JACADUOGO2.
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 930
- 220
Kwa kweli Jimbo la Rorya linaonekana kutawaliwa kwa maslahi ya watu wachache ambao kwa ujumla siyo waadilifu na wanafanya maamuzi kwa maslahi yao binafsi na siyo kwa maslahi ya wananchi wa jimbo la Rorya. Haya yote ni kutokana na sababu kwamba jimbo linatawaliwa na darasa la saba (Ndugu, LAMECK AIRO kupitia CCM) ambaye hana hili wala lile katika fani ya uongozi. Ndiyo maana tangu mwanzo sisi wanafunzi tunaosoma vyuo vikuu tulimpinga tangu mwanzo lakini alifanikiwa kuwarubuni wananchi kwa hela. Tatizo kubwa hapa ni uongozi wa darasa la saba (LAMECK AIRO), uchu wa madaraka, ubinafsi, chuki, fitina na kutokujua maana ya uongozi katika jimbo Rorya. Nawaahidi wanarorya kuwa ukombozi unakuja 2015 kupitia CHADEMA. Wasiwe na wasiwasi. Tuko pamoja.
JACADUOGO2, DODOMA UNIVERSITY.
JACADUOGO2, DODOMA UNIVERSITY.