PreGE2025 CCM: No reform, No election, ni matokeo ya matendo yetu, Tujisahihishe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Warioba na Butiku wanashabikia ccm?
 
Watendao hayo ni wahalifu kama wahalifu wengine, bila kujali itikadi zao. Ahadi namba moja kati ya ahadi kumi za wana CCM ni: "Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja" Mwana CCM wakweli hawezi kutenda hayo.
Na ndio wanatenda, kwani wanaotenda hayo ni chadema? Na tena wanatetea mauaji na utekaji hadharani na bungeni

Ccm na shetani ni ndugu
 
Dr. Adam ahsante kwa andiko lako. Kila mwenye akili anafikiria hivyo kama wewe, na si kuhubiri amani, amani huku nyuma wameficha mapanga.

Hata wakizuia hii 2025, mabadiliko hayazuiliki, watake ama wasitake. Bora wangekuwa wana uma na kupuliza kama ulivyowashauri. Ila kwa kubinya haki miaka yote hii, mabadiliko ni lazima.
 
Mimi nafikiri ungesema kuna kakikundi kadodo ndani ya CCM kilichojimilikisha Chama. Kikundi hicho kidogo ndicho kinachoamua nn kitendeke ndani ya Chama/Serikali.

Sasa wapo wachache waliokataa kuingia mikononi mwa watekaji wale. Mf ni hao uliowataja.
 
#

#No reforms -No election
#freetundulissu#
 
Na ndio wanatenda, kwani wanaotenda hayo ni chadema? Na tena wanatetea mauaji na utekaji hadharani na bungeni

Ccm na shetani ni ndugu
Tangu lini uanachama wa chama cha siasa ukawa ni nasaba ya kuwatambulisha wahalifu? Hawana utaifa, kabila, dini au ukoo? Katika kurekodi jinai, tunaanza na jina, utaifa, dini, kabila na katika kuchunguza hata ukoo waweza fikiwa. Itapendeza tukisema X Y, Mtanzania, mkristo/muislam, wa kabila fulani anafanya moja mbili tatu badala ya hii stereotyping. Mm ni CCM kwahiyo na mm nateka na kuua?
 
Utashangaa ushauri mzuri kama hu unaonekana adui wa ccm. Hivi kuna tofauti yoyote ya shetani ja ccm kweli? I doubt
 
Nadhani leo nimeshuhudia andiko bora zaidi hapa JF kwa miaka ya hivi karibuni.

Nakumbuka pia, ni wiki siyo nyingi sana nilipishana na mwandishi wa mada hii humu humu JF; sikumbuki vizuri maudhui ya mada ile, lakini huenda ni juu ya suala hili hili la siasa za CCM miaka hii ya karibuni.

Ni uamini wangu mkubwa, kwamba ndani ya CCM yenyewe sasa hivi kuna wanachama wengi wanaojiuliza maswali juu ya mwelekeo wa chama chao; kama huyu mmoja alivyohoji na kupendekeza.
Naamini wanachama wa aina ya huyu ndani ya chama hicho hawawezi kupuuzwa.
Kuwapuuza hawa, maana yake kutakuwa na njia moja tu iliyobaki kwa nchi yetu.
Kukubali Rais Samia aendelee kukaa madarakani isivyo halali; kwa kutumia nguvu, na katika kufanya hivyo kumwaga damu ya waTanzania; wakiwemo wanachama wa CCM wenyewe.
Maana yake ni kwamba, Samia atakuwa tayari kutawala nchi kwa mabavu; na nafasi ya chama, CCM itakuwa haina maana tena katika utawala huo.
Sijui kama nchi itakuwa na utulivu baada ya hapo.
 
Hilo wanalijua wao. Chukulia kwamba ni wana ccm. Ni lini uliwahi kuwasikia wakishabikia ccm kama wafanyavyo akina Wassira na Samia?
Mkuu 'Open school', hata sijui unako elekea wewe na fikra zako hizi.
Mzee Warioba na Butiku ni wanachama watiifu wa chama chao cha CCM. Unachotaka kukumbushwa ni kuwa uanachama wao hauwapunguzii upendo wao kwa nchi yao Tanzania. Hao ni waTanzania kwanza, na uCCM unafuata, kama inavyotakiwa kwa mzalendo yeyote.
 
Shida ni kuwa viongozi wa sasa wa ccm wamekuwa wagumu na kushupaza shingo lait wangekubali kufuata misingi iliyowekwa na waasisi wa Taifa Hili Tz ingekuwa sehemu salama ya kuishi.But now it's vise versa
 
Mwenye akili hutazama usahihi wa njia zake na huona makosa na kufanya marekebesho,lakini mjinga hutembea kwenye fikra za usahihi hata pale kwenye makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…