Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Na Sadick Mtulya
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinaonekana kimeanza kuziogopa fedha za mafisadi, baadala yake kimeanza kuchangisha fedha kupitia kwa wananchama wake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2010 kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (meseji).
Hatua hii ya CCM inafuatia chama hicho kutuhumiwa kufadhiliwa katika uchaguzi mkuu na fedha zilizopatikana kwa njia ya ufisadi.
Hatua hiyo pia ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM aliyewahi kukigiza chama hicho kutafuta vitega uchumi ili kisitegemee misaada kutoka kwa wafadhili.
Mweka Hazina wa CCM taifa, Amos Makala alitangaza mpango huo juzi katika Uwanja wa majimaji, wilayani Songea, Ruvuma wakati akiwasimika makanda watano wa Umoja wa vijana UVCCM mkoani humo ambazo ziliambatana na kupongezana kwa kupata ushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Makala alisema CCM imefikia uamuzi huo ili kutoa fursa kwa wanachama wake wote kupata nafasi ya kukichangia chama hicho na kuondokana na kutegemea fedha za wafadhili ambazo nyingine ni ufisadi.
"Kuanzia hii leo (juzi) CCM inatangaza rasmi kuanza kuchangisha fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, na miongoni mwa mbinu tutakazozitumia ni kuchangia kwa njia ya simu za mkononi kupitia ujumbe mfupi(meseji)," alisema Makala.
Mweka hazina huyo alisema kutokana na CCM kuwa na wanachama milioni nne wanatarajia kupata zaidi ya Sh40 bilioni kwa kupitia mpango huo.
"Kwa kuwa tunawanachama milioni nne nchini kote na kila mmoja akichangia Sh1000, tuna uhakika kwa mwaka mmoja kupata Sh40 bilioni," alisema.
Makala alifafanua kwamba mpango huo pia utasaidia kuondoa dhana ya kuwa CCM ni chama kinachoendeshwa na mafisadi.
Katika sherehe za kusimikwa ukamanda mbunge wa Piramiho, Jenister Mhagama alisimikwa kuwa kamanda wa UVCCM wilaya ya Songea.
Mwenyikiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja amesema uamuzi wa CCM kuchangisha fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2010 njia ya ujumbe wa mfupi (meseji) ni kipimo tosha cha kuonyesha kama chama hicho kinakubalika au la.
"Siku zote chama si kampuni na kinajengwa na wanachama na hao wanachama pamoja na wakereketwa ndio vyanzo tegemezi vya chama chochote duniani. Sasa utaratibu huu ni kipimo tosha cha kuonyesha kama CCM inakubalika au la," alisema Mgeja.
Mgeja alisema pamoja na wazo hilo kuchelewa lakini limefika katika wakati muafaka na linakwenda na wakati.
Tayari Chama Demokarsia na Maendeleo (CHADEMA), kilishaanzisha mpango wa kupata wanachama wake kwa kutumia ujumbe wa simu ambao unatarajiwa kukipatia chama hicho fedha nyingi kwa ajili ya uchaguzi.
CCM hivi sasa inahusishwa na makada wake ambao ndio wachagiaji wakubwa wa chama hicho katika uchaguzi kuhusishwa na tuhuma za ufisadi hali ambayo chama hicho kinaonekana kukumbia uhalifu.
Katika hali ya kujisafisha zaidi chama hicho hivi sasa kimeamua kufanya uchunguzi maalumu wa kuwabaini wanachama wake wanaovujisha siri mbalimbali kutoka katika vikao nyeti vya chama hicho.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya baadhi ya siri mbalimbali zikiwemo za kuchafuana na kudhalilishana miongoni mwa mawaziri na wabunge wake katika vikao vya ndani vya chama kuwekwa hadharani.
Hali hiyo ilijitokeza mara nyingi ikiwa ni pamoja na zilizotovunjiwa hivi karibuni mjini Dodoma katika vikao vilivyofanyika chini ya kamati ya Mzee Mwinyi inayotafuta kiini cha mgawanyiko ndani ya CCM.
"Kwa kweli tunasikitishwa na tabia ya wana CCM kuvujisha siri za vikao halali vya chama. Kutokana na mwenendo huu tunafanya uchunguzi maalumu ili kuweza kuwabaini wanaovujisha siri zetu," alisema Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa juzi jijini Dar es Salaam.
Msekwa alisema pamoja na kuwepo kwa tabia ya uvujishaji wa siri hizo, bado hawajapata sababu za siri hizo kuwekwa hadharani.
Bila kuzitaja mbinu watakazo zitumia kuwabaini wanaovujisha siri hizo, Msekwa alisema tabia hiyo wataithibiti.
"Pamoja na kuwa bado hatujapata sababu za siri zetu kutolewa kabla ya muda, tunaamini tabia hii tutaithibiti na kuiondoa ndani ya CCM," alisema Msekwa.
Msekwa alisema katika kurejesha maadili kwa wanachama wake CCM imeamua kuvirudisha vyuo vya mafuzo ya uongozi wa siasa nchini.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kubainika kuwepo kwa madhara makubwa ya kimaadili katika siasa na pia chama hicho kupata uwezo wa kifedha.
Msekwa alifafanua kwamba, madhara hayo yametokana na viongozi wengi wa siasa hivi sasa kutopitia katika vyuo maalum vya mafunzo ya uongozi.
"Kwa kuanzia, CCM inatarajia kufungua chuo chake kipya cha mafunzo ya uongozi mkoani Iringa na chuo hiki si tu kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanasiasa pekee bali hata kwa wafanyakazi wengine wa chama ambao watakuwa wanakwenda kupata mafunzo mbalimbali," alisema Msekwa.
Makamu mwenyekiti huyo alisema ujengaji wa chuo hicho umetokana na CCM kupata uwezo wa fedha wa kuendesha chuo hicho ikiwemo kuwalipa walimu.
Alisema awali vyuo vya mafunzo ya uongozi ikiwemo cha Malimu Nyerere vilikuwa vikiendeshwa kwa fedha za ruzuku iliyokuwa ikitolewa na Serikali lakini vilikufa kutokana kuacha kuchukua ruzuku hiyo mara baada kuingia kwa vyama vingi vya siasa 1992.
"Mbali na chuo cha mafunzo ya uongozi cha Mwalimu Nyerere ambacho watu wengi ndio wanakikumbuka hadi leo. Tulikuwa na vyuo sita vya namna hiyo katika kanda, vilikufa kwa sababu CCM kupitia Nec iliamua kuacha kuchukua ruzuku ya kuviendesha kutoka serikalini," alisema Msekwa