CCM ni Lazima Tuwe Accomodative Kwenye Katiba Mpya

Heshima kwako, W. Macela,
Ni mawazo mazuri na kweli kama ulivyosema CCM inaweza kutawala miaka mingi na si milele kama ambavyo baadhi ya wana wa CCM wanavyojidanganya. Ningekuwa na uwezo ningewashauri CCM hivi, simamieni mchakato wa kuandika katiba mpya kwa kujiandaa kuwa wapinzani ili katiba ijayo iwe huru na ya haki kwa kila Mtanzania bila kujali itikadi yake, iwe kweli katiba ya wa Tanzania na si ya kusaidia CCM kuendelea kutawala. Mwl. Nyerere 1995 kwenye mkutano mkuu wa CCM alisema, Watanzania wanahitaji mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.
 
Utumbo!!!!!! By the way suala la katiba mpya lilikuwa katika ilani ya uchaguzi ya CHADEMA!!! Ninyi magamba mmeparamia tu ilani ya chadema!!

CDM wangefanyaje hili bila ya wenye mamlaka na dola kukubaliana ? bila JK kwa huruma yake hili lisinge kuwepo.

 
Le Mutuz leo limeshuka nondo ila hiyo mistari miwili ya mwanzo kama CCM watatumia misimamo ya chama katika mabaraza ya katiba kuna hatari ya katiba mpya kuwa imetengezwa based on maoni ya CCM maana kwenye mabaraza ya katiba wao ndio wengi unless kama tume ya katiba itakuwa na uwezo wa kufanya uamuzi wa kuangalia maoni ya wachache pia kama vile ilivyotokea wakati wa kuanzishwa vyama vingi
 
Malecela, NO, and BIG NO for that matter. Yaani mnataka kutunga katiba itakayopipendelea CCM kushinda? NO. Watanzania tunataka katiba itakayoleta ustawi wa maisha ya watu wote. Kwenye hili ningeshauri hizo ziasa ziachwe kwanza, tutafute katika ya nchi kwa ajili ya wananchi, si kwa ajili ya vyama vya siasa
 
Utumbo!!!!!! By the way suala la katiba mpya lilikuwa katika ilani ya uchaguzi ya CHADEMA!!! Ninyi magamba mmeparamia tu ilani ya chadema!!

Hapa umenena mkuu.HAta Chikawe na yule mama mwingine waziri aliyekuwa ktk wizara ya sheria na katiba alisema iliyopo inakidhi ,lile pungu..ani lingine mnaoliita mwanasheria (Weee ree maa) wa serikali lilipinga vikali mabadiliko ya katiba sasa hapo iweje wajichukulie misifa?

 
Huwa sikubaliani na maandiko yako mengi lakini kwenye andiko hili ninakuunga mkono. Hivi ni kwa nini wakati mwingine huwa unajichizisha mpaka unaonekana kuwa useless kama t/paper?
 
Willy kakubali kuwa sio kila kitu wanachosema wapinzani ni kibaya. Kawataka magamba wenzie kukubali kukopa baadhi ya mazuri toka opposition. Actually kawapinga akina Werema, Chikawe na mama wa wizara ya sheria ya katiba
 
Pasco,

..lakini tunapoandika katiba tunatakiwa tutangulize maslahi ya nchi na wananchi.

..hatutakiwa kuendekeza masuala ya chama, na kuyatumbukiza ktk katiba.

..dhana ya kuendekeza maslahi ya chama, ndiyo imepelekea CCM kuvamia kwenye mabaraza ya katiba.

cc: EMT, Kiranga, Mag3
 
Last edited by a moderator:
kumbe unaujua ukweli
 

- Bahati mbaya sana kwamba CCM lazima ishiriki kama Chama cha Siasa na the worst ni chama kinachotawala sasa hivi so pole sana bro!!

Le Mutuz
 
- Bahati mbaya sana kwamba CCM lazima ishiriki kama Chama cha Siasa na the worst ni chama kinachotawala sasa hivi so pole sana bro!!

Le Mutuz
Nadhani CCM ndio wanapaswa kupewa pole kwa maana kuwa kama chama 'kinachotawala' katika hili hakiikupaswa kufikiria kwanza utawala bna badala yake kifikirie zaidi maslahi mapana ya watanzania.
Huu upofu wa kufikiria utawala zaidi ndio utakaotupayia katiba mbovu yenye maslahi mafupi ya wale waoafikiria kutawala zaidi badala ya ustawi wa watanzania na nchi kwa ujumla.
Sidhani kama katiba ya nchi ni jambo la 'mwamba ngoma'. Ninachokisema ni kuwa katika hili kila mmoja anatakiwa kufikiri juu ya maslahi yake, iwe ni chama cha siasa au kikundi cha ngoma. Katika hili sote tunapaswa kufikiri ustawi wa Tanzania na si vikundi vyetu
 
Pasco wa JF alishajitabilia nafasi ya Salva Pale ikulu iwapo kambi yake ambayo anaisemea itapita..EL group naona anakaribisha wenzake wajiunge
Mkuu Ben, kwanza sio kweli, mimi ndiye Salva wa ile kambi!, Salva wetu yupo, tena ni member humu!, wakati muafaka ukifika, mtamfahamu!.

Mimi ni "mpiga debe tuu!.
P.
 
Le MUTUZ baharia, kwa taarifa yako ni kwamba katiba inayoandikwa ni katiba ya nchi ya Tanzania na sio katiba ya kukilinda chama cha magamba!!!!
 
Kweli CCM hatuna washauri wa maana.
Wakati wenzetu CHADEMA wanafanya utafiti kujua nini watanzania wanakitaka na hapo ndio wanajenga hoja zao za msingi ili waje KUONGOZA vizuri nchi hii, sisi CCM kutwa tunakaa kupanga hila za kila namna ili tuendelee KUWATAWALA hao watanzania siku zote.
Haya ndio yananifanya nizidi kuwadharau sana wanaCCM wenzangu kila siku.

Poorer my CCM.
 

Mbona hoja zako zinaonekana zina mashiko, lakini unakosea unapozilenga moja kwa moja kwa ccm wakati mchakato wa katiba ni wa watanzania wote, ni vizuri vitu vizuri kwa taifa letu ukaviaddress kwa watanzania wote kwa manufaa ya taifa letu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…