Usitetee uzembe wa serikali. Uhusiano wa serikali na raia ni kama uhusiano wa baba na mwana, na kwa muktadha wa hoja inayojadiliwa, uhusiano huu ni kama wa mzazi na mtoto mdogo ambaye akili haijakomaa. Unamkataza mtoto asitende jambo fulani ni hatari, lakini bado anarudia. Hapo lazima utumie nguvu kwa manufaa ya mtoto. Utetezi kwamba waliambiwa waondoke au waliondoshwa na kulipwa fidia kisha wakarudi ni wa ovyo kabisa. Serikali Ina kila kitu- mamlaka, utaalamu, uwezo wa fedha kutekeleza jambo, rasilimali watu nk.
Ni kama vile unakuta mji unaanza mahali, mji unakuta kido kidogo maka unakuwa mji mkubwa. Pale serikali Ina kusanya kodi kwa wakazi wa eneo lile, watu wakiomba wanaunganishiwa umeme maji etc. Lakini utakutamji huo hauna huduma kama shule ya msingi/sekondari, hakuna Eno la soko, hakuna zahanati/kituo cha afya, Eneo la kuzikia nk. Ni wajibu wa serikali kwanza kutoa idhini kwamba eneo husika linafaa kwa makazi, na iweze kupangilia mji kwa kutenga maeneo kwaajili ya huduma mbalimbali.