Ila wapiga kelele maarufu wa CCM naona nao wamegoma kupumzika bado wapo humu wana randa randa.
Hii inaashiria hata na wao hawakubaliani na uongozi wa Serikali iliyopo na inayotaka kuingia ya CCM ndio maana kwenye ule uzi wa michango kwa ajili ya Maxence nao wamechangia
Nimeona mpaka yule kada wao maarufu LM kachangia buku 5.
Ogopa sana mtu aliyekosa mshipa wa aibu! Na usikute mpaka wale walio ifungua na wenyewe wapo. Ila cha kushukuru kwa sasa zile mada zao za kipuuzi zimepungua.
Niwaombe wasimamizi wa jamii forums, kutozipa kabisa nafasi mada za kumsifia mgombea wao, na ambaye ndiye chanzo kikuu cha kufungiwa kwa huu mtandao. Ikiwezekana wazifutilie mbali huko. Kamwe wasikubali kuwa wanafiki.