CCM pawaka moto Dodoma

CCM pawaka moto Dodoma

Wajumbe wasema Lowassa awajibishwe kwakuwa chama kimechafuka sana na asipo wajibishwa wasilaumiwe kwa yale yatakayo tokea.

Upande wa Lowassa wasema hamna cha kumuwajibisha Lowassa kama ni suala la ufisadi chama kiwajibike na si Lowassa

kwa hili niko upande wa Lowassa. Uchafu wa CCM chanzo chake si Lowassa. Lowasa hakuwa na ubavu wa kufungua milango ya BoT kukwapua pesa ya EPA. Lowasa ana makosa yake na CCM ina makosa yake ambayo ni mengi kuliko ya Lowassa. Kila mtu ababe msalaba wake.
 
jamani ya jana yalikuwa makubwa sana dodoma ccm ndiyo mwisho

Naona sasa unaifanya JF kama sehemu ya majaribio. Weka data zinazoeleweka, sio kusema tuu CCM ndiyo mwisho. Sasa hapo ndio unamaanisha nini? Audio recordings zenu ziko wapi? Hapa naona hamna ukweli wowote...Pasco jitoe kuwatetea hawa jamaa. Kuna harufu ya kutumwa kupima wana JF na kuwapoteza. Hilo wasahau kwa kweli.
 
Unajua CCM imedhihirisha udhaifu wake wa kuahirisha matatizo!

Hapa ndipo walikolifikisha hadi taifa letu,hivi kazi waliyopewa hao wazee watatu mmoja amekua rais for ten years akituwakilisha katika kutatua mataizo magumu ya nchi ,pia mwingine amekua spika wa bunge for more than Ten years still wameshindwa kuja na sufficient grounds za kusolve tatizo la camp mbili? Kumbe ndiyo maana Taifa letu bado ni maskini.

On the other hand, kwa kweli tunahitaji ukombozi.
 
Tuombe salama, kuanguka kwao kama chama ndio kuinuka kwetu kama nchi. Tulishawahi kusema mshikamano wa wezi ni hatari kwa jamii hivyo ukiona wezi wanagombana usisikitike kwani ndio maisha salama na thamani ya mtanzania vyaja!!

Shime yetu ni maombi waendelee hivyo hivyo.
 
Naona sasa unaifanya JF kama sehemu ya majaribio. Weka data zinazoeleweka, sio kusema tuu CCM ndiyo mwisho. Sasa hapo ndio unamaanisha nini? Audio recordings zenu ziko wapi? Hapa naona hamna ukweli wowote...Pasco jitoe kuwatetea hawa jamaa. Kuna harufu ya kutumwa kupima wana JF na kuwapoteza. Hilo wasahau kwa kweli.
.
Nadhani hawa jamaa wanatakiwa kuelimishwa ustaarabu na ukweli. Siamini ni watu wa kutumiwa hawa. Wanaonekana weupe sana hivyo wataunguza picha unless na aliyewatuma naye ni amateur.
 
Wajumbe wasema Lowassa awajibishwe kwakuwa chama kimechafuka sana na asipo wajibishwa wasilaumiwe kwa yale yatakayo tokea.

Upande wa Lowassa wasema hamna cha kumuwajibisha Lowassa kama ni suala la ufisadi chama kiwajibike na si Lowassa

Bwana Kilewo, acha kutujaza ngonjera hapa.
 
20751_303384212970_658587970_3501356_7035608_n.jpg


Hawa akili zao ni sawa na hiyo bendera wanayoipeperusha. Kazi ipo
 
jamani ya jana yalikuwa makubwa sana dodoma ccm ndiyo mwisho

Jamani mbona mnatufanya watoto. K, nina wasi wasi na status yako hapa jamvini!!!! To me, hizi ni ngonjera.
 
Yaani kwa kweli CCM wamefanya kosa lingine kubwa kisiasa..sasa wameahirisha tatizo,ugomvi wao na kuusogeza karibia na uchaguzi.

