CCM na Watanzania Kuweni Macho; Jamaa Anajiandaa Kuwatoka

Wimbo wa CCM Mpya
2025 tusonge mbele CCM Mpya inapiga hodi Mtaa wa Lumumba ,

CCM asilia/ Masalia tunakwambia angali maisha yako ya baadaye kama chama cha upinzani,

Tukumbuke wa mbele kwenda nyuma ndiyo 2025

Hodi Hodi wana CCM Mpya twaingia 2025

CCM asilia asiyekubali kushindwa siyo mshindani

Hodi Hodi wana CCM Mpya tunaingia 2025

CCM Asilia leo 2020 kwako yamekukuta
 
Duh...!.
P
 
Mtandao ndio ulikuwa tatizo kubwa kwa nchi hii.

Tunashukuru JPM kwa kuusambaratisha na kukirudisha chama kwa Raia na wanachama wa nchi hii.

Nyinyi mtandao membe endeleeni kulialia, CCM inapiga kazi na nchi inasonga mbele 100KMPH...
Mnajidanganya kiboya kweli....Amerudisha chama kwa wanachama? Sasa hivi jiwe lenu ndo ccm na ccm ndo jiwe. Hakuna mwanachama wa kuleta fyoko fyoko huko na wewe unalijua Ila unakuja kujidanganya hapa. Acheni uoga, acheni kujipendekeza mwambieni ukweli ili mkijitapa hapa tuwaelewe.
 
Kwenye uchambuzi (mdogo) nimeshauri tusubiri. Tafadhali tufanye hivyo. Tuendelee na trend readings.
Kama ni swala la "trend reading", mbona tayari ipo wazi?

Huyu hata angebaki na watu wanne ndani ya chama CCM, hata hiyo 'mpya' akiianzisha, 'trend' ni ile ile haibadiliki. Kati ya hao wanne atakaokuwa nao, bado atakuwa na wasiwasi juu yao na kuendelea kuwavuruga. Huo ndio mtindo wake, hawezi kuubadili.

Bunge lililopita hakuwa na upinzani wowote, ndani ya chama chake au toka kwa wapinzani, kwa sababu alishaliteka bunge zima, bado unasema hakuridhika na kwamba anataka bunge lifuatalo aweke watu anaowapenda yeye? Watu hao watakuwa na tofauti gani na hawa aliokwishawaweka chini yake katika bunge lililopita?

Sawa, tuendelee kutoa uchambuzi, hata katika maswala ambayo tayari tunajua mwekeo wake ulivyo!

If this is not an exercise in futility, I wonder what else it could be!
 
Jiweeeeeee anahaha kweli wenzie wanaplan a na b ,yeye ana plan a to z.
 
Mtandao ndio ulikuwa tatizo kubwa kwa nchi hii.

Tunashukuru JPM kwa kuusambaratisha na kukirudisha chama kwa Raia na wanachama wa nchi hii.

Nyinyi mtandao membe endeleeni kulialia, CCM inapiga kazi na nchi inasonga mbele 100KMPH...
Point of reference: " inategemea nimeamkaje"!!!!! Sijui kama akili yako imejipa nafasi ya kulitafakari Hilo neno!
Isome Tena hoja ya mleta hoja Kisha jumlilisha na Hilo neno la kuamka huenda ukawaza tofauti!
 
Tuache woga ili iweje. Wewe unaomba maafa yatokee, kwa hiyo unatushawishi tukuunge mkono.Jinga kabisa, kwanza hamna ulichochambua zaidi ya kuomba dua la mwewe. Leo kutwa nzima Rais anazindua miradi ya mabillion na ni mkoa mmoja tu wa Pwani.Piga simu bukoba New MV Victoria imetumia saa 6 kutoka Mwanza kwenda Bukoba mradi umeghalimu bil 20+ kesho meli inageuza kurudi lock city na tani 200 bure za walipa kodi.
 
Hakuna CCM mpya,CCM ni ile ile ambayo siku zote na mara zote haitabiriki.
Sema Magu kajiongeza cheo kimmoja zaidi ya kuwa Supreme Leader wa nchi ya Tanzania Bara.
Kwa muonekano huo,hakuna wa kumzuia au wa kumsumbua labda spymaster Membe ana uwezo wa kuthubutu.Lakini makada waandamizi wa Membe walipotishwa kwa kudukuliwa wakanyea debe ni waoga hawana msaada.
 
