CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!

CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Salaam wana jamvi,

Nimesoma maazimio ya kikao cha NEC ya Chama cha Mapinduzi, yameniacha na maswali bila majibu.

Kuna wengi hawajui,wanadhani CCM ni chama tuu cha siasa,kama vyama vingine, CCM sio chama tuu cha siasa kama
vyama vingine ,CCM ni chama na ni dola,hivyo CCM ni Chama dola, CCM ni dola!.

CCM ilipozaliwa ile 77,katiba ya CCM,ndio katiba ya JMT ya 1977,enzi hizo za chama kimoja,CCM ndio ilikuwa supremacy kuongoza Dola,hivyo CCM kwa chama kushika hatamu.

Tulipoingia mfumo wa vyama vingi,tulifanya
Mabadiliko ya katiba cosmetics tuu kwa kubadili maneno tuu ku replace neno chama kimoja,into vyama vingi,lakini katiba ni ile ile ya chama kimoja,CCM bado ni chama dola ni dola!

Mwenyekiti wa CCM ndie rais wa nchi,mkuu wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu!。There is no any dividing line between Mwenyekiti wa CCM , mkuu wa nchi,mkuu wa serikali,na CinC,is the one and the same person!.

Hivyo CCM sio tuu ni chama tawala, bali pia ni chama dola, ni dola !.

Hivi kweli CCM kama chama kina uwezo wa kumhoji spika wa the legistlature jinsi anavyoliendesha Bunge?!

CCM kimeunda kamati ya wenye busara kufuatilia uendeshaji wa Bunge!.

Madudu yote ya the executive CCM haijayaona wala kuyahoji kwa vile mkuu wa the executive ni mwenyekiti wa CCM hivyo CCM ni excutive party kinachodhibiti Bunge na kudhibiti judciary kunafuatia!

Je, tunarudi tena kwenye party supremacy?

CCM na Bunge nani zaidi?...ni
CCM!.

Naomba kuwasisha.

Pasco
 
Sioni cha kujadili hapo.

Wafu wanaendesha Misa ya kumzika mfu mwenzao, sisi tulio hai tufanye nini??

"Uimara wa kamba imara ni Imara sawsawa kabisa na pale penye ubovu na udhaifu mkuu"

CCM hawawezi kujiokoa wao kama CCM kwa kujitoa kafara mikia yao, masikio yao,makalio yao au tupu zao, damu na uhai wao unaitwa dhidi ya uovu ulozidi haki.

Wakimla Mzee Six mzimamzima wajue mwingine kati yao zamu yake itawadia.
 
CCM kinaishi kwa sababu ni chama dola tu, nje ya hapo hakina uhai.

Hakina uhai kimaadili, kijamii, kisiasa, na sasa kiuchumi pia. Tukiacha mengine na kuzungumzia kidogo kiuchumi, ni kwamba, hata uchaguzi huu, kampeni zake zinagharamiwa na serikali.

Magari yanayotumika yenye rangi ya kijani ni ya Serikali yaliyobadilishwa rangi kwa muda. Gharama za wapambe wake akiwemo Waziri Mkuu na makamu wa Rais ni gharama za serikali, msururu mkubwa wa magari kwa wote hao ni gharama za serikali, matangazo ya TBC ni gharama za serikali, nk.

CCM ingeachwa peke yake, bila shaka pumzi ingekuwa imeshaka zamani. Hivyo, mara tu CCM itakapokosa kuwa chama tawala, usiombe kugombea uenyekiti wa chama hicho. Kitakufia mikononi mwako.
 
Spika ni mjumbe wa kamati kuu ya Ccm,kuhojiwa namna bunge linaisimamia vipi serikali na kutunga sheria sio jambo baya.

Unaposema executive haihojiwi sababu rais ni mwenyekiti,kwani hapa Tanzania hamna check and balances? Bunge halihoji utendaji wa executive?
 
