CCM nambari wani

tpaul nanyi mnakuja na ngonjera kuwa mtawapatia wananchi maisha bora kumbe ni tamaa ya kushika dola tu. hakuna namna mtaongeza vyanzo vya mapato kuweza kuwapatia watanzania wote maisha bora. picha hizi kama ungezichukua kwa mlinganisho.mfano nyumba mbovu na nyumba bora za kisasa zinazojengwa nchini kote na nssf, na nhc, shida ya maji na juhudi za kutandaza mabomba na miundombinu mingine ya maji, zahanati ya makuti na zahanati bora na zenye vifaa zilizojengwa kwa kipindi chetu hapo ungeeleweka. lakini umefanya makusudi na kujikampenia kwa kuwadanganya watanzania kuwa hali hiyo ndio uhalisia wao kumbe wao wanaona tofauti. wanasafiri kwa barabara za lami, wanalima na wanapata pembejeo kwa wakati, wanauza mazao yao kwenye vyama vyao vya ushirika wanapata umeme wa rea na tanesco, wanapata maji kupitia mamlaka zao za maji wanawapeleka watoto wao wote shule tena sasa hivi zenye maabara na mengineyo mengi tu. wanatumia vipato vyao kujijengea nyumba bora na kujiwekea umeme.hayo uliyotupia ni kaupande kamoja tu ka shilingi tupia upande mmoja wa shilingi na ulinganishe na upande wa pili wa shilingi..usiwahadae watanzania
 
Kwa hizi picha natamani kulia japo nipoze machungu
 
Kwa upande wangu huu ndio uzi bora kwa 2014 , Mungu akulinde sana mkuu tpaul .
 
[TABLE="class: cms_table_tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: cms_table_tr-caption"]Ridhiwani Kikwete mbunge wa Chalinze akigawa ndizi kijini Kwa Msanja
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana

 
ukisoma kwa umakini uzi huu na posti zake ndio utajua kwanini wanasema watanzania wana IQ ndogo. Kuna watu wanapost bila kusoma uzi unahusu nini, akishaona rangi ya kijani ni kuitukana ccm tu hivi hakuna mazuri yaliyofanywa na ccm au ndio mnafikiri kwa akili za kuambiwa?. Uhalisia na maana ya picha hizi hauwakilishi hali ya watanzania sababu unaweza kutumia picha hizi hizi ukatoa ujumbe ulio positive kwa CCM.
tpaul kwanini usiweke uzi wenye mambo mazuri yaliyofanya na wabunge wa chama chako? au hawajafanya lolote?
Mzee Ndesa yeye alitoa hii ameweka na ushahidi kabisa hebu tupe za hao wengine
 
Last edited by a moderator:
We ultaka wakuletee hela CCM Kwenu?

No. Nilitaka mafisadi wa CCM wa ESCROW, Meremeta, Richmond, Tangold, Kagoda, etc wabebe pesa kwenye LUMBESA wampelekee JK kama walivyofanya mafisadi wa EPA. Na wakishamkabidhi fedha awaruhusu warudi mtaani (pasipo kuwachukulia hatua) ili waendelee kuiba tena wampelekee. Na asitokee hata mtu mmoja anayehoji wezi hao wanaorejesha fedha ni kina nani, wamerejesha pesa ngapi na zipo wapi! Haya ndiyo MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ambayo kila mwananchi anayataka. Umeona eeh? CCM oyeeeeeeeeeeeee!!!!
 
Hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha
 
Hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha HAHAHA😛eace:Hahaha hahaha
 
Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana


Like father...




...like son!



Asante sana mkuu BAK na Mag3 kwa picha za nyongeza. Hapa ndipo CCM na makuwadi wao wa ufisadi walipotufikisha. Ninachoshukuru ni kwamba sasa wananchi wote, mijini na vijijini, wameshaung'amua ulaghai wa CCM na hawako tayati tena kuendelea kuhadaiwa na hawa manyang'au....2015 lazimia kitaeleweka tu. Dawa ya magamba na mafisadi wanaowafuga iko jikoni inachemka.
 
Last edited by a moderator:

kwel uzalendo unashika kasi upo fresh big up
 


I dont think one could have a better answer than this! Ni jibu SAHIHI kabisa kwa muulizaji! - What a critical mind! Big up!
 

Mkuu laiza mbona unachangia kwa uoga sana, hujiamini? Tuliza akili zako upate kuelewa ujumbe ninaotaka kuufikisha kwa watanzania. Haya maswali yote uliyouliza naona umejikanaganya ama kwa makusudi au kwa kutokujua:

1. Vyanzo vya mapato vitaongezwa kwa kuzuia UFISADI wa fedha za umma tofauti na CCM wanaowatetea mafisadi kwa nguvu zao zote. Wewe hujui kwamba mabilioni ya fedha yanayopotea kila siku ni fedha za wananchi ambazo zingetumika kuwaletea maendeleo? Na je unadhani kwamba yale mabilioni ya EPA aliyoyachukua Kikwete kutoka kwa wezi wa EPA yangejenga barabara ngapi kama angeyarejesha kwa wananchi?

2. Pesa za NSSF sio za UMMA...hizi ni fedha za wanachama zinazotumiwa vibaya kujengea miundombinu ya serikali huku wenye fedha zao hawanufaiki na kitu chochote kutokana na vitega uchumi hivyo. Huoni kwamba ni UCHIZI serikali kutegemea fedha za wanachama huku ikiwaachia wezi wanajichotea fedha za umma? Aidha NHC ni shirika la umma linalojiendesha kibiashara na nyumba wanazojenga wanakaa mafisadi huku wananchi wa kawaida wakiwa hawana mahali pa kuishi. Pia, fahamu kwamba zaidi ya 50% ya nyumba zote zilizojengwa na NHC zimeishanyakuliwa na mafisadi...wamejiuzia kwa bei ya kutupa. Ina maana hata hili hilifahamu au umeamua tu kujitoa akili?

3. Shida ya maji nimeishaionglea kwenye uzi mama hapo juu...hebu tazama picha tu kama hujui kusoma. Unataka SHIDA hii ya maji niiongelee mara ngapi?

4. Ni kweli kabisa kwamba haya matatizo niliyotupia humu ni machache ukilinganisha na hali halisi ya maisha ya watanzania. Hali ya maisha ya wananchi ni mbaya kuliko hii inayoonekana kwenye picha hapo juu. Ni juzi tu mwananchi mmoja aliamua kunadi figo lake ili apate fedha za kujikimu....hali ya maisha ya wananchi ni mabaya kuliko kawaida. Nakupongeza kwa kuuona huo ukweli. Ungana na wazalendo tukaikomboe nchi kutoka mikononi mwa mwa wakoloni weusi (CCM) mwezi wa Oktoba mwaka huu wa 2015.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana Mkuu tpaul kusoma michango kama yako na wengine wengi hapa katika kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania na Tanzania kwangu mimi ni motivation kubwa sana ya kuja hapa kila siku na kusoma misimamo yenu kuhusu mustakabali wa nchi yetu, bila michango yenu mimi siku nyingi ningekuwa nimeshasepa hapa mahali. Mbarikiwe sana wote na msichoke kuleta michango yenu ya ina mbali mbali ikiwemo picha kama hizi zinazoonyesha hali ya kusikitisha sehemu nyingi nchini mwetu.

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…