Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Katibu wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga amewataka wazazi kuacha kushiriki mahusiano ya kimapenzi na vijana wadogo wanaowazidi umri, akisema vitendo hivyo vinawaharibu vijana na kuwadhalilisha wazazi wenyewe.
Akizungumza leo, Machi 14, 2025 katika ziara ya kukagua uhai wa chama na kutatua changamoto zinazowakabili wanachama katika Kata ya Lyabukande, Halmashauri ya Shinyanga, Katibu huyo ameeleza kuwa baadhi ya kinamama wanajihusisha na vitendo hivyo, hali inayowafanya vijana kuwadharau na kuwabatiza majina kama "mashangazi."