CCM pawaka moto Dodoma

MkamaP,
Mkuu, Kiswahili lugha yangu, lakini hoja na mafumbo uliyotoa hapojuu naona yako nje ya mstari hayalingani kabisa na Hoja iliyopo mezani. Naomba ufafanuzi ili tuendeleze mjadala na kusaidiana.
 

Hiyo ya kutoka nje kwa hao unaowasema ili ripotiwa jana J3 na magazeti na walitoka nje siku ya Jumapili siku ya kwanza ya kikao cha NEC si jana J3 wakati hiyo thread ya kilewo ni ya jana J3 acheni fix zenu hata hivyo hatuhitaji tena audio yake tumeshapata ajenda zake
 
Angalia sana haya magazeti ya Bongo mengi siku hizi yanatumia JF kama chanzo cha habari

RayB,

Ninachofanya hapa ni kuunga mambo. Hawa jamaa wa 16/Kilewo walisema Sitta alikunywa maji glasi nzima na kutoka nje ambako alikaa muda mrefu bila kurudi. Gazeti la Mwananchi linaripoti Sitta alitoka ndani ya kikao na kuwa na kikao kingine cha faragha na Mwakyembe na Kilango. Kilewo nadhani anawish kuandika 'mamboz' ila huenda anaandika kwa wasiwasi au hata kutype kwenye kompyuta kwake ni tatizo... rejea maandishi yake.. typos nyingi laini zake hazizidi tano.
 

Luteni,

Hata kama hukubaliani na kinachosemwa lugha za kibabe hapa sio mahali pake! Ushafahamu! Hata sisi twazijua. Kwani Kilewo alitaja Sitta alitoka ndani lini? Au kwa sababu aliongea j3 na kwa hiyo lazima Sitta alitoka ndani j3 na si j2? Kama tunavyokusikiliza wewe ni haki yako na mtu mwengine yoyote ana haki ya kusikilizwa. Sasa kama wewe umeshapata hizo ajenda mbona hujatuletea hapa?? Nina imani Uluteni wako ni wa 'kiukweli' na si kama wa kina Makamba!!
 

Gottee
Fuatilia post zangu sina lugha za kibabe lakini huwa mdadisi sana
Hizi ndizo agenda za kilewo unazotaka tuziamini unauhakika RA aliongea jana?

Kilewo: agenda za kipuuzi walizo kuwa nazo jana ni 1. kuhakikisha upnzani haukuwi kwasababu wanawafanya waonekaniki silolote wa chochote mbele ya jamii kitu ambacho sitta alikataa alipokuwa anachangia na kuhoji mulianzisha vyama vingi vya nini, si ilikurekebisha pale tunapokosea na kuleta maendeleo kwa wananchi, 2.kutobadili sheria za uchaguzi na kutumia uchaguzi wa serikali za mitaa kama kupima upepo wa kisiasa kuwa wankubalika au laa, kulikuwa na kauli moja ilyo tolewa na mjumbe mmoja kuwa kwanini chaguzi zisiunganishwe ilkuokoa fedha zinazotumika hovyo kwenye changuzi za serikali za mitaa? hapa wale ambao hawapo kambi ya ufisadi waliunga mkono huku wengi wale mafisadi wakibisha wakisema kufanya hivyo nikukiangusha chama alisema......... rostarm

kulikuwa hata hamna la maana ilawalikuwa wanajaribu kujiokoa ila wakashindwa ndiyo amri ikatoka kuwa watumie vyombo vya habari kuwa mambo nishwari ila hakuna ufumbuzi kama ufumbuzi upo kwanini mwinyi waongezewe muda? angalieni mbali jamani, na wateteeni watanzania wa lalahoi kwa kupitia vyombo mbalimbali kwa kujadili kama hapaz jf naamini ipo siku itawezekana
 

Ni haki ya mtu kusikiliza na kusikilizwa lakini si haki kudanganya wengine kama unahitaji ajenda zilizozungumzwa angalia post no 298 ya bumbumbile hizo ndizo tunazitaka kuzichambua haijarishi kama ni nzuri au mbaya

habari unayoizungumzia ilitoka jana gazetini matukio aliyokuwa anatuletea kiwelo na wa 16 ni ya jana ina maana gazeti liliandika matukio ya siku hiyo hiyo na kutoka siku hiyo hiyo lazima nijulize legitimacy ya habari mnazotuletea vinginevyo nitakuwa napoteza muda tu hapa JF nitakuwa useless kama napokea chochote mradi kimeletwa na JF members

Date::2/15/2010
Kikao cha NEC-CCM ngoma nzito Dodoma
na Habel Chidawali, Dodoma

MKUTANO wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), umeanza mjini hapa ukiwa umefunikwa na usiri mkubwa kutokana na mambo mazito yanayojadiliwa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.
.........................................................................................
Mnamo saa 12:15 hivi jioni Spika Sitta, Mbunge wa Kyela Dk Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela walitoka ndani ya chumba cha mikutano na kukaa kwenye chumba kimoja kwa pamoja wakijadili jambo linaloonekana kuwa ni zito kwa muda wa takribani saa nzima.

Baada ya kuketi pamoja kwa muda huo, baadaye waliamua kuingia ndani ya kikao, haikufahamika kama waliitwa au la, lakini alianza kuingia Dk Mwakyembe akifuatiwa na mama Kilango na baadaye Spika Sitta.
 
..hakuna chochote kilichotokea ni business as usual. kama ulifuatilia kikao cha bunge na maazimio yaliyopitishwa basi utaelewa kwamba wananchi tumepigwa changa la macho.

NB:
..pia fuatilieni mahojiano kati ya Dr.Ndulu na kamati ya bunge mtajua tuna wabunge wa aina gani Tanzania. hawa watu wakishafika Idodomya wana-loose touch na maisha ya wa-Tanzania masikini.
 
Mkuu Pasco,

Hili mbona halihitaji Hesabu kali au roket sayans, kwani kila siku tunabweka humu, kuna jambo lolote uliloliona au kusikia kuwa UWT wamewajibika kwa sababu ya kelele au vielelezo walivyochukua toka JF? Upo uwezekano wa Afisa fulani kupita Jf kwa wakati wake na pengine pia akawa mchangiaji kama mimi na wewe, lakini aliyewekwa/waliowekwa Rasmi kwa kazi ya kumonita JF hakuna.Mimi si no 2 wala mfungua na mfunga geti kwa hesabu za Bongo ni kuweka mbili na mbli na jibu liko wazi.

Ndio mana nikasema ili washughulikie maswala tunayoyapigia kelele ni lazima tutafute mbinu nyingine ya kuwahusisha na kuwafanya wahusike. Na ikiwa tutaweza kufanya hivyo basi iwe kwa TAASISI zote muhimu tukianzia Ofisi ya Rais, Waziri mkuu, Bunge, Mahakama ,Polisi, Tukukuru na nyinginezo, Usitegemee Taasisi zote hizo hususan UWT ati watakaa wakingojea mimi na wewe tukerwe tuandike na wao wawe kazini, Hayendi hivyo mkuu.
 
Thread hii bomu, JF sio sehemu ya uzushi. Kama huna taarifa kaa kimya sio kutunga na kupotezana kifikira CCM NEC hawajadili haya yanayoongelewa hapa.

ANGALIZO.
Kenge,
Who ever belive in this Thread, could belive anything!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…