PreGE2025 CCM: No reform, No election, ni matokeo ya matendo yetu, Tujisahihishe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Mwaka 1962, Mwalimu Nyerere aliandika kitabu kidogo cha kurasa 20 kinaitwa TUJISAHIHISHE. Kwa maoni yangu wana CCM ni vema tukajikumbusha maudhui yake ili tulisaidie taifa.

Katika kitabu hiki Mwalimu Nyerere anasema "Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu ya mambo kama mafuriko, nzige, kiangazi, n.k., matatizo yao mengi hutokana na ubinafsi." Ni jambo lililo wazi kuwa ubinafsi wetu katika michakato ya uchaguzi ndio umetufikisha hapa. Picha tuliyoijenga ni kuwa nafasi zote tunataka ziwe zetu CCM, iwe tumechaguliwa au hatukuchaguliwa? Hata chache wanazopata wapinzani kwa haki, tunawapora.

Tutafakari ikiwa wagombea wa CCM wakikatwa nchi nzima, tukaambiwa hawajui kusoma na kuandika, sisi kama wana CCM tutajisikiaje? Au wagombea wetu wanapoenda kurudisha fomu wawe wanapigwa chenga na wakurugenzi mpaka muda wa kurudisha fomu unaisha halafu waambiwe wameshachelewa hivyo fomu zao hazitapokelewa? Au mawakala wa wagombea wetu wafanyiwe mizengwe kuingia kwenye vituo vya kupigia kura? Sisi wana CCM, tukitendewa mambo kama hayo tutakubaliana nayo?

Katika kitabu chake Mwalimu anasisitiza kuwa: “Makosa ni makosa bila kujali ni nani ameyafanya. Muhimu ni kuyajua makosa hayo na kujisahihisha.” Tujiulize, fomu za wagombea wa upinzani zingekuwa zinapokelewa bila mizengwe, wanateuliwa kugombea bila mizengwe, mawakala wao wanaruhusiwa kusimamia kura za wagombea wao bila mizengwe na pale wanaposhinda wanatangazwa bila mizengwe, Je, tungekuwa na No reform, No election?

Mwalimu alisema "hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujifanya hayapo" Yanayolalamikiwa na CHADEMA, yanaakisi kauli za Ndugu Nape za halali, nusu halali na halamu, pamoja na zile za DC Ng'umbi wa Longido kuhusu walichofanya 2020. Wenye wasiwasi na utendekaji wa haki kwenye chaguzi zetu sio CHADEMA tu, hata Prof. Assad CAG mstaafu naye anasema hata piga kura mpaka reform zifanyike. Madai ya reform sasa hivi yamekuwa ni ya watu wetu, na Mwalimu anatuasa "Chama cha siasa hakina budi kujishughulisha na shida za watu."

Mwalimu alitufundisha “Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwapuuzwa!”

Tumeaswa na baba wa Taifa kuwa "Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu." Hakutakuwa na ubawa kuyafanyia kazi maoni ya wazee wetu akina Butiku na Warioba. Haswa ukizingatia hata viongozi wa dini nao wameshauri mazungumzo yafanyike. Kasoro zinazowezekana kurekebishika zirekebishwe, twende kwenye uchaguzi October tukiwa wamoja kama Taifa.

“Tujisahihishe. Tujitazame. Tujikague. Tujione. Tujirekebishe.” Mwl Nyerere 1966.


View: https://vm.tiktok.com/ZMA27FELK/

 
Watakuua.Jinyamazie na ufuate kilicho chema.
 
CC: Lucas Mwashambwa Tlaatlaah chiembe Lucha Pascal Mayalla Shotocan Dr wa Manesi ChawaWaMama MamaSamia2025 na mices, vyura na wadudu wengine wa CCM waisome na kuielewa hii
 
Kama bado upo CCM basi jua haupo sehemu sahihi. Mie nilishajiondokea baada ya kuona ukiwa na akili wewe ni adui.

Njoo Chadema.
 
Madaraka hulevya, hivi umuambie Mtu kama Mchengerwa kwamba kuna siku ccm itaanguka unadhani atakuelewa?
Mwalimu nyerere ni kiongozi aliyefeli pakubwa
 

Attachments

  • IMG_20250608_202508.jpg
    348.7 KB · Views: 32
PhD yako mkuu

Umeisotea haswaa na niyakweli kweli

Ubarikiwe kwa kuwaambia ukweli ccm

Ila swali moja tu, umejipangaje na wapotezaji?

Maana kitu wasichokipenda ccm ni kuambiwa ukweli

No reforms no election
 
UTAVUNA UNACHOKIPANDA NDYO NATURE ILIVYO.
Kwakujisahihisha tutarajie kuvuna nini? Wana CCM tuwasaidie viongozi wetu badala ya kuwasindikiza shimoni. Katika mwaka mmoja wa urais wa Dr. Samia tulikuwa tunaongelea mama kushinda tuzo ya Mo Ibrahim. Je, hali ipoje leo? Mafanikio makubwa tuliyoyapata kitaifa na kimataifa kupitia 4R tutayapoteza kwa kuhangaika na CHADEMA ambayo is not even a threat kwa ushindi wa mama. Kikwete alitufundisha kuishi na wapinzani inawezekana, tunaweza poteza majimbo mawili matatu, its okay, hiyo ndio gharama ya demokrasia.
 
Ni mtu mjinga pekee anayeweza kushabikia ccm. Ccm kimekuwa sio chama cha siasa tena. Limekuwa genge la kusaka na kung'ang'ania madaraka ili waendelee kuwanyonya watanzania ndio maana wako tayari kuua wananchi ili wabakie mdarakani.

Kwa kuwa wamekuwa wakifanya usanii kwenye sanduku la kura hakuna sababu ya kupanga foleni kupiga kura hadi watakapokubali uchaguzi huru na wa haki.
 
Hamuwezi kujisahisha nyie, badala yake mnnaua mnateka mnafira na kututisha
 
Hamuwezi kujisahisha nyie, badala yake mnnaua mnateka mnafira na kututisha
Watendao hayo ni wahalifu kama wahalifu wengine, bila kujali itikadi zao. Ahadi namba moja kati ya ahadi kumi za wana CCM ni: "Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja" Mwana CCM wakweli hawezi kutenda hayo.
 
Tunapozungumzia ukomavu wa kisiasa ni pamoja na kujiepusha na kutoa kauli zisizofaa. Sasa hii label ya "Ni mjinga tu" ilikuwa na sababu gani kuitumia hapa? Je, unataka tuamini akina Warioba na Butiku ni wajinga? Maana ni wana CCM hawa? Mm nadhani tuyakemee maovu bila kufanya stereotyping, kwa kufanya hivi tutajenga badala ya kubomoa.
 
Uchaguzi ukiwa haki, ccm haina uhakika wa kupata 2/3 ya kuwawezesha kuamua chochote watakacho bungeni. Hawakatai uchaguzi wa haki kwa bahati mbaya, ila zama zimewaacha kwa sasa.
 
Mimi sielewi Kabisa,, Hivi Kuna ubaya Gani kufanya reforms..Kwani Ni Dhambi Mbona Watu wanachukiana bila sababu!???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…