Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kitu kinachoendelea sasa ni jitihada ya Polisi na serikali kujaribu kutoa picha kwa Watanzania kwamba Hamza hakuwa mtu mzuri na Polisi ni watu wanaofanya kazi yao vizuri. Polisi na serikali hata wamekuwa wakijitahidi kuonyesha Hamza alikuwa mtu hatari angeweza kuua raia wengi kama Polisi wasingemuua, jambo ambalo watu wanajua ni uongo.
Tumesikia kauli ya Polisi kwamba Hamza alikuwa mtu wa hovyo hovyo, na kauli toka uongozi wa serikali ukisema kwamba ilikuwa lazima Hamza auwawe siku ya hilo tukio. Polisi pia wanajikita kwenye kufanya watu waone familia ya Hamza pia ni watu wabaya. Kuna kiongozi mmoja wa mtaa alipoishi Hamza alitoa kauli ya kipumbavu sana, labda aliambiwa aseme hivyo, eti inaonekana Hamza hakuwa na tabia nzuri kwa kuwa hakuna mtu aliyekuja kumripoti kwamba ana tabia nzuri!
Na sasa hata kuna propaganda kwamba Hamza alifanya alichofanya kwa msongo wa mawazo baada ya kupata hasara ya Tshs 400m, japo sijajua kwa nini kupata hasara kama hiyo kutasababisha chuki dhidi ya Polisi kama Polisi hawakuwa chanzo cha hasara yenyewe.
La kutisha ni kimya cha CCM juu ya Hamza, kada wao.
Kwa ujumla hakuna kauli toka Polisi, CCM na serikali inayogusia juu ya kwa nini Hamza aliamua alichoamua - kitu katika masuala ya kijamii tunaita cause and effect relationship; kisababishi na matokeo. Kwa nini hatusikii kauli yeyote juu ya nini kilifanya Hamza afanye alichofanya, au aamue lazima awaue Polisi wengi kadiri atakavyoweza?
Lakini huyu mtu ambae Polisi na CCM/viongozi wanataka tumone alikuwa mbaya, alikuwa na kichaa, alikuwa gaidi, alistahili kuuwawa, ndio huyo huyo ambae hapa chini anaongea akiwasifia Raisi Magufuli na Samia.