Binafsi ninavyofahamu ni kuwa CCM si chama cha waislamu ila kuna viongozi wa juu wa sasa wa chama na serikali (ambao ni waislamu) wanaamini kuwa kuna watu fulani ndani ya uislamu walichangia sana wao kuwa madarakani na kutamani kutimiza yale yote wayatakayo kama njia ya kulipa fadhila. Hawa viongozi ndio wanafanya CCM kionekane kuwa chama cha waislamu.
Nyerere na serikali yake mtakumbuka walikuwa ni wapinzani wakubwa wa udini na ukabila. Mtaona namna ambavyo upinzani wao wa udini na ukabila ulivyokuwa chanzo kikuu cha amani nchini. Hivi vyumba viwili vikifunguliwa na kuachwa wazi bila usimamizi thabiti ndani ya chama na serikali, then tutegemee mipasuko ambayo madhara yake tunayajua sote.
Natumai ni sahihi, lakini naamini kuwa kuna waislamu wakorofi na watulivu; the same applies kwa dini zingine. Watu hawa huwa wanaisumbua sana nchi na kujifanya wao ndio wamewaweka viongozi wa juu madarakani, matokeo yake kuishia kuwaghasi na matakwa kibao kushinda hata wahisani na wafadhili.
JK amka na uwageuke wanaokudanganya na kujifanya kukuweka madarakani kisha usimamie katiba na misingi mikuu iliyotufanya tuwe nchi ya umoja na amani. Kuna wakristo, wapagani, waislamu watulivu na dini zingine kibao ambao walipambana kukuweka madarakani, usikubali kudanganywa na kuwasaliti watu hawa na kuwaona si lolote katika juhudi za kukurudisha state house. Usikubali kufavor dini fulani na kuigeuza serikali kuwa ya kidini (sina maoni zaidi juu ya chama chenu, mkichakachue muwezavyo but tuachieni nchi yenye amani, umoja na utulivu).