Uchaguzi 2020 CCM na Serikali yake tulikosea. Kwa hili lazima Lissu atupige bao

Uchaguzi 2020 CCM na Serikali yake tulikosea. Kwa hili lazima Lissu atupige bao

Hata Ulaya na USA ajira ni tatizo ndugu
Vijana wanaojielewa wamaejiajiri!
Na siyo wote kwenye mikusanyiko ya Lisu hawana ajira!
Na siyo wote waliokusanyika watampigia kura Lisu!
Subiri Oct ndiyo utaijua siasa
Huna details kaa kimya kuficha upumbavu wako; ulaya kijana ambaye hajaajiriwa analipwa nusu mshahara ya professional yake; je na hapa kwetu wanalipwa?
 
Huna details kaa kimya kuficha upumbavu wako; ulaya kijana ambaye hajaajiriwa analipwa nusu mshahara ya professional yake; je na hapa kwetu wanalipwa?
Kulipwa nusu mshahara ndiyo ajira?
Au hujui tafsiri ya ajira!
Elewa mada ndugu
 
Ukirudi kwa vijana wengiwetu hatujajiandikisha kwenye daftari la wapiga kula,na wzee wengi j wapenzi wa magufuli
Ko msoto hado tutaendeleanao
 
Hapo uliposema tutawaambia nini vijana hawa na wazazi waliowasomesha,ni tafakari kubwa,nadhani vijana hawa wakiamua kueneza elimu hii ya uraia kwa ndugu zao wote hapata tosha na ikumbukwe wametapakaa nchi nzima, mwaka huu tutasikia mengi,kwakweli hatukutegemea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana walidekezwa sana..eti kila akimaliza chuo anasubiri post, ulikuwa upotevu mkubwa wa hela vijana wakawa wanaishia maofisini tu, nani akalime sasa?
Hebu fikilia baba angu amekataa mkaa sana kanisisomesha hata ualimu akijua mwanangu atanipa nafuu hata kwa kakazi hako Leo hii tangu 2015 hakuna kitu has a walimu wa Sana'a huyu mzazi hawezi kukuelewa kabisa
Hapa tuseme tulikosea tu hatuna wa kimulaumu
Moyo wa upendo
Moyo usio na hila
 
Kati ya makosa yaliyofanywa na Serikali yangu ya CCM ni kushindwa kutoa ajira kwa vijana na kuacha wazagae mitaani bila kazi.

Ni kosa kubwa sana kwa sababu vijana hawa ni bomu tulojitegea wenyewe kutumaliza.

Maelfu ya vijana wanaojitokeza kwa wingi kwenye hadhara za bw. Tundu Antipas Lissu ni sababu yetu sisi.

Kwa miaka minne tumewatelekeza mitaani kama kuku wa videri; tumeua future zao; tumewaua kisaikolojia; tumewatoa kwenye reli hadi baadhi wamekata tamaa wameamua kuwa walevi wa gongo na wavuta bangi.

Uchaguzi umefika tutawaeleza nini hawa vijana watuelewe na watuchague?

Tutawashawishi vipi wazazi wao waliowasomesha kwa shida ili watuamini na watuchague?

Tutawambia tumenunua ndege?

Tutawambia tunajenga SGR?

Tutawambia tunajenga daraja la Busisi?

Tutawambia tumejenga flyover?

Wana CCM wenzangu; 'maendeleo ya vitu bila kuboresha maendeleo ya watu ni sawa na kazi bure'

Kwakuwa tumelikoroga kwa miaka minne sasa muda wa kulinywa umewadia.
Ngumu kumesa
 
Yaani Nina hasira na Fisiyenu nawasubiri kwenye box LA kura nawachinjia shingoni kama mbuzi wa kafara ,mmesababisha wahitimu wengi tumekosa muelekeo wa maisha sasa tunaenda kuwavueni nguo nanyie msubuke kama mbavyo wahitimu tumeteseka miaka 5 mpaka taaluna zetu zinapotea vichwani
 
Back
Top Bottom