Spika ni mjumbe wa kamati kuu ya Ccm,kuhojiwa namna bunge linaisimamia vipi serikali na kutunga sheria sio jambo baya.

Unaposema executive haihojiwi sababu rais ni mwenyekiti,kwani hapa Tanzania hamna check and balances? Bunge halihoji utendaji wa executive?
Nakubaliana na wewe....

Bunge ndio nguvu za kuongoza nchi zinapoanzia.....Bunge linakuawa chini ya Spika, na Spika anakuwa chini ya Chama. Kama anakwenda nje ya mstari wa chama ni sahihi kabisa kuhojiwa.
 
Hakuna wa kujadili huu upuuzi wako. Acha kushoboka na hizi threads zako zilizojaa pumba!
 
Kwa kweli zile hela za kampeni kuwalipa wasanii ni za serikali tu.. Hivi ccm wanavitega uchumi gani vya kuwawezesha kumudu gharama zote zile za kampeni kuanzia kukodi wasanii na mengineyo?
 
Aisee!! Kwa uzi huu ulioenda shule leo hii ukiulizwa utashangaa unaukana mchana kweupe! Kisa tu umeunga mkono juhudi.

Eti leo hii unatakiwa umuunge mkono Gwaji boy kwenye kampeni za ubunge kule Kawe ili chama dola kishinde! Ngoja tusubiri uchaguzi upite tuone kama mzee atakukumbuka kwenye uteuzi.

Hakuna namna. Fuata nyayo za watangulizi wako akina Kitila, Kafulila, nk. Ila kiukweli Maisha ya kufungwa mdomo, mikono, macho, miguu na masikio ni magumu sana. Kisa tu mkono uende kinywani!!!
 
So what , watang'oka tu iwe jua , iwe mvua .
IMG_20201005_081937.jpg
IMG_20201005_081859.jpg
 
Kila nikiangalia, mahesabu yangu yananiambia kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 MAGUFILI anapigwa asubuhi na mapema tu

1. Kura za Kaskazini zitamkataa vibaya mno
2. Kura za kusini zitamkataa katakata
3. Kura za Waislamu ndiyo kabisaa maana teuzi zake nyingi wamezilalamikia
4.Kura za mji mikubwa kama Mbeya na Dar es salaam atazisikia katika bomba
5.Kura za Singida kwa Tundu Lissu na Nyalandu hizo asahau
6.Kura za wafanyakazi ambao hajawaongezea nyongeza za mishahara atazisikia katika bomba
7. Kura za Vijana wasio na ajira, Vijana wa vyuoni wanamwangalia wanasema hiiiiiii etc
8.Kura za Watanzania walioko kwenye social media wengi hawamkubali
9. Iringa atapigwa asubuhi na mapema tu
10.Kagera ndiyo kabisa wanasubiri wapitishe hukumu
11. Kule Kigoma kwa Mwami Zitto ndo asahau kabisa
12. Wafanyabiashara wanaosumbuliwa kodi na TRA wamenyuti hawana maneno mengi wanamsubiri kwa hamu wamsulubu
13. Wenye Magari waliogeuzwa ng'ombe wa kukamuliwa pesa na Matrafiki hawa wanamgojea kwa hamu kubwa wamuonyeshe kilichomnyoa kanga manyoya
 
Miaka 11 badae maneno yako yanabiproved positively lakini wewe saivi umekuja kuwa worship team

Paskal zaman ulikuwa na akili sana.
Mkuu mugah di matheo, japo kwa sasa na mimi ni kada, sijawahi kuwa a praise & worship team!, ukiona napongeza kitu ujue ni kitu cha kweli bonafide genuine kinachohitaji pongezi!.

Na licha ya kupongeza, kukitokea jambo linalohitaji ukosoaji, huwa nakosoa.
P
 
Hilo mbona linajulikana

Ni sawa na kusema,wakati wa muchi
Refa wewe,lines man wewe,msimamiz wa mechi na waamua matokeo wewe

Ova
 
Back
Top Bottom