CCM waeneza propaganda Dodoma kumtuhumu Warioba kuvuruga bunge leo jioni

CCM waeneza propaganda Dodoma kumtuhumu Warioba kuvuruga bunge leo jioni

CCM ni kila mwanaCCM.Usitake kupindisha hoja ya Mwana Mpotevu. Kuna wakati yabidi uongee katika utaifa kuliko kichama muda wote Mkuu MwanaDiwani
Umejibu hoja yangu bila hata kuelewa mantiki ya hoja yangu pamoja na kuweka ufafanuzi ambao hata kijana wa darasa la tano anaweza kuuelewa vizuri.

Kama huwezi hata kuelewa tofauti ya CCM na mwanaCCM sioni uwezekano kama ninaweza hata kukuelewesha ukaelewa tofauti inayobainisha kauli ya wanaCCM na CCM.
 
CCM imekula kwenu, kila mtakachopanga kinyume na Katiba ya Wananchi, hakitafanikiwa!!!!!!!!!!!!!!!
 
Elungata who is Nyerere? A ghost? God? Or? Kuwa na upeo wako wa kufikiri sio mtu mwingine afikirie kwa niaba yako.

By the way, warioba alijifungia chumbani kuandika rasimu?
 
Last edited by a moderator:
Ukweli utajidhirisha tu, Mwisho wa propaganda uko karibu, hakika naamini Mungu yuko nyuma ya katiba bora ya watanzania, ndio maana haya yanatokea!
 
MwanaDiwani mie siandiki kwa kutunga hata siku moja. Nipo hapa bungeni since day one na naandika kweli tupu bila kujali kama ukweli huu unakukera na kukuchukiza au lah
Naomba uelewe kuwa "Kweli tupu" katika hoja za wabunge wa bunge la Katiba ni relative term.

Hiyo unayodhani ni kweli tupu ndani ya hoja wa wabunge inaweza isiwe kweli tupu katika uhalisia wake.

Kauli za wanaCCM haziwezi zikawa ni kweli tupu ya kauli ya CCM. Kauli ya CCM ndiyo kweli tupu ya maamuzi ya CCM.

Ninasema tena, hizi propaganda haziwezi kuondoa maamuzi ya wananchi wengi katika mstakabali wa Taifa lao.
 
CCM hawataki katiba ya wananchi wanataka wananchi waendelee kudumisha fikra zao.
 
Sijamsikia jembe ziyo kabwe hadi sasa kwny bunge hili
 
Comreed kanuni za bunge maalum la katiba kifungu cha 7(1)g kinamtaka rais aje kuzindua bunge na kifungu cha 7(1)h inamtaka warioba aje kulikabidhi bunge rasimu ya katiba tayari kwa mjadala baada ya rais kuzindua.

Kanuni hizi ndio sitta amepindisha kwa g kuipeleka h na h kuirudisha g kwa ubabe bila kuzingatia taratibu zinazotakiwa kufanya mabadiliko. Hope umeelewa now
 
Last edited by a moderator:
ni vigumu kuwaekewa wenye kutaka serikali 3,lakini ni vigumu zaidi kuwaelewa wenye kutaka serikali 2!wanaeleweka wenye kutaka serikali moja tena ya Tanganyika!Pambana Mtikila pambana!
 
Nashindwa kuelewa. Mnasema 6 alitaka kukiuka kanuni, na wajumbe wa Bunge maalum la Katiba walitaka kanuni za kuendesha Bunge Maalum la katiba walitaka kanuni zifuatwe, Je kuzomea ni kanuni ya ngapi ya Bunge maalum la Katiba? Je kila Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba atakapokiuka kanuni watazomea? Kanuni zinasemaje Mjumbe au kikundi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba anapokwenda kinyume cha kanuni?
Generalize katika kujenga hoja inaakisi mapungufu yaliyoko ndani ya hoja na kutokana na mapungufu hayo, unatumia mbinu ya mwanvuli kujaribu kuyafunika.

Unapoleta hoja ukisema CCM wanaeneza propaganda, kwa mtu mwenye maono pevu atafahamu hoja yako iko based on institution na kila institution ina taratibu na sheria katika uendeshaji wake.

CCM ina wasemaji wake na katika wasemaji wake ndiyo tamko au sauti rasmi ya CCM linapotolewa, kinyume cha hivyo, kutumia neno CCM katika kubainisha individuals within CCM ni upofu wa fikra na kama siyo upofu wa fikra, basi unachokifanya ni mwendelezo wa propaganda za kilaghai.

Kama kuna watu wamemtuhumu Mzee Warioba wana uhuru wa kufanya hivyo hasa ikichukuliwa kuwa hayo ni mawazo ya individuals kama wabunge wa bunge la Katiba. Kwa mtazamo wako unataka kutuambia kuwa hakuna wanaCCM waliozomea bungeni au kupinga Rasimu ya pili ya Katiba kuwasilishwa kabla ya hotuba ya Rais Kikwete ya kulifungua Rasmi Bunge la Katiba. Kama wapo, unawaweka wapi katika hoja yako hii.

