Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Tukiwa katikati ya mtanange mkali wa kidemokrasia wa CHADEMA ambao umetoa usawa na fursa kwenye kugombea nafasi mbalimbali hivo kuibua vipaji vipya vya uongozi; CCM waliibuka na wao Dodoma kwenye mchakato wao wa kutafuta makamu mwenyekiti wa chama.
Kwa mbwembwe za msururu wa magari mapya (vinyulaa) yaliowabeba wajumbe wa CCM wakiambatana na viongozi wazito wa chama hicho, tulijua kuna jambo kubwa linaenda kutokea Dodoma ambalo halijawahi kutokea.
Kwa masikitiko makubwa, kimetokea kihoja Dodoma; mbali na nafasi ya makamu kupatikana pasipo misingi ya demokrasia ya kugawa fursa za kuchaguana kwa wote, CCM wamekuja na mzee asiyeendana na nyakati za kileo na mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayotokea.
Nimepata huruma sana kwa wana CCM wengine ambao wao hawatoki kwenye familia za vigogo wala hawana ushawishi wowote kwenye chama; je hao watapewa lini fursa za kuonesha vipaji vyao vya uongozi kama bado kuna misingi ya demokrasia za majina ya mfukoni?
Au hawa wana CCM wengine wataishia kuwa wapagazi wa kuwabebea ma 'giants' wa CCM majembe na manyundo mpaka wanazeeka, huku wakisindikizwa na wapiga madebe akina Tlaatlaah ChoiceVariable na kamanda asiyechoka kububujika machozi Lucas Mwashambwa ?
Hii inahitaji tafakari sana, CCM msidhani kwamba kushangilia kwenu ukosefu wa misingi ya demokrasia nchini kunawanufaisha kwa chochote. Kwa misingi iliyopo ndani ya CCM wengi mtaishia kuwa wapagazi, wapambe na machawa mpaka mzeeke.
What a waste of life.