Inakuwa umefanikiwa kuingia rasmi kwenye mfumo wa Oligarchy
Mfumo ambapo nguvu na utawala zinalimbikizwa kwa kikundi kidogo cha watu wachache hasa familia zenye mali na mamlaka katika na kulindwa na utawala wa kijeshi
Wabunge na mawaziri huwa ni sehemu tu ya vijakazi wao na huwekwa kwa lengo la kulinda maslahi maalumu ya waliyopo kwenye mamlaka kwa lengo la kuwasaidia waonekane wanafanya mambo kwa kufuata protocol na sheria yakimataifa na siyo kwa lengo la kuisimamia serikali kwa niaba ya wanainji.
Upatikanaji wa watumishi wengine nilazima uwe ni ule uliyotayari kulinda mfumo na siyo kwa maslahi mapana ya Taifa .
Ninawahurumia sana watanzania masikini wanaoiunga mkono hii CCM ya sasa .
Huko mbeleni tujiandae kuwa na mpasuko mkubwa sana kati ya kundi la watawala na watawaliwa .
Ndiyo za mtoto wa mkulima kapuku kuja kuwa kiongozi ni ndoto isiyofaa kuotwa,
Mfumo uliyopo sasa ni ule ukishika wakusanye .
Nadhani tumeona namna family za waliyobahatika kuingia kwenye system na namna wanavyokusanyana .
Huo ndiyo uelekeo rasmi .
Hujachelewa ,ukitaka uwe miongoni mwao amua kuwa chawa leo ,Wenda mbeleni utajakuja kuokota dodo japo siyo kirahisi kihivyo ,inaweza kukuchukua hata kizazi chako cha 200 mbele.