Ni kama mtu anapambana na chui asimdhuru mtoto halafu anakubali chui akimtisha na kujikuta amepeleka mapambano karibia na mtoto ambaye anaweza kudhurika na huyo chui.wana kazi kweli kweli,wacha unabii utimie!
 
agenda za kipuuzi walizo kuwa nazo jana ni 1. kuhakikisha upnzani haukuwi kwasababu wanawafanya waonekaniki silolote wa chochote mbele ya jamii kitu ambacho sitta alikataa alipokuwa anachangia na kuhoji mulianzisha vyama vingi vya nini, si ilikurekebisha pale tunapokosea na kuleta maendeleo kwa wananchi, 2.kutobadili sheria za uchaguzi na kutumia uchaguzi wa serikali za mitaa kama kupima upepo wa kisiasa kuwa wankubalika au laa, kulikuwa na kauli moja ilyo tolewa na mjumbe mmoja kuwa kwanini chaguzi zisiunganishwe ilkuokoa fedha zinazotumika hovyo kwenye changuzi za serikali za mitaa? hapa wale ambao hawapo kambi ya ufisadi waliunga mkono huku wengi wale mafisadi wakibisha wakisema kufanya hivyo nikukiangusha chama alisema......... rostarm

kulikuwa hata hamna la maana ilawalikuwa wanajaribu kujiokoa ila wakashindwa ndiyo amri ikatoka kuwa watumie vyombo vya habari kuwa mambo nishwari ila hakuna ufumbuzi kama ufumbuzi upo kwanini mwinyi waongezewe muda? angalieni mbali jamani, na wateteeni watanzania wa lalahoi kwa kupitia vyombo mbalimbali kwa kujadili kama hapaz jf naamini ipo siku itawezekana
 
Baada ya ze comedy ya Richmond na Ripoti ya Kiwira ambayo ndio inaonyesha kuwa hakuna lililotekelezwa na serikali mpaka sasa ila likamalizwa mlitegemea nini kifanyike?
 
Thread hii bomu, JF sio sehemu ya uzushi. Kama huna taarifa kaa kimya sio kutunga na kupotezana kifikira CCM NEC hawajadili haya yanayoongelewa hapa.

ANGALIZO.
 
http://www.cms.ccmtz.org/index.php?section=news&cmd=details&newsid=80

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM tarehe 14 – 15 February, 2010

UTANGULIZI

Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, imefanya mkutano wa kawaida tarehe 14 – 15 February, 2010 chini ya Mwenyekiti wa CCM, Mhe, Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma.

Katika mkutano huo Halamsahauri Kuu ya Taifa imejadili masuala mbali mbali kuhusu hali ya kisiasa nchini, maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani na Uteuzi wa wagombea wa nafasi mbali mbali. Aidha Halmashauri Kuu ya Taifa ilipokea na kujadili taarifa ya Kamati Teule inayoongozwa na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi.

1. MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU

1.1 Ratiba
Halmashauri Kuu ya Taifa, imepitisha ratiba ya CCM kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010. Kwa mujibu wa ratiba hiyo muda wa kuchukua fomu kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano na kwa Rais wa Zanzibar ni tarehe 1/7/2010 na kurudisha tarehe 8/7/2010. Kwa upande wa nafasi za Ubunge na Baraza la Wawakilishi kuchukua fomu ni tarehe 26 Julai na tarehe ya mwisho ya kurudisha fomu ni tarehe 28/7/2010.

Kwa upande wa Udiwani fomu zitachukuliwa tarehe 10/7/2010 na tarehe ya mwisho wa kurudisha fomu itakuwa 14/7/2010.
Kuanzia tarehe 31/7 hadi 7/8/2010 zitakuwa siku za wagombea ubunge, wawakilishi na madiwani kufanya kampeni matawini kwa mujibu wa ratiba na utaratibu utakaopangwa na kusimamiwa na Kamati ya Siasa za wilaya.

Wana CCM watapiga kura za maoni katika matawi yote nchini tarehe 8/8/2010 kwa wagombea wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.

Mkutano Mkuu wa CCM kwa ajili ya kuteuwa Mgombe Urais wa Jamuhuri ya Muungano umepangwa kufanyika tarehe 18/7/2010 hapa Dodoma, na pia kwa upande wa Urais wa Zanzibar uteuzi wa mgombea utafanywa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa tarehe 16 Julai 2010.

1.2 Kura za Maoni
Halmashauri Kuu ya Taifa, inahimiza kila wanachama wa CCM ahakikishe anajiorodhesha katika Daftari la wanachama katika tawi lake. Mwisho wa kujiorodhesha katika Daftari ni tarehe 30/6/2010. Baada ya tarehe hiyo CCM itasimamisha kupokea wanachama wapya hadi baada ya kura za maoni mwezi Agosti. Halmashauri Kuu ya Taifa imesisitiza kwamba kila mwanaCCM atakuwa na haki ya kupiga kura za maoni kwa wagombea wa nafasi ya ubunge, Baraza la Wawakilishi na udiwani, lakini watakao piga kura ni wale tu waliojiorodhesha katika Daftari la wanachama kwenye matawi yao.

