Uchaguzi 2020 CCM tuwe wakweli, mpaka mwisho wa kampeni tunaweza tukashindwa vibaya sana

KWA akili zangu timamu upinzani unge waachia KILA kitu CCM
Serikali za mitaa,udiwani, Ubunge na urais Ingenoga sanaa.
Inafikirisha....
Ifikapo 2025 tuwapime.
Miaka 60 muko madarakani lkn mpaka Leo naona bado nchi inaomba mpaka msaada wa kuziba mashimo ya vyoo

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
CCM bado sana kutoka marakani,bado tena sana tu.yanayotokea sasa pia yashatokea chaguzi zilizopita lakini CCM ni chuma cha pua,ushindi wa CCM mwaka huu ni zaidi ya 90%.
Madaraka hupofusha. Sadam Hussein mpaka anachojolewa shimoni bado alikuwa anaamini majeshi yake yangeyashinda yale ya Marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kushindwa utashindwa wewe na familia yako na sio CCM
 
Madaraka hupofusha. Sadam Hussein mpaka anachojolewa shimoni bado alikuwa anaamini majeshi yake yangeyashinda yale ya Marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sadam wakati anatawala Iraq kuliwa akuna vita na amani ilikuwepa ila baada ya Sadam kuchojolewa kwenye shimo kama unavyosema Iraq apakaliki.
 
Wewe hujawahi kuwa CC M!

Siku hizi wapinzani wamekuwa watoa ushauri kwa CCM!

Kwani hutaki CCM ishindwe uchaguzi!

Yaani kuna wajinga wanaamini CCM itashindwa katika Uchaguzi huu!
Wajinga zaidi ni wale wanaoamini CCM itashinda, ila wanajua itashinda kwa mbinu zisizo halali, halafu sijui umejuaje huyo ndugu ni mpinzani au ndio kukurupuka tu lile jiwe likiguswa.
 
KWA akili zangu timamu upinzani unge waachia KILA kitu CCM
Serikali za mitaa,udiwani, Ubunge na urais Ingenoga sanaa.
Inafikirisha....
Ifikapo 2025 tuwapime.
Mbona walishaachiwa toka tunapata uhuru 1961 mpaka vyama vingi vilipoanza 1992 lakini hakuna walichofanya dogo.
 
Kama ubaguzi wa kaburu dhidi ya Waafrika wenzetu wa Afrika haukuwa mzuri, ubaguzi wa Magufuli dhidi ya watu wa vyama pinzani na dhidi ya watu wa kanda nyingine, hauwezi kuwa mzuri kamwe.

Ili kumuenzi Mwalimu Nyerere aliyeupiga vita ubaguzi wa aina yoyote ile kwa nguvu zake zote, tumkatae mbaguzi Magufuli kwa nguvu zetu zote. Watanzania wote wana haki sawa ndani ya Taifa lao. Yeye kwa kinywa chake ametamka wazi kuwa anawabagua watu kwa misingi ya vyama na makabila.

Anaposema, 'mnichague mimi ni msukuma mwenzenu', by implication anataka kusema wengine tusimchague kwa vile siyo wa kabila letu. Labda ndiyo maana anapiga kampeninl kanda ya ziwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sadam wakati anatawala Iraq kuliwa akuna vita na amani ilikuwepa ila baada ya Sadam kuchojolewa kwenye shimo kama unavyosema Iraq apakaliki.
Hakukuwa na vita!! Kasome historia ya Iraq, uone Sadam alivyowaua raia wake kwa gas ya sumu, kwa sababu tu kwenye eneo hilo la Kaskazini kulionekana kuna watu wengi waliokuwa wakimpinga.

Lakini pia ni uwongo kusema kwamba wakati wa Sadam Iraq ilikuwa na amani. Iraq haikuwa na amani bali ilikuwa na utulivu.

Anayefanya Iraq isitawalike mpaka leo ni Sadam. Madikteta wote Duniani hawatengenezi mifumo, hivyo akiondoka tu lazimu mtaangukia kwenye vita. Madikteta wanapenda kuua mifumo, na hupenda matakwa yao ndiyo yawe mfumo na sheria. Na hiyo imeanza taratibu hapa kwetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikia kutengwa ndio huko,CCM wengi wameshaicha mkono kampeni wamebaki kuvaa magwanda hadi wakati muafaka utakapofika hizo sare watafutia magari.

hata Chakubanga ametaharuki ameacha kuchekacheka hovyo kumchekea ovyo Magufuli hata jambo alichekeshi,Magu kamshtukia polepole.
 
Ila kiukweli tukuacha Unafiki, Kunasehemu Magu Ana mess up Sana.
Hasa kwenye hizi Kampeni.

Anahitaji Kupumzika Akae sawa kwanza. Narudia hii mtu kuwa Raisi wakati huo huo ni mgombea imekaa vibaya.
Inapaswa kuwe na Kasecretariet ambayo inapaswa iwe chini ya neutral person. Mda huu.

Ili Aliyekuwa Raisi apate mda wa kumpumzika. Na kujipsnga kufanya Kampeni akiwa na kofia moja.

Hii itapunguza Malalamiko toka Upinzani, pia inampunguzia mzigo huyo mgombea Uraisi.
 
Wewe hujawahi kuwa CC M!

Siku hizi wapinzani wamekuwa watoa ushauri kwa CCM!

Kwani hutaki CCM ishindwe uchaguzi!

Yaani kuna wajinga wanaamini CCM itashindwa katika Uchaguzi huu!
Kimbia mapema nyumba isha anza kushika moto
 
Hatuko consistent we ave many tongues. Leo litasemwa hivi kesho lilelile litasemwa tofauti.
 
Hawa jamaa ni wa ajabu sana, wameficha silaha zao pembeni za kampeni kama vile katibu mkuu na naibu wake, mwenyekiti wao pia wamemtangulizia Mgombea na mgombea mwenza na viongozi wa kikanda. Wanataka mwishoni watumalize sisi ambao kila safari tunaambatana timu yote.[emoji1536][emoji1536][emoji1534]
 
Hiyo power vacuum watawala hawataki kuisikia....
ni kama vile kumpeleka mkeo akalale kwenye nyumba ya mabachela....
 
Hoja ya kuigawa nchi katika majimbo ndiyo hiyo unasema. duuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…