CCM wajumbe wengi wa NEC taifa ni watu wenye pesa na wamehonga kupata nafasi hizo, tutarajie nini huko mbeleni?

Nayasema haya si kwa kubahatisha,nimefanya uchunguzi karibu nchi nzima kujiridhisha,nafasi hizi zimejaa wengi wao matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao hawana kabisa ufahamu kabisa wa masuala ya siasa zaidi ya biashara,hii imepelekea wanaccm wafiia chama kushindwa kupenya.

Hii CCM ya sasa au inayoundwa na kina Kinana ni ya ubavu wa pesa,

Je bado wananchi waweke matumaini kwa hiki chama?,
Imani yangu NEC taifa ndio injini ya nchi sasa imejaa wafanyabiashara,hatutauzwa kweli?,nchi itabakia kuwa ya wachuuzi na si wazalishaji mali,
Hata mtawala atakayepatikana kupitia hii NEC taifa atakuwa influenced na hili tabaka la wafanyabiashara kupitiaha mambo yao.

Shime wananchi watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama vyetu,ikifika 2025 tuwakatae hawa wahuni kwa gharama yoyote ile
Wewe tulikuonya humu Mapema sana , Kwamba CCM ina wenyewe na kwamba wewe kidampa haumo , lakini ukabisha , ukaendelea na uchawa wako kwa Makonda , Haya kiko wapi sasa ?
 
Hawa watakisaidia sana chama, hatutaki viongozi masikini wa kutupwa, tunataka viongozi matajiri ambao watautumia utajiri wao kuimarisha chama na kusaidia kutatua changamoto za wananchi.

P
Unauhakika hao matajiri wanalengo la kuja kutatua changamoto za wananchi??au ndugu yangu njaa unajitoa akili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tugange yajayo wewe kapuku wa wafipa,acha uchuro
 
Unauhakika hao matajiri wanalengo la kuja kutatua changamoto za wananchi??au ndugu yangu njaa unajitoa akili.

#MaendeleoHayanaChama
Ulifuatilia vetting ya Mawaziri wa Kenya? Maskini wa lile baraza is worth more than 100m KShs ambayo ni roughly 2B TShs! Umaskini sio sifa ya kuwa kiongozi mzuri. Wanasema uongozi huanzia ndani ya familia, hauwezi kuinua maisha ya watu kabla hujanyanyua ya kwako
 
Hawa watakisaidia sana chama, hatutaki viongozi masikini wa kutupwa, tunataka viongozi matajiri ambao watautumia utajiri wao kuimarisha chama na kusaidia kutatua changamoto za wananchi.

P
Muulize km alifuatilia vetting ya Mawaziri wa Kenya? Maskini wa lile baraza is worth more than 100m KShs ambayo ni roughly 2B TShs! Umaskini sio sifa ya kuwa kiongozi mzuri. Wanasema uongozi huanzia ndani ya familia, hauwezi kuinua maisha ya watu kabla hujanyanyua ya kwako na familia yako! Tatizo la nchi hii ni kufikiri umaskini ni sifa njema au kiongozi mzuri ni yule anayejifanya maskini na kula mahindi ya kuchoma mbele ya watu
 
Ni makosa makubwa kuendelea kuitegemea CCM achilia mbali hao sijui wajumbe wa NEC.

Suluhu pekee itakayowaokoa watanzania na kuwaweka huru ni kuachana na CCM na kuifanya nchi mali ya Watanzania.
Lets suppose usemayo ni kweli, tukiieweka pembeni CCM, tuchague chama gani kushika nafasi badala ya CCM?.
P
 
Nayasema haya si kwa kubahatisha,nimefanya uchunguzi karibu nchi nzima kujiridhisha,nafasi hizi zimejaa wengi wao matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao hawana kabisa ufahamu kabisa wa masuala ya siasa zaidi ya biashara,hii imepelekea wanaccm wafiia chama kushindwa kupenya.

Hii CCM ya sasa au inayoundwa na kina Kinana ni ya ubavu wa pesa,

Je bado wananchi waweke matumaini kwa hiki chama?,
Imani yangu NEC taifa ndio injini ya nchi sasa imejaa wafanyabiashara,hatutauzwa kweli?,nchi itabakia kuwa ya wachuuzi na si wazalishaji mali,
Hata mtawala atakayepatikana kupitia hii NEC taifa atakuwa influenced na hili tabaka la wafanyabiashara kupitiaha mambo yao.

Shime wananchi watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama vyetu,ikifika 2025 tuwakatae hawa wahuni kwa gharama yoyote ile
Kama RA kasharudi, Karamagi kasharudi hapo tufunge mikanda watanzania !! tunaingia kwenye turbulance zone.
 
Lets suppose usemayo ni kweli, tukiieweka pembeni CCM, tuchague chama gani kushika nafasi badala ya CCM?.
P
Hatuchagui chama kwa sasa, kwa katiba hii kuchagua chama chochote cha siasa ni kupoteza muda, jukumu letu la kwanza kabisa ni kujenga mifumo inayofanya kazi kwa usahihi katika nchi yetu. Mifumo hii iainishwe vizuri mno kwenye Katiba yetu.