1.3 Kufanya Kampeni kabla ya wakati
Kanuni za CCM zinaruhusu mwanachama kutangaza nia ya kugombea, hatas hivyo, Halmashauri Kuu ya Taifa , Imekemea vikali mwenendo wa baadhi ya wanachama wa CCM wanaowania kugombea Udiwani, Baraza la Wawakilishi na Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa kuanza kutembea matawini na kwenye kata na kufanya kampeni kabla ya wakati.

Halmashauri Kuu ya Taifa imekumbusha kwamba Kanuni za Chama Cha Mapinduzi kuhusu uteuzi wa wagombea wa CCM katika vyombo vya dola hairuhusu mwanachama yeyote kufanya kampeni kabla ya ya wakati uliowekwa rasmi.

Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa wito mahsusi na imeziagiza kamati za Maadili na Kamati za Siasa za ngazi zote kudhibiti hivyo. CCM inatambua kuwa kugombea nafasi ya uongozi ni haki ya kila mwanachama lakini ni lazima kila mwanachama azingatie utaratibu na kanuni zinazotawala shughuli za uchaguzi. CCM haitawavumilia wagombea watarajiwa wanaofanua fujo na vurugu kwa kuvunja kanuni katika kipindi hiki ambacho umakini unahitajika katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.

Aidha Halmashauri Kuu ya Taifa imekemea vikali viongozi wanaofanya kazi ya udalali wa kuwatembeza matawini wagombea watarajiwa kwani viongozi hao nao wanavunja kanuni na wametakiwa kuacha mara moja tabia hiyo vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

2. NAFASI WAZI KATIKA UONGOZI WA CHAMA
Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, imetangaza nafasi za uongozi katika mkoa wa Dar es Salaam na wilaya ya Shinyanga Mjini.

2.1 Nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar es Salaam
Nafasi ya wazi katika mkoa wa Dar es Salaam imetokana na Katibu wa Siasa na Uenezi, Ndugu Haji Sunday Manara kujiuzulu nafasi hiyo bada ya kutuhumiwa kukodi magari kwa njia ya udanganyifu na kuyaweka rehani.

Halmashauri Kuu ya Taifa inatangaza kwa wanachama wenye nia ya kugombea nafasi hiyo kuwa siku ya kuchukua na kurejesha fomu kuanzia tarehe 16 – 20/2/2010. Uchaguzi wa nafasi hiyo utafanyika kati ya tarehe 27 – 28/3/2010.

2.2 Nafasi ya Mwenyekiti Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Nafasi ya wazi katika Wilaya ya Shinyanga Mjini imetokana na kifo cha Mwenyekiti wa Wilaya, Marehemu Hassan Bhiku Lukindagila kilichotokea tarehe 8/11/2009.

Uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo imepangwa kufanyika kati ya tarehe 22-28/3/2010 na tarehe ya kuchukua na kurejesha fomu kwa wanaotaka kuwania nafasi hiyo ni kuanzia 16 – 20/2/2010.

3. UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2009, Chama Cha Mapinduzi kilipata ushindi wa asilimia 91.71, CUF walipata asiliamia 3.94, CHADEMA walipata asilimia 2.76, UDP asilimia 0.43, NCCR- Mageuzi asilimia 0.32, TLP asilimia 0.73, Chausta asilimia 0. 08, PPT – Maendeleo 0.01.

Halmashauri Kuu ya Taifa imewapongeza viongozi, Wana CCM na wananchi kwa ujumla kwa kukipatia ushindi mkubwa Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi huo ushindi ambao unadhihirisha kukubalika kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kiwango kikubwa.

Pamoja na kuwashukuru Watanzania kwa ushindi huu mkubwa, Halmashauri Kuu ya Taifa inawaomba waendelee kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

4. TAARIFA YA MWAFAKA (ZANZIBAR)
Halmashauri Kuu ya Taifa ilipokea taarifa kutoka Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar kuhusu mazungumzo ya maridhiano baina ya Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Seif Shariff Hamad.
Baada ya kujadili kwa kina taarifa hiyo Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa maazimio yafuatayo:-

(i) Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume kwa kuyakwamua mazungumzo ya Muafaka yaliyokuwa yamekwama kwa takriban miaka miwili tangu baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ta Taifa cha Butiama mwezi Machi, 2008.

