Ile operesheni inayoendeshwa na Green Guard wa CCM ya kukata mapanga wapinzani, sasa imeripotiwa kutekelezwa vyema huku Musoma Mjini. Katika tukio la hivi karibuni, vijana hao wanaolipwa ujira mdogo, na bangi nyingi, wamewacharanga wafuasi wa CHADEMA mapanga mjini huko, huku wawili kati yao wakiripotiwa kuwa mahututi.
Operesheni hiyo iliripotiwa tena kutekelezwa juzi huko Shinyanga. Pia iliwahi kutekelezwa maeneo mengine kama Njombe (ambapo watu wawili kwa uchache walifariki), Morogoro, Tarime na Moshi.
Bado haijawekwa wazi rasmi kuwa mratibu wa operesheni kata mapanga (OKAMA), taifa ni nani, ingawa inajulikana kuwa shughuli zake zinasimamiwa kwa karibu na wagombea wa Chama hicho katika Majimbo yao.
Mungu ibariki Tanzania.