MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,266
Umejibu hoja yangu bila hata kuelewa mantiki ya hoja yangu pamoja na kuweka ufafanuzi ambao hata kijana wa darasa la tano anaweza kuuelewa vizuri.CCM ni kila mwanaCCM.Usitake kupindisha hoja ya Mwana Mpotevu. Kuna wakati yabidi uongee katika utaifa kuliko kichama muda wote Mkuu MwanaDiwani
Naomba uelewe kuwa "Kweli tupu" katika hoja za wabunge wa bunge la Katiba ni relative term.MwanaDiwani mie siandiki kwa kutunga hata siku moja. Nipo hapa bungeni since day one na naandika kweli tupu bila kujali kama ukweli huu unakukera na kukuchukiza au lah
Generalize katika kujenga hoja inaakisi mapungufu yaliyoko ndani ya hoja na kutokana na mapungufu hayo, unatumia mbinu ya mwanvuli kujaribu kuyafunika.
Unapoleta hoja ukisema CCM wanaeneza propaganda, kwa mtu mwenye maono pevu atafahamu hoja yako iko based on institution na kila institution ina taratibu na sheria katika uendeshaji wake.
CCM ina wasemaji wake na katika wasemaji wake ndiyo tamko au sauti rasmi ya CCM linapotolewa, kinyume cha hivyo, kutumia neno CCM katika kubainisha individuals within CCM ni upofu wa fikra na kama siyo upofu wa fikra, basi unachokifanya ni mwendelezo wa propaganda za kilaghai.
Kama kuna watu wamemtuhumu Mzee Warioba wana uhuru wa kufanya hivyo hasa ikichukuliwa kuwa hayo ni mawazo ya individuals kama wabunge wa bunge la Katiba. Kwa mtazamo wako unataka kutuambia kuwa hakuna wanaCCM waliozomea bungeni au kupinga Rasimu ya pili ya Katiba kuwasilishwa kabla ya hotuba ya Rais Kikwete ya kulifungua Rasmi Bunge la Katiba. Kama wapo, unawaweka wapi katika hoja yako hii.
Wewe ndiyo unaeneza propaganda kutaka kutushawishi kuwa chama cha CCM kina tatizo na utendaji wa Mzee Warioba kama vile Rasimu ya Katiba iliandikwa na mjumbe mmoja.
Huu upotoshaji wenu hautawasaidia katika kupata kile mnachokitafuta kwa mlango wa nyuma.
Maamuzi ya kuridhia Katiba mpya yako mikononi mwa wananchi wengi.
Hapa dodoma baada ya Mzee Warioba kushindwa kuwasilisha rasimu ya katiba baada ya UKAWA kupinga ubabe wa Sitta kuvunja kanuni, sasa ccm imeanzisha propaganda kumtuhumu warioba.
Wabunge wa ccm wanadai warioba ameingia dili na UKAWA kuhakikisha kuwa rais anazundua jwanza bunge ndipo awasilishe rasimu kama kanuni zinavyosema kinyume na matakwa ya ccm na sitta kutaka warioba avunje kanuni kwa kuwasilisha rasimu kablq ya rais kuja.
Ccm sasa wanasema pamoja na kwamba kweli.warioba kuja leo ni kinyume cha kanuni lakini mzee huyo amewachochea wapinzani wavuruge mkutano wa leo.
Ni jambo lisiloingia akilini kumtuhumu mzee huyu.utadhani alijifungia chumbani kuandika rasimu peke yake wakati wote tunajua mchakato ulivyokuwa.
Hata hIvyo hakuna mbunge aliefurahia tukio la leo kama Job ndugai. Nimekutana nae hapa nje ya ukumbi akiwa na furaha isiyo kifani akisema hili ni fundisho kwa sitta na waliokuwa wakimbeza kila ilipokuwa ikitokea vurugu bungeni wakati akiongoza vikao bunge la jamhuri
Acha wehu,aliyekuambia muundo WA serikali tatu Ni utetezi na kusimama na wanyonge Ni nani?huu Ni uwendawazimu sikiliza na soma hitaji la wanyonge.
1.Elimu bora kwa Watanzania hasa maskini vijijini
2.Upatikanaji WA uhakika WA chakula na Madawa
3.Upatikanaji WA miundombinu ya Maji,umwagiliaji,barabara,Viwanda bei nzuri za mazao kama pamba,Korosho.
4.uwepo wa maeneo tengwa kwa wafugaji na wakulima
4.Uwepo wa vitanda na dawa zakutosha katika mahospitali
5.Uwepo wa uhakika wa ajira kwa kuongeza tija ya uzalishaji na kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani,
Hitaji la serikali tatu Ni,hitaji la kishetani.
hitaji la Umma Ni kuongeza ufaulu na kuwalipa vema walimu mishahara,
kujenga nyumba za waalimu na kuwapa mahitaji madaktari,
Serikali tatu Ni porojo za kishetani zinazolenga kulivuruga Taifa.