Baada ya jukumu hilo kukamilika hapo sasa hata kama ibakie CCM ama ije CDM, ACT ama CUF watanzania tutakuwa salama, mifumo sahihi iliyojegwa ndani ya Katiba yetu itatutetea.

Kwa sasa tupo mtu kati, hatuna pa kukimbilia.
 
Lets suppose usemayo ni kweli, tukiieweka pembeni CCM, tuchague chama gani kushika nafasi badala ya CCM?.
P

"kuachana na CCM na kuifanya nchi mali ta Watanzania"

Kwa sasa nchi ni mali ya CCM sio Watanzania, hata hivyo vyama unavyoviona ni mali ya CCM pia.

Ninaposema nchi kuwa mali ya watanzania, ni watanzania kukubaliana CCM haifai na kuingia barabarani kufanya mapinduzi ya amani, hasira hizi ndio zitawaweka mbali wahuni wote na CCM na mamlaka ya nchi hii.

wapo watanzania wengi mahiri ambao hawako kwenye siasa kwa sasa na mifumo iliyopo sio salama kwao kuwa kwenye siasa, ila kukisha kuwa na mifumo huru mamilioni watajitokeza kupambania nafasi mbalimbali, na vyama vya siasa vya ukweli vitaibuka maana hakutakuwa kuwa na vizuizi.

Mapinduzi ya wananchi yatatuweka kwenye kipindi cha mpito na nchi itakuwa chini ya wazee wenye heshima na hekima kutoka kila kona na nyanja ya nchi, kupitia baraza la muda utatengenezqa mfumo utakaohusisha wananchi wote kwenye kila nyanja.

Mwananchi yeyote kwasasa anaweza kuchochea muamko kwa wananchi na wananchi wa Tanzania kuidai nchi yao kupitia msukumo huo, unaweza kuwa hata wewe pascal Mayala.
 
Ulifuatilia vetting ya Mawaziri wa Kenya? Maskini wa lile baraza is worth more than 100m KShs ambayo ni roughly 2B TShs! Umaskini sio sifa ya kuwa kiongozi mzuri. Wanasema uongozi huanzia ndani ya familia, hauwezi kuinua maisha ya watu kabla hujanyanyua ya kwako
Nchi kama kenya kwa katiba yao na mwamko wa wananchi ni virahisi kuwa control hao matajiri...njoo kwetu shamba la bibi uone maumivu watakayoenda kuyapata watz.

#MaendeleoHayanaChama
 
"kuachana na CCM na kuifanya nchi mali ta Watanzania"

Ninaposema nchi kuwa mali ya watanzania, ni watanzania kukubaliana CCM haifai na kuingia barabarani kufanya mapinduzi ya amani, hasira hizi ndio zitawaweka mbali wahuni wote na CCM na mamlaka ya nchi hii.

Mwananchi yeyote kwasasa anaweza kuchochea muamko kwa wananchi na wananchi wa Tanzania kuidai nchi yao kupitia msukumo huo, unaweza kuwa hata wewe pascal Mayala.
Japo mawazo yako ni mazuri, ila unachozunguza hapa ni utopian politics kwa wishes and day dreams.

Siasa ni sayansi, inafuata scientific process za political science, kwa Tanzania hapo tulipo, tuna chama kimoja tuu cha siasa chenye uwezo wa kutawala nchi, chama hiki ni one and only CCM!, hakuna chama mbadala cha kuireplace CCM!. Hili la kufanya mapinduzi, ndicho Dr. Bashiru alichowashauri wakulima, Watanzania sio watu wa hivyo!. Hivyo CCM itaendelea kuwepo na kuendelea kutawala for a long long time to come mpaka atokee mbadala!.

Ukweli ni huu Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
P
 
Nayasema haya si kwa kubahatisha,nimefanya uchunguzi karibu nchi nzima kujiridhisha,nafasi hizi zimejaa wengi wao matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao hawana kabisa ufahamu kabisa wa masuala ya siasa zaidi ya biashara,hii imepelekea wanaccm wafiia chama kushindwa kupenya.

Hii CCM ya sasa au inayoundwa na kina Kinana ni ya ubavu wa pesa,

Je, bado wananchi waweke matumaini kwa hiki chama?,

Imani yangu NEC taifa ndio injini ya nchi sasa imejaa wafanyabiashara,hatutauzwa kweli?,nchi itabakia kuwa ya wachuuzi na si wazalishaji mali.

Hata mtawala atakayepatikana kupitia hii NEC taifa atakuwa influenced na hili tabaka la wafanyabiashara kupitiaha mambo yao.

Shime wananchi watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama vyetu,ikifika 2025 tuwakatae hawa wahuni kwa gharama yoyote ile
Sasahivi rushwa CCM ipo juu kupita maelezo
 
Lets suppose usemayo ni kweli, tukiieweka pembeni CCM, tuchague chama gani kushika nafasi badala ya CCM?.
P
Paskal,wapinzani wa kweli wapo ndani ya ccm kinachatakiwa kitokee ni hili dubwasha ccm kukatika vipande viwili,hapo ndio nchi itapona
 
Back
Top Bottom