CCM waeneza propaganda Dodoma kumtuhumu Warioba kuvuruga bunge leo jioni

CCM waeneza propaganda Dodoma kumtuhumu Warioba kuvuruga bunge leo jioni

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
3,295
Reaction score
2,501
Hapa dodoma baada ya Mzee Warioba kushindwa kuwasilisha rasimu ya katiba baada ya UKAWA kupinga ubabe wa Sitta kuvunja kanuni, sasa ccm imeanzisha propaganda kumtuhumu warioba.

Wabunge wa ccm wanadai warioba ameingia dili na UKAWA kuhakikisha kuwa rais anazundua jwanza bunge ndipo awasilishe rasimu kama kanuni zinavyosema kinyume na matakwa ya ccm na sitta kutaka warioba avunje kanuni kwa kuwasilisha rasimu kablq ya rais kuja.

Ccm sasa wanasema pamoja na kwamba kweli.warioba kuja leo ni kinyume cha kanuni lakini mzee huyo amewachochea wapinzani wavuruge mkutano wa leo.

Ni jambo lisiloingia akilini kumtuhumu mzee huyu.utadhani alijifungia chumbani kuandika rasimu peke yake wakati wote tunajua mchakato ulivyokuwa.

Hata hIvyo hakuna mbunge aliefurahia tukio la leo kama Job ndugai. Nimekutana nae hapa nje ya ukumbi akiwa na furaha isiyo kifani akisema hili ni fundisho kwa sitta na waliokuwa wakimbeza kila ilipokuwa ikitokea vurugu bungeni wakati akiongoza vikao bunge la jamhuri
 
Daah naona mwanzo mgumu kwa mzee wa Speed&$tandard bt tutaona mambo mengi sana anyway mzee WArioba najua ni jembe hana cha kupoteza wanafunz wa ukweli wa mwl jk nyerere
 
Ndugu yangu, mzee warioba amegeuka kuwa adui wa chama cha mapinduzi, maskini mungu amlinde mzee huyu mwema aliejivua mavazi ya ccm na kusimama upande wa wanyonge, kwani ni ukweli usio na kificho ccm hawataki uwepo wa katiba mpya. Mungu mlinde mzee wetu mzalendo warioba,
 
PRINCE CROWN mzee wa watu kweli anaonewa sana kwa ukweli wake na uzalendo wake kwa taifa
 
Last edited by a moderator:
Daah naona mwanzo mgumu kwa mzee wa Speed&$tandard bt tutaona mambo mengi sana anyway mzee WArioba najua ni jembe hana cha kupoteza wanafunz wa ukweli wa mwl jk nyerere
warioba amemsaliti kambarage nyerere.
 
Ndugu yangu, mzee warioba amegeuka kuwa adui wa chama cha mapinduzi, maskini mungu amlinde mzee huyu mwema aliejivua mavazi ya ccm na kusimama upande wa wanyonge, kwani ni ukweli usio na kificho ccm hawataki uwepo wa katiba mpya. Mungu mlinde mzee wetu mzalendo warioba,

Acha wehu,aliyekuambia muundo WA serikali tatu Ni utetezi na kusimama na wanyonge Ni nani?huu Ni uwendawazimu sikiliza na soma hitaji la wanyonge.

1.Elimu bora kwa Watanzania hasa maskini vijijini
2.Upatikanaji WA uhakika WA chakula na Madawa
3.Upatikanaji WA miundombinu ya Maji,umwagiliaji,barabara,Viwanda bei nzuri za mazao kama pamba,Korosho.
4.uwepo wa maeneo tengwa kwa wafugaji na wakulima
4.Uwepo wa vitanda na dawa zakutosha katika mahospitali
5.Uwepo wa uhakika wa ajira kwa kuongeza tija ya uzalishaji na kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani,

Hitaji la serikali tatu Ni,hitaji la kishetani.

hitaji la Umma Ni kuongeza ufaulu na kuwalipa vema walimu mishahara,

kujenga nyumba za waalimu na kuwapa mahitaji madaktari,

Serikali tatu Ni porojo za kishetani zinazolenga kulivuruga Taifa.
 