Ni kazi yake kuzindua alishajipa, ulitaka nimsifie wajibu wake?...Yani wewe ukipeleka chakula nyumbani Unataka mkeo na watoto wakusifie? Nyie endeleeni tu kumtukuza yesu wenu mi nawaona maboya tu
 
Kuna hoja hapa, bahati mbaya wengi ni wapofu
 

Wakati wenu ulipita ooops sio wewe lakini mliwezeshwa, kutesa ni kwa zamu. Hakuna lisilo na mwisho hapa duniani kila aliyezaliwa na mwanadamu ni lazima ana siku yake ya kuondoka. Mola ndiye aliyepanga haya yanayotokea hata mpige ramli namna gani hamuwezi tena kurudia dhulma mliyokuwa mnawafanyia Watanzania. JMK na BWM ni mashahidi, hivi sasa wanalea Tausi ambao walishindwa kuwaendeleza wakati wa uongozi wao.

JPM wakati wake tausi wamezaliwa hadi kwa kuwaweka ni shida, hivyo aliamua kuwazawadia ili wafahamu yale waliyokuwa wanawatendea Watanzania hayakuwa ya haki. ''Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.'' Kumbukeni mlisema kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala, sasa mbona nyie mnapiga kelele, mnafikiri mwenye nyumba atashindwa kulala? Kumbukeni wahenga walisema ''Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu uchungu.'' Hatma ya Uongozi wa Tanzania katika mwaka wowote ipo mikononi mwa Watanzania na sio mtu mwingine yeyote ambaye ametawaliwa na chuki au tamma ya madaraka. Mola ndie mpaji na lile ambalo mola amepanga hakuna kiumbe yoyote ambaye anaweza kubadilisha.
 
Ndio maana tunamuunga mkono Mkuu.
M4C iko ndani ya CCM.

Wapinzani wamepoteza muelekeo kidogo wamshukuru Zito kuanzisha Chama cha ACT .
Zito angekimbilia CCM leo hii upinzani Tanzania ungekua umeshakufa kifo cha asili.

Hata hivyo kumwambia mtu usigombee Ubunge nitakupa Cheo ni Rushwa ya madaraka.

Linatakiwa kupingwa kwa vikali ili waachwe wapambane kuomba ridhaa kwa wananchi.
Mbunge amekaa miaka 20 kwa nini asipingwe.
Mfano Job Ndugai kwa nini asipingwe na akashinda kwa hoja badala ya mizengwe.
Waliokaa miaka mingi kama Mbowe wapingwe pia ndani ya Chadema.
Akishinda ashinde kwa kushindana sio kutishana na kupitishana kwa Rushwa ya vyeo vya uteuzi.
 
Kwani wanachama wa Ccm wakongwe ikiwemo viongozi wastaafu hawaoni haya? Mbona wako kimya?
 
Mkuu hii ni hatari.
Hii si ramuli ni uchambuzi mdogo wa kisayansi. Tusishangae baada ya uchaguzi mkuu 2020 kuona kinachoitwa CCM mpya kuwa chama tawala kipya hapa nchini na kisha CCM inakuwa chama cha upinzani. Tusubiri yajayo kuhusu utabiri huu.
 
Mkuu hii ni hatari.
Hii si ramuli ni uchambuzi mdogo wa kisayansi. Tusishangae baada ya uchaguzi mkuu 2020 kuona kinachoitwa CCM mpya kuwa chama tawala kipya hapa nchini na kisha CCM inakuwa chama cha upinzani. Tusubiri yajayo kuhusu utabiri huu.
 
Ujinga ni kuingiza mada nyingine wakati inajadiliwa nyingine, huo ni ubakaji
Ulishawahi kuwa hata M/kiti wa kikao Fulani wewe? Mbona unashindwa hata kuelewa mada huwa inachakatwaje mkuu, halafu unakuwa mkali utazani Mimi nimekukatalia kutoa maoni yako bhana!!
 
Mtu akiwa mbaya kutokana na tabia na mienendo yake watu HAWAMPENDI, ni kweli na haiwezekani wakawepo watu WANAOMPENDA mtu huyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…