(ii) Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (Zanzibar) kwa kutoa maelekezo sahihi kwa Kamati ya Wajumbe wa CCM wa Baraza la Wawaklishi kuhusu namna ya kushughulikia hoja binafsi iliyowasilishwa katika Baraza hilo kuhusu kuanzishwa kwa Serikali Shirikishi.

(iii) Halmashauri Kuu ya Taifa imelipongeza Baraza la Wawakilishi kwa kupitisha kwa kauli moja hoja kuhusu kuanzishwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa Shirikishi kwa kuzingatia maazimio ya Butiama.

(iv) Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhia na kupongeza uamuzi wa Kamati Maalumu ya Zanzibar kuhusu kuundwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa kwani hii ndio njia sahihi ya kuondoa chuki, uhasama na vurugu katika siasa za Zanzibar na badala yake itaimarisha amani, utulivu, umoja na ushikiano miongoni mwa Wazanzibari na hivyo kuharakisha kasi ya maendeleo.

(v) Halmashauri Kuu ya Taifa imetoa maelekezo kwa Kamati Maalumu (Zanzibar) na viongozi wa CCM wa ngazi zote Tanzania Zanzibar wafanye kazi ya kutoka elimu kwa umma kuhusu maana na manufaa ya Serikali Shirikishi inayotarajiwa kuundwa baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba, mwaka huu.

5. UCHAGUZI WA KUJAZA NAFASI 2 ZA WAJUMBE WA NEC KUPITIA KUNDI LA WANAWAKE

Kutokana na nafasi mbili za NEC kuwa wazi, baada ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa UWT, Ndugu Sophia Simba na Makamu Mwenyekiti wa UWT, Ndugu Asha Bakar Makame, Halmashauri Kuu ya Taifa imewachagua Ndugu Amina Makilagi na Ndugu Mwanaid Kassim Mussa kujaza nafasi hizo.
Katika uchaguzi huo, upande wa Tanzania Bara nafasi hiyo iligombewa na :

(i) Ndugu Amina Makilagi (190)
(ii) Ndugu Sakina Kabeza ( 3 )
(iii) Ndugu Elieta Switi ( 5 )

Kwa upande wa Tanzania Zanzibar waliogombea walikuwa ni:
(i) Ndugu Raya Talib Ali ( 25 )
(ii) Ndugu Subira Mohamed Ali (29 )
(iii) Ndugu Mwanaidi Kassim Mussa (145 )

6. TAARIFA YA KAMATI TEULE YA MZEE ALI HASSAN MWINYI

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imepokea na kujadili taarifa ya Kamati Teule inayoongozwa na Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi na kutoa maamuzi yafuatayo:-

(i) Halmashauri Kuu ya Taifa imeelekeza kuwa Kamati iendelee na juhudi za upatanishi kwa makundi ya Wabunge yanayohasimiana kwa lengo la kurudisha umoja na mshikamano miongoni mwa Wabunge wa CCM.

(ii) Halmashauri Kuu inaipongeza Kamati ya Mzee Ali Hassani Mwinyi kwa kazi nzuri inayofanya ya kurudisha utulivu na mshikamano miongoni mwa Wabunge wa CCM na hasa kwa kuzingatia kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.

(iii) Halmashauri Kuu ya Taifa inapongeza Kamati ya CCM ya Baraza la Wawakilishi kwa kudumisha umoja na mshikamano katika kutekeleza shughuli zao ndani ya Baraza.

(iv) Halmashauri Kuu ya Taifa inatambua kuwepo kwa shauku na utashi wa viongozi na wananchi wa Zanzibar wa kuimarisha utendaji wa kamati ya pamoja inayoshughulikia mambo ya Muungano chini ya Uwenyekiti wa Makamu wa Rais. Aidha, Halmashauri Kuu ya Taifa inaielekeza Kamati hiyo kuongeza kasi ya utendaji kazi na kutoa taarifa mara kwa mara.

7. KUWEKA UKOMO WA WAGOMBEA WANAWAKE WA VITI MAALUMU VYA UBUNGE, UWAKILISHI NA UDIWANI

Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea na kujadili ombi kutoka Baraza Kuu la UWT kwamba Viti Maalumu vya wanawake katika ubunge, uwakilishi, na udiwani viwe na ukomo wa vipindi viwili na baada ya hapo waende kugombea majimboni kwani baada ya vipindi viwili watakuwa wamepata uzoefu, uwezo, ujasiri na kujiamini kugombea majimboni.

