Kufa c mwiko
JF-Expert Member
- May 26, 2013
- 752
- 320
Nianze kwa kuwapa pole na kuwaombea kwa mwenyezi Mungu ndugu zetu wote waliopata majanga ya mafuriko popote nchini Tanzania, pili nimpe pole Mh. Raisi mama Samia suluhu Hassan kwa kitendo cha kuzalilishwa kwenye mitandao, binafsi naamini ni utamaduni mbaya sana na hasa niliposikia waratibu wa huo uzalilishaji ni Mawaziri ambao ni wanachama wa chama Cha mapinduzi (CCM), niviombe vyombo vyote vya usalama na uchunguzi, vilifanyie kazi jambo hili na kuwaweka bayana wahusika kisha kuwapeleka mahakamani na iwe wazi kama wanavyofanya kwa wauza Bangi na gongo ili kufuta huu utamaduni wa hovyo.
Kuna jambo lingine nimelishuhudia juzi nikajiuliza, hivi ni kwanini hiki chama kikongwe CCM kinaichezea AMANI ya nchi hii? Nilienda kumtembelea jirani yangu muda mfupi akaja mama mmoja akijitambulisha kuwa ni balozi wa CCM kwenye shina la mtaa huo akiwa na daftari na peni akatuomba vitambulisho vya NIDA pamoja na vya mpiga kura.
Tukamuliza unavitaka vya nini, akasema anahitaji namba za hivyo vitambulisho pamoja na namba zetu za simu ni maandalizi ya uchaguzi mwaka huu. Tukamwambia sisi sio wanachama wa CCM akasema nachukua kwa wote kisha mtapigiwa simu, tukamtosa.
Sasa leo tena asubuhi na mapema kaja balozi mwingine mwanaume nyumbani kwangu kudai namba za hivyo vitambulisho nikakataa, akaniambia Ili zoezi ni la nchi nzima kama wewe unakataa!
Sasa nikabaki najiuliza, ina maana hawa CCM ndiyo hiyo Tume Huru ya Uchaguzi? Wasi wasi wangu zile kura ambazo zinaletwa zikiwa tayari zimeshapigwa mchakato wake ndio unaanza sasa, tafadhari CCM tulinde AMANI ya nchi yetu chama chenu ni kikongwe hakuna sababu ya kuiba uchaguzi tumieni ukongwe wa chama chenu.
Asante.