CCM na Serikali wasijidanganye kuwa wameshinda hii vita, uwanja wa mapambano tu ndio umebadilika

CCM na Serikali wasijidanganye kuwa wameshinda hii vita, uwanja wa mapambano tu ndio umebadilika

Kalamu ya Mwananchi

Senior Member
Joined
Oct 27, 2020
Posts
100
Reaction score
552
Wenye kuridhishwa, kufurahia na kushangilia huu 'ushindi' wafanye hivyo. Ingawa sielewe kuna faida gani ya kushangilia huu 'ushindi' katikati ya uwanja uliojaa damu.

Ila kitu pekee ambacho kinatakiwa kibaki kwenye fikra, mioyo na nafsi zao ni kuwa hii vita haijaisha bado. Kamwe wasijidanganye kuwa sasa upinzani umekufa. Hilo ni kosa.

Uwanja wa mapambano tu ndo umebadilika, tumezoea upinzani kuwa ndani ya bunge sana sana, sasa upinzani unaenda kuhamia sehemu nyingine.

Upinzani ni kama maji, it takes form, shape and structure kulingana na hali iliyopo wakati huo.

Unaweza kukanyaga, siginya na kuuponda ponda upinzani, ila daima huna uwezo wa kuuua.

Kama tu katika ngazi ya familia, watu wanaweza kuishi, kukua na kulelewa pamoja lakini kila mtu akaishia kuwa na mawazo na tabia zake tofauti, sembuse ngazi ya taifa...

Hata Nyerere tu katika kipindi cha chama kimoja bado alikumbana na upinzani ndani ya chama, kina Kambona, Aboud Jumbe n.k

China pamoja nakuwa ni nchi ya chama kimoja lakini bado kuna mass incidents zaidi ya 500 kila siku.

Nchi ni watu, na wote hatuwezi kuwa na mawazo yanayofanana hata siku moja.

Kwahiyo Serikali na CCM isi-relax na kubweteka kuwa sasa upinzani nchini umeisha. As long as watu nchini wanakuwa na mtazamo na mawazo tofauti, upinzani daima utadumu.

Kilichobadilika sasa ni uwanja wa mapambano tu, vita haijaisha.

Kwasasa 'wamefanikiwa' kuuondoa upinzani bungeni, ila utahamia sehemu nyingine. Unaweza kuhamia ndani ya chama chao wenyewe, na kuibukia pia kutoka sehemu nyingine ambayo hawajaitegemea bado.

Kuna msemo unasema, you have won the battle but not the war.

Kama ni kipenga ndo kwanza kimepulizwa, they should prepare for round two!
 
Ndiyo maana kilasiku tunawaambia baadhi ya WAJINGA-WAJINGA wa CCM kuwa huu ushindi wa kiini-macho utakuja kuleta shida Kwa wananchi wote na sio upinzani pekeyao...
huko mbele ya Safar hakutakuwa na maisha ya kujipendekeza Kwa Raisi Kwa style ya kuponda upinzani ili wapate vyeo kama akina(silinde,patrobas,kafulila na wengine).

Maisha ya Tanzania yatakuwa magumu kuanzia uwekezaji,na mahusiano ya kimataifa
 
Duh.. Kuna watu wana moyo jamani,

Kwahiyo hata baada ya hapa bado mnajifariji?

Sio kujifariji, bali ndo ukweli wenyewe huo.

Hakuna sehemu yoyote duniani ambapo upinzani ulishawahi malizwa kabisa. Bali hubadilika aina na muundo tu, kulingana na mazingira yaliyopo.
 
Kesho Siro ataamua mwenyewe. Ama kutuacha tuandamane au kuitafuta ICC. Lkn kesho, haki ya mama naapa patachimbika.
Wanafiki nyie..mitandaoni mnapiga kelele weee kumbe UPOPOMA tu
 
Kilaza wewe unajua ICC ni kama polis post
Kesho Siro ataamua mwenyewe. Ama kutuacha tuandamane au kuitafuta ICC. Lkn kesho, haki ya mama naapa patachimbika.
 
Mimi Kuna wakati roho ya kishetani inaniingia nataman ugaidi uje tuwe Kama Somalia au kongo au zaidi yao
Ukosefu wa ajira,mambo Kama haya ya uchaguzi yanaweza create vijana wengi kujiunga magenge ya kihalifu
 
Wajinga kulishana Ujinga Mlisha zoeleka Kazi kwenu
 
Back
Top Bottom