Generalize katika kujenga hoja inaakisi mapungufu yaliyoko ndani ya hoja na kutokana na mapungufu hayo, unatumia mbinu ya mwanvuli kujaribu kuyafunika.

Unapoleta hoja ukisema CCM wanaeneza propaganda, kwa mtu mwenye maono pevu atafahamu hoja yako iko based on institution na kila institution ina taratibu na sheria katika uendeshaji wake.

CCM ina wasemaji wake na katika wasemaji wake ndiyo tamko au sauti rasmi ya CCM linapotolewa, kinyume cha hivyo, kutumia neno CCM katika kubainisha individuals within CCM ni upofu wa fikra na kama siyo upofu wa fikra, basi unachokifanya ni mwendelezo wa propaganda za kilaghai.

Kama kuna watu wamemtuhumu Mzee Warioba wana uhuru wa kufanya hivyo hasa ikichukuliwa kuwa hayo ni mawazo ya individuals kama wabunge wa bunge la Katiba. Kwa mtazamo wako unataka kutuambia kuwa hakuna wanaCCM waliozomea bungeni au kupinga Rasimu ya pili ya Katiba kuwasilishwa kabla ya hotuba ya Rais Kikwete ya kulifungua Rasmi Bunge la Katiba. Kama wapo, unawaweka wapi katika hoja yako hii.

Wewe ndiyo unaeneza propaganda kutaka kutushawishi kuwa chama cha CCM kina tatizo na utendaji wa Mzee Warioba kama vile Rasimu ya Katiba iliandikwa na mjumbe mmoja.

Huu upotoshaji wenu hautawasaidia katika kupata kile mnachokitafuta kwa mlango wa nyuma.

Maamuzi ya kuridhia Katiba mpya yako mikononi mwa wananchi wengi.
 
sidhani km kuna nchi ilipata katiba mpya yenye faida kwa watu wake wote kwa urahisi km tunaotaka sie.huu ni mwanzo tutashuhudia mengi kati ya watetea wananchi na watawala nchi watetea maslai yao
 
Nimejisikia vibaya sana leo,inakuwaje watu kama wabunge kula njama ya kuwahujumu wananchi?
 
Acha wehu,aliyekuambia muundo WA serikali tatu Ni utetezi na kusimama na wanyonge Ni nani?huu Ni uwendawazimu sikiliza na soma hitaji la wanyonge.

1.Elimu bora kwa Watanzania hasa maskini vijijini
2.Upatikanaji WA uhakika WA chakula na Madawa
3.Upatikanaji WA miundombinu ya Maji,umwagiliaji,barabara,Viwanda bei nzuri za mazao kama pamba,Korosho.
4.uwepo wa maeneo tengwa kwa wafugaji na wakulima
4.Uwepo wa vitanda na dawa zakutosha katika mahospitali
5.Uwepo wa uhakika wa ajira kwa kuongeza tija ya uzalishaji na kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani,

Hitaji la serikali tatu Ni,hitaji la kishetani.

hitaji la Umma Ni kuongeza ufaulu na kuwalipa vema walimu mishahara,

kujenga nyumba za waalimu na kuwapa mahitaji madaktari,

Serikali tatu Ni porojo za kishetani zinazolenga kulivuruga Taifa.
Mbona mtoa mada uliyemjibu hajatamka sehemu yoyote serikali 3!!,mbona unakurupuka kujibu bila kusoma mkuu,kama ni serikali 3 ni tatizo kwako na una uchungu,kwanini isiwe moja ambayo gharama zitapungua kama ilivyo madai ya upande unaopinga!!,binafsi mimi serikali moja ndiyo sahihi,serikali 2 ni ulaghai tu.
 
Generalize katika kujenga hoja inaakisi mapungufu yaliyoko ndani ya hoja na kutokana na mapungufu hayo, unatumia mbinu ya mwanvuli kujaribu kuyafunika.

Unapoleta hoja ukisema CCM wanaeneza propaganda, kwa mtu mwenye maono pevu atafahamu hoja yako iko based on institution na kila institution ina taratibu na sheria katika uendeshaji wake.

