Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rombo, April 17, 2025 kimetoa Semina kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Wilaya, kuhusu Mabadiliko madogo yaliyofanyika ya Katiba ya Chama hicho kwa Mwaka huu 2025.
Akizungumza mara baada ya semina Hiyo Katibu wa Siasa, Mafunzo na Uenezi wa chama Hicho Themistocles Massae amesema mbali na kutoa semina wamewaeleza wajumbe wa chama hicho kuhusu Utekelezwaji wa Ilani ya Chama cha CCM kwa mwaka 2020/2025.