Wewe ndiyo unaeneza propaganda kutaka kutushawishi kuwa chama cha CCM kina tatizo na utendaji wa Mzee Warioba kama vile Rasimu ya Katiba iliandikwa na mjumbe mmoja.

Huu upotoshaji wenu hautawasaidia katika kupata kile mnachokitafuta kwa mlango wa nyuma.

Maamuzi ya kuridhia Katiba mpya yako mikononi mwa wananchi wengi.
 
Hapa dodoma baada ya Mzee Warioba kushindwa kuwasilisha rasimu ya katiba baada ya UKAWA kupinga ubabe wa Sitta kuvunja kanuni, sasa ccm imeanzisha propaganda kumtuhumu warioba.

Wabunge wa ccm wanadai warioba ameingia dili na UKAWA kuhakikisha kuwa rais anazundua jwanza bunge ndipo awasilishe rasimu kama kanuni zinavyosema kinyume na matakwa ya ccm na sitta kutaka warioba avunje kanuni kwa kuwasilisha rasimu kablq ya rais kuja.

Ccm sasa wanasema pamoja na kwamba kweli.warioba kuja leo ni kinyume cha kanuni lakini mzee huyo amewachochea wapinzani wavuruge mkutano wa leo.

Ni jambo lisiloingia akilini kumtuhumu mzee huyu.utadhani alijifungia chumbani kuandika rasimu peke yake wakati wote tunajua mchakato ulivyokuwa.

Hata hIvyo hakuna mbunge aliefurahia tukio la leo kama Job ndugai. Nimekutana nae hapa nje ya ukumbi akiwa na furaha isiyo kifani akisema hili ni fundisho kwa sitta na waliokuwa wakimbeza kila ilipokuwa ikitokea vurugu bungeni wakati akiongoza vikao bunge la jamhuri

............CCM sio wote wanapenda kuburuzwa lakini wafanyeje? wanataka kushibisha matumbo yao... Ndugai lazima afurahie ............. maana Mh. 6 anajiona super .... ila wasihau kwamba kwa hali yoyote na dua za wa TZ kwa MUNGU wao ni kila uchwao .... iwe isiwe MUNGU lazima ataingilia kati na kuwaumbua wote wenye lengo baya kwa nchi hii... hasa wanaojisahau na kudhani watanzania wa leo ni wale wa miaka 47 iliyopita....

 
Kwa hiyo Job Ndugai leo ni mwendo wa :target::target::target::target::target::target::target::target::target::target::target::target::target:
 
Acha wehu,aliyekuambia muundo WA serikali tatu Ni utetezi na kusimama na wanyonge Ni nani?huu Ni uwendawazimu sikiliza na soma hitaji la wanyonge.

1.Elimu bora kwa Watanzania hasa maskini vijijini
2.Upatikanaji WA uhakika WA chakula na Madawa
3.Upatikanaji WA miundombinu ya Maji,umwagiliaji,barabara,Viwanda bei nzuri za mazao kama pamba,Korosho.
4.uwepo wa maeneo tengwa kwa wafugaji na wakulima
4.Uwepo wa vitanda na dawa zakutosha katika mahospitali
5.Uwepo wa uhakika wa ajira kwa kuongeza tija ya uzalishaji na kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani,

Hitaji la serikali tatu Ni,hitaji la kishetani.

hitaji la Umma Ni kuongeza ufaulu na kuwalipa vema walimu mishahara,

kujenga nyumba za waalimu na kuwapa mahitaji madaktari,

Serikali tatu Ni porojo za kishetani zinazolenga kulivuruga Taifa.

Hapo ndo kikomo cha uwezo wako wa kufikiri? Je, ni hayo tu?
 
CCM mtajuta, mnapokuwa mnaadimisha uhuru day ya Tanganyika mna maanisha nini ? Huwezi kumfanyia marehemu birthday.

Sasa marehemu anataka kufufuka, mnaogopa nini ?
 
Maadui wakubwa wa tanganyika ni ccm, wanataka muungano huu wa paka na sisimizi uendelee kwa maslahi ya watawala na sio wananchi! Hongera jaji warioba, Allah akulinde dhidi ya madhaalimu ya kiccm na mafisadi.
 
La!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Ndugai si ndiye aliyesema Hapatatosha mle ndani na kwamba watagawana mbao za mle ndani akajibiwa na muungwa mmoja kuwa mbao zile si zao wenyewe ni Watanzania walipa kodi ambao wapo nje haya hayakumuingia tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
msamehe tu kama mtu hafaham athar za serikal moja au mbili au tatu huyo si wa kumlaumu hata kidogo. mbaya ni kuwa anadhan anajua.
 
Back
Top Bottom