Halmashauri Kuu ya Taifa imekubali ombi hilo la viti maalumu kuwekewa ukomo lakini utaratibu huu utaanza kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili kuwapa muda wa kujiandaa wanawake wabunge, wawakilishi na madiwani wa viti maalumu kwenda kugombea majimboni.

8. UTEUZI WA MAKATIBU WAPYA WA MIKOA
Halmashauri Kuu ya Taifa imefanya uteuzi wa Makatibu wa Mikoa wawili;

(1) Ndugu Catherine Nao - Aliyekuwa Katibu wa Wilaya Mjini

(2) Ndugu Avelin Peter Mushi- Aliyekuwa Katibu wa Wilaya Kinondoni

Watapangiwa vituo vyao vya kazi na ofisi ya Katibu Mkuu .

Wanachukua nafasi zilizoachwa wazi na Ndugu Valentine Senguo (Mtwara) na Ndugu Catherine Ndahani (Manyara) ambao wamepangiwa kazi Makao Makuu ya Chama.

9. MKAKATI WA CCM KUPATA FEDHA ZA UCHAGUZI
Mwaka 2010 ni mwaka wa uchaguzi na ili kufanikisha uchaguzi huu, Chama kinahitaji fedha. Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea mapendekezo ya namna Chama kitavyoweza kupata fedha za kugharamia uchaguzi. Njia zilizopitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ni hizi zifuatazo;

(a) Michango ya hiari kutoka kwa wanachama, viongozi, Chama na
Serikali (wabunge, mawaziri Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya)
(b) Kwa njia ya harambee za kitaifa na mikoani
(c) Kwa njia ya mitandao ya simu za mikononi.

Imetolewa na:
Capt John Chiligati (Mb),
KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI
15/2/2010
 
.
Luteni, nimesema, na ninasema tena siwajui! ila I was just thinking aloud and formulating my own hypothesis na modus operandi yao humo ndani.

Yote hayo nimefikiria tuu, assumptions nothing more, nothing less, ila pia, siwezi kuzuia fikra za mtu.
Kitu kimoja naomba nikuhakikishie Luteni, I take JF very seriously na kuitreat with much respect, mimi sio miongoni mwa wasanii humu ndani wenye mi ID kibao na wengine huleta maigizo ya kujiuliza na kujijibu, mimi ni Pasco tuu na Pasco ni mimi ingawa hili nalo ni pen name sio jina halisi!.

Ukimya wa hawa jamaa, unanipelekea kuamini ni kweli kwa jinsi nilivyo wafikiria.

Pasco hilo la Sitta kutoka nje ni la kweli kuna gazeti moja la hapa Tanzania nadhani ni Mwanachi limeripoti kuwa Sitta, Anna Kilango, Dr Mwakyembe walitoka nje na wakaingia kwenye ofisi moja na humo walikaa zaidi ya saa moja na nusu wakijijadiliana na badaye walirudi kwa nyakati tofauti akianza Mwakyembe, baadaye Kilango na mwisho Sitta.

Mimi hawa jamaa wa 16 na mwenzake Kileo naamini sehemu kubwa waliyokuwa wakiongea ni ya UKWELI ila sijui wanaongea kwa maslahi ya nani! Saa nyingine huwa najiuliza hawa jamaa wanaoshinikiza akina wa 16 walete vitu ni kweli wanavitaka hivyo vitu au 'kimtindo' hawavitaki na wanachofanya ni vitisho vya 'kimtindo??

JF!!!! I dare to listen!!!
 
Pasco hilo la Sitta kutoka nje ni la kweli kuna gazeti moja la hapa Tanzania nadhani ni Mwanachi limeripoti kuwa Sitta, Anna Kilango, Dr Mwakyembe walitoka nje na wakaingia kwenye ofisi moja na humo walikaa zaidi ya saa moja na nusu wakijijadiliana na badaye walirudi kwa nyakati tofauti akianza Mwakyembe, baadaye Kilango na mwisho Sitta.

Mimi hawa jamaa wa 16 na mwenzake Kileo naamini sehemu kubwa waliyokuwa wakiongea ni ya UKWELI ila sijui wanaongea kwa maslahi ya nani! Saa nyingine huwa najiuliza hawa jamaa wanaoshinikiza akina wa 16 walete vitu ni kweli wanavitaka hivyo vitu au 'kimtindo' hawavitaki na wanachofanya ni vitisho vya 'kimtindo??

JF!!!! I dare to listen!!!

Angalia sana haya magazeti ya Bongo mengi siku hizi yanatumia JF kama chanzo cha habari
 
Back
Top Bottom