MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Bila shaka hamna chama tawala barani Afrika kinachoenjoy upinzani dhaifu kama CCM.
Chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema ni moja ya vyama ambavyo unaweza kuviendesha kisaikolojia kutoka uchaguzi mmoja mpaka uchaguzi mwingine katika kipindi cha miaka mitano, na ninashukuru hilo linawezekana na linafanyika ndani ya CCM.
Siku Chadema wakiamka kudai katiba mpya, CCM inaweza kumtumia moja ya makada wake mwaminifu(mf Diallo) kutoa kauli tata, basi Chadema wote wataacha kujadili Chadema watahamia kwa Diallo.
Wakianza chokochoko tena, kwa kupitia mpango maalum Sabaya anaweza kutoka kwa dhamana au Makonda anaweza kwenda kuripoti kituo cha polisi basi Ufipa wote watahamia huko na kuacha tena suala la katiba.
Baada ya muda sio mrefu miaka mitano itakuwa imekatika hivi, uchaguzi huu hapa na hawana cha kuonesha kwa wapiga kura, wanapigwa tena chini. Wanarudi kulalamika kwa wananchi.
Naiona miaka 50 mingine ya CCM madarakani hii hapa kabisa.