CCM ina wasemaji wake na katika wasemaji wake ndiyo tamko la CCM linapotolewa, kinyume cha hivyo, kutumia neno CCM katika kubainisha individuals within CCM ni upofu wa fikra na kama siyo upofu wa fikra, basi unachokifanya ni mwendelezo wa propaganda za kilaghai.

Kama kuna watu wamemtuhumu Mzee Warioba wana uhuru wa kufanya hivyo hasa ikichukuliwa kuwa hayo ni mawazo ya individuals kama wabunge wa bunge la Katiba. Kwa mtazamo wako unataka kutuambia kuwa hakuna wanaCCM waliozomea bungeni au kupinga Rasimu ya pili ya Katiba kuwasilishwa kabla ya hotuba ya Rais Kikwete ya kulifungua Rasmi Bunge la Katiba. Kama wapo, unawaweka wapi katika hoja yako hii.

Wewe ndiyo uneeneza propaganda kutaka kutushawishi kuwa chama cha CCM kina tatizo na Mzee Warioba kama vile Rasimu ya Katiba iliandikwa na mjumbe mmoja.

Huu upotoshaji wenu hautawasaidia katika kupata kile mnachokitafuta kwa mlango wa nyuma.

Maamuzi ya kuridhia Katiba mpya yako mikononi mwa wananchi wengi.

CCM ni kila mwanaCCM.Usitake kupindisha hoja ya Mwana Mpotevu. Kuna wakati yabidi uongee katika utaifa kuliko kichama muda wote Mkuu MwanaDiwani
 
Last edited by a moderator:
MwanaDiwani mie siandiki kwa kutunga hata siku moja. Nipo hapa bungeni since day one na naandika kweli tupu bila kujali kama ukweli huu unakukera na kukuchukiza au lah
 
Last edited by a moderator:
kingukitano inaonyesha hata hujui katiba ni nini maana uliyotaja yote hayawezi kuwakwa kwenye katiba bala ni kwenye sheria na sera mbalimbali halafu eti unajiona na wewe mwana harakati, nenda shule kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Muungano lazima uwe na faida kwa pande zote zilizoungana sio changu chetu,chako chako.
 
Mkakati wa Magamba ni kuwa JK aje kumjibu Warioba , na kuwa Acha wabunge wa CCM wakipongeza hotuba yake na kujaribu kuisahaulisha ya msingi ambayo ni rasimu ya katiba , Olecsndeka leo alikuwa Msata akinadi Ridhiwani......kaongea kimasai kitupu ....sikumuelewa ...
 
Hebu niambieni wakubwa kwani ni kanuni gani iliyovunjwa na mwenyekiti wa bunge maalum?
 
CCM ilaaniwe kwa kwenda kinyume na Warioba aliyejitoa mhanga kuwakilisha maoni yetu wananchi kama yalivyo, bila kuyachakachua.
 
CCM nchi hii si ya kwenu peke yenu!! Rasimu ni maoni ya watanzania na si ya Jaji Warioba... Kwanza Tume ya Warioba si ya kwanza kupendekezo Serikali 3. Tume nyingi zilizoundwa zimependekeza Serikali tatu kwa sababu mfumo wa Serikali mbili umeshindwa kututatulia matatizo na isitoshe kero za Muungano zinazidi kuongezeka...

Cha kujiuliza ni kwanini CCM wanang'ang'a mfumo ambao umeshindwa kutuondolea kero?? Jibu ni moja tu, kulinda maslahi yao na watoto wao na si maslahi ya taifa...

Wanaosema eti Serikali tatu sio muhimu kwa wananchi, kilichomuhimu ni huduma kama elimu, maji, afya barabara nk hao ni vipofu na wahajui wanazungumza nn..

Bila kuwa na mfumo madhubiti wa kuongoza nchi hii kwa maana ya utawala... hizo huduma ni ndoto kuzipata. Mfumo wa utawala ndiyo Serikali.. Sasa huwezi ukapata huduma bora kama una mfumo mbovu wa kiutawa/Serikali...

Shikamoo WABUNGE kwa kukataa kuburuzwa na macc. Hiyo ndiyo iwe njia mahususi ya kukabiliana na njama za CCM!!
 
Back
Top Bottom