Uchaguzi 2020 CCM Tabora hali tete, kampeni za CHADEMA zawachanganya, Waanza kuwadanganya wazee kwa vitambulisho vya matibabu ya bure, wazee wastuka!

Uchaguzi 2020 CCM Tabora hali tete, kampeni za CHADEMA zawachanganya, Waanza kuwadanganya wazee kwa vitambulisho vya matibabu ya bure, wazee wastuka!

Acha mambo yako wewe Mungu kashuka Tanzania kwa kutuepusha na COVID 19 na hii inatokana na kuongozwa na Kiongozi mwenye hofu ya Mungu na mcha Mungu na si mwingine ni Mzalendo wa kweli JPM.

October 28th tutampa kura kwa upendo na wivu Mkubwa shujaa huyu JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Eti hofu ya Mungu labda Mungu wa kushona maana Mungu wa kweli hakubaliani na wauaji
 
Kiongozi anaye wakumbusha wananchi wenzake kumlilia Mungu ni wakumheshimu sana.

JPM ametuoneshea kuwa inapokuwa kwenye matatizo ya kukata tamaa jibu lipo ni KUMUOMBA MUNGU, unajuaje pengine maombi yetu wachache yameikomboa Africa

October 28th jura zote za ndio ni kwa JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Kiongozi anetubagua kwa itikadi za vyama ni. Mnafiki! Muongo! hana hofu ya Mungu! anajifikiria yeye tu!! Kiongozi aneua na kutesa watu wake!! kiongozi anefukarisha watu wake huyo ni wakumuogopa! jiwe hatufai!!
 
I see. Basi wamepiga pesa ndefu sana, kwa sababu kuna
  1. Mwambe wa Mtwara
  2. Kafulila
  3. Katambi
  4. Silinde
  5. Waitara
  6. Mollel
  7. Mtulia
  8. Lijua LIPOLE (likali)
  9. Gekul nk
Habari ndio hiyo
 
Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana ! hatimaye amejibu kikamilifu maombi ya Watanzania baada ya kuwaamsha Wazee wa Tabora waliokuwa kwenye usingizi wa pono, ambao sasa wameapa kuiteketeza kabisa ccm bila huruma kwa kukataa hongo ya matibabu ya bure iliyoletwa kwa lengo la kuwarubuni ili waichague tena CCM, chama kilichoshindwa kwa miaka 60 kuboresha maisha ya Wananchi .

Ushahidi huu hapa.

Sasa kama hawakupata awamu ya kwanza unataka wasipewe kabisa? WanaCdm tunaibishana.
 
Kuna wazee kule Dodoma walilalamika kuhusu matibabu. Ofisi ya Mkurugenzi kwa kutumia ofisi za Kata ikatuma wafanyakazi wao kuja kuchukua picha za wazee wote wa Jiji na baadae wakatengenezewa vitambulisho. Waliambiwa kuvitumia hivyo vitambulisho kila waendapo hospitalini ili kupata matibabu ya bure.

Cha kusikitisha ni kwamba hivyo vitambulisho havikubaliki mahali popote hata huko vilikotolewa! Sera ya Wazee ya 2003 ipo lakini hakuna Sheria yeyote ambayo inawawezesha Wazee kupata matibabu bure kama ilivyoainishwa katika Sera hiyo. Hivyo hata hao Wazee wa Tabora wajue kabisa hicho ni kiini macho tu. Watumie kichinjio chao kwa busara ili kuweza kupata haki zao na si vinginevyo.
Leo kwa mara nyingine Wazee wameahidiwa kwamba miaka mingine mitano ijayo, itatungwa Sera ya Wazee. Mwaka 2003 Sera ya wazee ilitungwa na hadi leo baada ya miaka 17 bado Sheria inayoendana na Sera hiyo haijatungwa. Wazee wamekuwa wakililia Sheria na wala si Sera. Tujaribu kuwa wakweli, ni dhambi mbaya sanaa kuwahadaa Wazee ambao siku zao za kuishi zinayoyoma kila uchao. Kwa miaka yote hii 17 zimetolewa ahadi lukuki kuhusu kutungwa kwa Sheria hiyo. Sasa tena wanarudisha kila kitu nyuma na kuanza upya. Wazee subirini tena miaka mingine kama hiyo kabla kilio chenu hakijajibiwa, na kiukweli wengi watakuwa wametangulia mbele ya haki.
 
Polepole kakiua Chama kwa tamaa za kijinga huwezi kumnunua Waitara kwa Milioni 600 halafu mnazigawana.
Endapo Magufuli atapita Basi viongozi wengi wa CCM watapigwa chini na wapambe wengi wa Magufuli watalia na kusaga meno
 
Leo kwa mara nyingine Wazee wameahidiwa kwamba miaka mingine mitano ijayo, itatungwa Sera ya Wazee. Mwaka 2003 Sera ya wazee ilitungwa na hadi leo baada ya miaka 17 bado Sheria inayoendana na Sera hiyo haijatungwa. Wazee wamekuwa wakililia Sheria na wala si Sera. Tujaribu kuwa wakweli, ni dhambi mbaya sanaa kuwahadaa Wazee ambao siku zao za kuishi zinayoyoma kila uchao. Kwa miaka yote hii 17 zimetolewa ahadi lukuki kuhusu kutungwa kwa Sheria hiyo. Sasa tena wanarudisha kila kitu nyuma na kuanza upya. Wazee subirini tena miaka mingine kama hiyo kabla kilio chenu hakijajibiwa, na kiukweli wengi watakuwa wametangulia mbele ya haki.
😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom