CCM wafunzeni adabu vijana wenu kuwaheshimu wazee wetu

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Kitendo cha Kihongosi kumfokea Mzee Warioba kwa sababu tu katoa maoni tofauti na chama chake CCM si cha kiungwana kinatakiwa kukemewa na jamii nzima na wapenda haki wote.

Mzee hanuniwi mzee hafokewi hata kama kakosea kuna njia nzuri na sahihi za kumueleza.



Kiumri Kihongosi ni mjukuu wa Mzee Warioba, anatakiwa atambue bila hawa wazee kujitolea kulipigania taifa hili hiyo amani anayoililia na hicho cheo asingekipata.

Kuna wazee wangapi waliostaafu kila siku tunawaona kwenye matamasha ya kiserikali wakitoa maoni yao wengine hadi kuwaombea kazi serikalini wapenzi wao.

Kwa dhana ya Kihongosi, ni lini atamkemea Mzee Kikwete aache kuingilia utendaji kazi wa serikali ya Samia.
 
Halafu mtu kama Huyu anakuwa mbunge na waziri wa Habari na Utamaduni, utamaduni upi?!
 
Kwa dhana ya Kihongosi, ni lini atamkemea Kikwete aache kuingilia utendaji wa serikali ya Samia.
Hio jamaa imeanza kua haina akili ilipokua kule maporini kwenye fisi wengi ndipo ilipoonekana kumbe ina akili za fisi..
 
Ila kibongo Bongo hata mtaani ukimkosoa mtu ni lazima akuone adui wake, n kama vile Wabongo tuna laana.

Mbaya zaidi ukiwa na mamlaka afu ukakosolewa ndo hatari zaidi mana kuua sio kosa kwako, hata ukiua watu 1k kwa siku kama Manyonyo ni sawa tuu na kuna Wapumbavu watakuunga mkono.
 
Vijana wa CCM wanajikuta wao ndio top yaani kila mtu wanamuona kama sisimizi tu. Wanakera!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…