CCM wamejiaibisha kwa tukio hili. Kama Reginald Mengi alivyokuwa anasema sasa hivi kwamba ''watu wakitaka kumbambikia madawa ya kulevya mtoto wake,hiyo haiwezi kuitwa 'rushwa,hiyo ni zaidi ya rushwa'' Kwa wale wanaosoma Biblia unaweza kulifananisha na ile hadithi katika Biblia ambapo kashfa inatokea katika kabila la Benjamin,mwanamke mmoja anauawa kikatili,halafu watu wote wa Israel wanapelekeana habari wanaulizana maswala,kama unyama huo unaruhusiwa,mwisho wake,makabila yale yote mengine yanakwenda kupigana na kabila la Benjamin.
Sijasoma Biblia siku nyingi,in fact,miaka kumi na tatu sijasoma Biblia. Zamani nilikuwa nasoma sana Biblia,kwa sababu,among other things,nilikuwa sijaigundua CNN. [Hili swala la kutosoma Bibila kwa siku nyingi linaweza kuwa kesi dhidi yangu.]
Kwa kifupi,ninalosema ni kwamba this kind of incident is very serious,linaweza kuleta sympathy vote kwa Dr.Slaa,mtu ambaye,I had already written him off. Lakini CCM wakifanya namna hii,na watu wote Tanzania wakilijadili,haya ni mambo ambayo yanaweza kuiletea matatizo CCM.
Nilikuwa Butiama wakati ule wa Kampeni ya Ubunge,by election,baada ya kufariki Chacha Wangwe,na CCM walikuwa wanakuja kutua na Helicopter yao,halafu sijui ikatokea nini,nadhani wakatoa amri watu wakatwekatwe mapanga huko chini ili helikopta iweze kutua.
Halafu utaona huko Mara wapinzani wamekuwa very successful,jambo ambalo usingetegemea kutokea kwa sababu ule ndio Mkoa wa Mwalimu Nyerere. Inaonyesha wanaona ishara,wanapokuwa kule kwamba CCM hii ya leo haimwakilishi Mwalimu Nyerere.
Kwa sababu nimeona watu kadhaa walikuwa wanaulizwa maswali hapa na Mlimani TV kuhusu Uchaguzi,na wapo kina mama pale Kinondoni walikuwa wanasema CCM imeongoza Nchi kwa utulivu,na sasa pia inaongoza kwa utulivu;CCM ndio imetulea siku zote;CCM ni toka enzi za mababu,babu yangu aliichagua CCM,baba yangu aliichagua CCM, kwa hiyo na mimi pia nitaichagua CCM. Hayo ni maneno yenye mantiki. Lakini kwa nini watu wa Mara wanaikana CCM? Na huyo mgombea anayefanyiwa fujo hapo ni Vicent Nyerere,mtoto wa Josephata Nyerere,mdogo wake Mwalimu, ambaye anagombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema,ndipo zilipotokea hizo vurugu za watu kukatwa mapanga.
Haya mambo hayakubaliki. Inafanya mimi nifikirie kwamba yoyote akichaguliwa kuwa Rais ni sawa tu,kama ni Lipumba au Dr, Slaa,au Mziray au Kikwete. Siyo lazima Kikwete achaguliwe kuwa Rais. Hakuna maafa yatalifika Taifa kama Rais asipokuwa wa CCM.
Lakini hata kama nikienda a step further na kusema kwamba sitaki Kikwete achaguliwe kuwa Rais,sidhani kama Watanzania wanachagua Rais kwa kufuata kauli yangu. Lakin ndio hivyo,mimi napinga Kikwete kuchaguliwa Rais,kwa sababu sasa naona gloves zi