CCM tusiache kulindana, Tunaona wenzetu wanavutwa mmoja mmoja mahakamani

CCM tusiache kulindana, Tunaona wenzetu wanavutwa mmoja mmoja mahakamani

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Sioni shida kujitokeza na kusema ile ada yetu ya kulindana tusiiache, sasa kumekuwa na msukumo wa watu wasiojulikana kutaka au kuwafikisha mahakamani wenzetu ambao wakati ulee walikuwa ndio tegemezi na walisimamia na kukipa chama uthubutu.

Hizi hila za wapinzani koko zinaonekana kuzaa matunda wamemfunga Kijana ngangari kabisa Ole Sabaya kama haitoshi wanamnyemelea Braza Paul Makonda kesho na kesho kutwa Nape na wengine wengi itakuwa wamo kwenye list of shame yao,

Tufahamu hawa hawakitakii mema Chama Chetu cha CCM ,wanajenga chuki ndani yetuwanataka tuchukiane ili watuvamie na kututawala, ni lazima tuzinduke na ile taratibu ya kulindana tusiiwache.

Kwa vyovyote vile hiki kitu ni lazima kiwepo, tusiwache tukavurugwa na vyama vya ukoo,Chama chetu ni Chama Dume na lazima kingurume na kina taratibu zake, tufuate taratibu zetu ikiwemo kulindana.
 
Umechelewa

Kesi za jinai hazina ukomo wa muda.

Hata Sisi ndani ya chama chetu ccm hatutaki uhalifu, kwa hiyo kulindana HAKUNA.

Kama ulitenda maovu kipindi cha jiwe, nk, utaburuzwa ubaoni tu sooner or later
 
Kuwa na kadi ya ccm tu
Wakuna nazi

2960778_AMf6ME.jpg
 
wanaCCM wenzangu mmeona hayo maneno yaliyopo juu,hao ndio katika kundi la mikakati wanaotaka kwanza kutugpmbanisha na tuonane maadui,amini amini nami nawaambia maadui zetu wapo mbioni kuona tunafarikiana ili mambo yao yawe supa. Tusipoamka na mapema mwishowe watafurahia.
Saa ya kupambana nayo ni sasa na tushikamaneni na kulindana,hawa hawataishia kwa Sabaya tu ,wanawatafuta wengi ili kuona CCM inasambaratika makundi ,kama mnavyoona eti ndani ya CCM kuna mpasuko.Jamani hivi tusikubali kugawanywa eti wanadai kuna Sukuma gang kuna Samiya gang ,wanajaribu kuunga uunga na kuchukua mambo ya maamuzi yetu na kuyafanya watu waamini sababu ni kuwa kuna makundi.

Tuwaambie CCM ni ile ile na haitabadilika ,tuzidi kulindana na hawa wanaonyakuliwa tufanye juu chini tuwalinde na kuwarudisha ndani ya mstari.
Yaani wamejipanga kuona anafuata Makonda kisha Bashiru Polepole mmoja mmoja wanatudhoofisha kwa kusababisha tuanze kukamatana na kufungana. Wamewalenga wapambanaji mahiri . Tulindane kwa hali na mali ili tuendelee kushinda na kuilinda anzania na vibaraka wanaokimbilia Ulaya na wengine kujipanga kutaka kusababisha majanga humu nchini. tusikubali kugombanishwa ,kwani CCM tuna taratibu zetu.
 
Mheshimiwa Magufuli alisema wazi kama hutaki kuwa na sisi hukubaliani na taratibu zetu ondoka,jitoe kaa pembeni ,sasa hawa wagagagigikoko wasisababishe tuwe tunakamatana wenyewe kwa wenyewe wakati tupo ndani ya kuongoza nchi na sisi ndio wenye dola.
Tukanyane wenyewe kwa wenyewe tuonyane wenyewe kwa wenyewe na tulindane ,vidudu watu wasituvuruge.
 
Back
Top Bottom