CCM Temeke ndani ya Kashfa nzito



Hivi hizi fedha za marejesho ni sehemu ya mapato ya halmashauri? Kwa ufahamu wangu mdogo sidhani kama kumbukumbu za marejesho ya fedha hizi huhifadhiwa. Kuna uwezekano mkubwa zinaishia mifukoni mwa watu. Na pia kuna uwezekano mkubwa wakopaji wengi hawazirejeshi.
 
Bibie, kama ni kweli, rudisha haraka fedha unazodaiwa.
 
Nadhani huu uchunguzi wa kuwabaini hawa ungefanyika nchi nzima kata kwa kata, mtaa kwa mtaa. Viongozi wengi wanaishi kama mchwa mnakula kweli kweli. Kupata mkopo wa vikundi ni kero unazungushwa kweli. Mara mnaambiwa mwandike Katiba, mkiandika na kuleta inakataliwa baadae mnauziwa na wao hao hao CCM kata Tshs 30000/= mpaka 50000/= . Ili ipitishwe na afisa maendeleo. Huu ni wizi mkubwa kwa vikundi vya watu masikini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…