengine tatizo ni matumizi ya elimu. Niachie hapa kwanza!