CCM wameamua kutafuta kura kwa nguvu, yaani nchi nzima imepata zero 68 pekee?

Sio poa, ziro 68 kwa zamani ilikuwa ni ziro ya shule mbili kubwa pekee lakini sasa hivi ni nchi nzima. Yaani kupata ziro unakuwa celebrity, maana mko wachache sana.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dr. Said Mohammed ametangaza matokeo ya kidago cha sita leo July 07,2025 Visiwani Zanzibar ambapo kati Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 125,779 sawa na 99.95% ya Watahiniwa wenye matokeo.

Dr. Said amesema “Watahiniwa walioshindwa mtihani ni 68 sawa na 0.05%, mwaka 2024 Watahiniwa 103,252 sawa na 99.92% ya Watahiniwa wa Shule walifaulu, hivyo ufaulu wa Watahiniwa wa Shule umeongezeka kwa 0.03% ikilinganishwa na mwaka 2024”
#MillardAyoUPDATES
Mitano tena ,zero kutakuwa hakuna kabisa mpaka 2030....OCTOBER TUNATIKI.
 
Hahaha hao siku wakimaliza vyuo vikuu hawaajiriki tutaanza kupanua magoli kwenye usahili.

Hamna shida ikiwa wao wenyewe ndio wako madarakani.
 
Waliingiza siasa kwenye elimu toka Magufuli alipoingia madarakani,eti big results now, wanazidi kudidimiza na kuzika elimu yetu, mtu anamaliza chuo lakini hana tofauti na form 4 wa zamani,
 
tukifeli shida tukifauli shida. binadamu sijui anataka nini . Form six 99% ni watu wanaojitambua na wanasoma masomo makuu matatu, usifauli kwel? ndio maana mungu akaamua akae mbali, mvua ikinyesha shida, jua likiwaka shida
 
Sio poa, ziro 68 kwa zamani ilikuwa ni ziro ya shule mbili kubwa pekee lakini sasa hivi ni nchi nzima. Yaani kupata ziro unakuwa celebrity, maana mko wachache sana.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dr. Said Mohammed ametangaza matokeo ya kidago cha sita leo July 07,2025 Visiwani Zanzibar ambapo kati Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 125,779 sawa na 99.95% ya Watahiniwa wenye matokeo.

Dr. Said amesema “Watahiniwa walioshindwa mtihani ni 68 sawa na 0.05%, mwaka 2024 Watahiniwa 103,252 sawa na 99.92% ya Watahiniwa wa Shule walifaulu, hivyo ufaulu wa Watahiniwa wa Shule umeongezeka kwa 0.03% ikilinganishwa na mwaka 2024”
#MillardAyoUPDATES
Elimu ya sasa ukifeli maanayake wewe hujui hata kusoma na kuandika
 
Back
Top Bottom