Sophist
Platinum Member
- Mar 26, 2009
- 4,486
- 3,408
Huu ni uchambuzi mdogo. Msingi wa uchambuzi huu ni matukio yenye shaka katika utawala na siasa za Tanzania kuanzia 2016.
Kuna muda, ndani ya kipindi hicho, wakongwe ndani ya CCM, wakiwemo Pius Msekwa na Benjamin William Mkapa, wamewahi kuonya. Kwamba haifai kwa mtu mmoja ndani ya CCM kujitangazia kuwa ni maarufu zaidi kuliko chama chake kilichompatia fursa ya uongozi.
Wakongwe hao waliona hatari kwa Chama chao siku za usoni. Waliogopa madhara ya kisiasa, kama ilivyowahi kutokea nchini Malawi na kwingineko. Mwaka 2006 aliyekuwa rais wa Malawi, marehemu Bingu wa Mutharika alihama chama chake cha UDF, kisha kuanzisha chama chake cha DPP na kuendelea na cheo chake cha urais. UDF kilirejea kuwa chama cha upinzani.
Maandalizi yanayofanyika kwa sasa hapa nchini yanafikirisha. Ni bahati mbaya kuwa wanachama wengi wa CCM wanalishwa kasumba kuwa umaarufu wa chama chao unatokana na kutegemea umaarufu wa mtu mmoja. Ni bahati mbaya hasa kwa kuwa wengi wa wanachama wa CCM wameendelea kuamini kuwa hivyo ndivyo ilivyo badala ya kinyume chake.
Maandalizi yaliyosukwa kuteua wagombea wa urais, lakini zaidi utaratibu wa kupata ubunge kupitia CCM, ni dhairi kuwa, kwa macho ya uchambuzi kisayansi, wabunge watakaoingia kwenye Bunge la 12, watakuwa wamenyanyuliwa moja kwa moja (handpicked) kwa mkono wa mtu Bwana yule (mmoja siyo mfumo). Hakutarajiwi kuwepo kwa diversity ya wabunge kwa kuzingatia ukongwe na asili ya CCM.
Aidha, jitihada za kunyamazisha vyombo vya habari vyenye sauti mbadala; jitihada za kutengeneza upinzani bandia bungeni uliopewa hadhi mpya ya 'kambi rasmi ya wachache' Bungeni (official minority), [kanuni za Bunge zilirekebishwa siku moja kabla ya Bunge kuvunjwa rasmi] badala ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB); jitihada za kusambaratisha asasi za kiraia zenye msimamo wa kujisimamia badala ya kupokea maelekezo kutoka serikalini; jitihada za kusogeza muda wa kustaafu (extend) wa Msajili wa Vyama Vya Siasa (Jaji Francis Mutungi) kwa miaka miwili zaidi; na jitihada zinazofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhakikisha watuele wa Bwana yule ndio pekee wanapitishwa (siyo kuchaguliwa - nitawawekea uchambuzi wa kanuni mpya za uchaguzi mkuu, 2020 zilizoandaliwa na NEC na kwa sasa ziko mbioni kuwa gazetted) ni ishara au viashiria vya kutosha kwa wataalam na wachambuzi wa masuala ya siasa na utawala kubaini mwelekeo wa Tanzania baada ya uchaguzi Mkuu 2020.
Hii si ramuli ni uchambuzi mdogo wa kisayansi. Tusishangae baada ya uchaguzi mkuu 2020 kuona kinachoitwa CCM mpya kuwa chama tawala kipya hapa nchini na kisha CCM inakuwa chama cha upinzani. Tusubiri yajayo kuhusu utabiri huu.
Ni hayo tu kwa leo