tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
- Thread starter
- #401
![]()
![]()
TAKRIBANI wanafunzi 700 katika Shule za Msingi Machimweru na Kinyambwiga A na B, zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, wanasomea chini ya mti wakiwa wamekalia mawe na magogo, huku mbao za kufundishia zikiwa zimepigiliwa misumari kwenye miti, FikraPevu imebaini. Hali hiyo imeelezwa kuwa chanzo kikuu cha kudhoofisha hali ya taaluma katika wilaya hiyo kwa kiwango kikubwa. Taarifa zilizoifikia FikraPevu Agosti 31, 2014 zinaeleza kuwa licha ya wanafunzi hao kukaa chini wakati wa masomo pia shule hizo zina matundu machache ya choo, ikiwemo matundu manne ya shule ya msingi Machimweru yanayotumiwa na wanafunzi pamoja na Walimu 18 wa shule hiyo.
Na wakati wanafunzi wakisomea chini ya miti, kuna MATUTUSA kule Dodoma wanatafuna 300,000 kwa siku bila sababu zozote za msingi....inauma sana! Ee Mungu tunasue kutoka ukoo huu wa panya mwaka 2015. Amina.



