Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Wilayani kwetu tangu nikiwa mdogo, kuna kiwanja kilichotengwa kwa ujenzi wa Ofis za Chama Wilaya, kiwanja hiki kilikuwa kwenye prime area kinatazama barabara kuu.
Wakubwa walifika bei na kumuuzia Mwarabu ambae amejenga Hotel. Mpaka sasa ofisi ya CCM ni ile ile iliyokuwa ya TANU. Kuna pesa za ujenzi ziliwafikia, makada walibadilisha madirisha na kupaka rangi, mengine usiulize ila Ofisi ya Chama wilaya Ina vyoo vya shimo tena viwili.
Nape alipigania maslahi ya vijana walio wengi dhidi ya makada wakubwa walionufaika na jengo la Umoja wa Vijana pale Dar. Naye alipopewa ukuu wa Wilaya alinyamaza kimya. Maisha yakaendelea.
Mwalimu Nyerere alipofariki kuna Mzungu mmoja Mark Hastings aliandika chapisho kuhusu maisha ya Nyerere alivyomfahamu tangu akiwa mwanafunzi wa elimu ya juu Edinburgh. Mzungu yule aliichambua sana siasa na sera za Ujamaa na kusema kuwa, miaka ya 80-90 Watanzania waliokuwa na vitambi wengi walikua viongozi wa Chama cha Mapinduzi ambao walikuwa na uhakika wa usafiri kwani walikuwa wanaendeshwa kwenye Landrover 109.
Rais Magufuli alipoingia madharajabu iliundwa kamatiya kuhakiki Mali za Chama. Ile ripoti mpaka kesho haijawekwa hadharani.