Elections 2010 CCM wametumia shilingi ngapi kwenye huu uchaguzi?

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
54,762
Reaction score
59,204
Wandugu hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza kila siku,hawa wenzetu wa chama cha nambari wani wametumia/watakuwa wametumia shilingi ngapi kwenye huu uchaguzi hadi uishe? na hizi hela wametoa wapi hata na kama wamekopa watatoa wapi hela ya kulipa?kwanza tukianzia na nguo inaonekana kabisa ccm wananguo ambazo wakizigawa tunaweza kuvaa wananchi wote wa TANZANIA kuanzia na mikofia yao na mitshirt tukija kwenye matangazo ya kwenye tv na mabango kwanza mabango ni bei kubwa sana tu kwa mwezi mmoja .jamani ukifkiria tu kwa hali ya kawaida utakuta ni mabilioni ya hela yametumika.tukija kwenye maisha ya mwananchi wa kawaida nadhani wenyewe majibu mmnayo.swali wametoa wapi hizi hela zote na kama wamekopa watalipaje??
 
hizi ni baadhi ya picha za mikutano yao
 

Attachments

  • z12.jpg
    74.9 KB · Views: 42
  • z2.jpg
    67.6 KB · Views: 47
Katu hawatakuambia! Dola milioni mbili kwa mabago yaliyotengenezwa Canada. Bado hujaweka hela ya t shirts na kanga. Pia kule Arusha kila taxi iliyokuwa inapeperusha bendera ya CCM ilipewa shilingi elfu kumi za petroli, kuna malipo ya watumbuizaji, kuna safari za mama Kikwete na ndege ya serikali, kuna safari za Ridhwani na magari ya serikali/chama. Na hii ni just the tip of an iceberg. Hawatakwambia! Pia labda ungeuliza CCM imekusanya fedha kiasi gani kutoka kwa makampuni ya madini, wafanyibiashara maarufu, nchi za nje zinazopendelea kuona CCM ikiendelea kutumikia maslahi yao, na kadhalika na kadhalika.
 
Wanachota hazina tu! Kama wanataka bilioni 20 wanaenda hazina kuchukua. Kuna thread hapa ilikuwa inasema shughuli nyingi za Serikali zimesimama. Hili linasababishwa na pesa yote kuchukuliwa na CCM ili kuhakikisha "ushindi wa kishindo"
 
Hata nchi zilizoendelea katika europe hawa dhubutu kutumia kiwango ccm inachotumia.sisi ambao hospitali hazina vifaa,shule vijiji hauwezi kujua kama ni boma la mbuzi au shule ndio chama chetu kina kiburi cha kutumia si chini ya bilioni 50.

Conservative party uk hawa wezi kuchanga pesa ccm waliochanga kwa muda mfupi ingawa kuna members wengi ambao ni matajiri wakubwa.Mittal ambaye ni tajiri mkubwa alitoaga milioni 5 kwa Labour party mpaka leo imekuwa historia.Tanzania ni nchi yenye uchumi mdogo nina weza kusema pia matajiri wake ni wakaida,cha kujiuliza wanapata wapi hizo pesa za kuweza kuchangia bilioni 50 kwa miezi miwili au kwao biashara unatoa shilingi kupata shilingi tano.
 
Mwizi ni mwizi tu, hatakama huwezi kumficha hata siku moja maana keshazoea. Tunahongwa kwa khanga, vikofia na T-shirt lakini hatutaki kuuliza zimetoka wapi? Nani kachangia hizo pesa za kununulia? kwa nini wasichangia pia kujenga Vyuo Vikuu kila mkoa? Au hata pale UDSM wanafunzi wanalala wamebebana kila siku aka mzungu wa nne utadhani wako gerezani matokeo yake tunaona vijana wetu wanaanza kugawa maumbile yasiyo rasmi kwa wazungu migodini.

CCM waende zao huko, tunahitaji mabadiliko hata kwa kumwaga damu. hawa jamaa walionje joto la kuwa kando ya utawala watajifunza.
 
walitenga bajeti ya bilioni 40 (soma tena, bilioni with b). Kadri siku zinavyoenda, inaonekana watatumia zaidi ya bilioni 90.
 
Hili nadhani tuwaachie wanachama wa CCM, hela zao sisi zinatuhusu nini?
 
Hili nadhani tuwaachie wanachama wa CCM, hela zao sisi zinatuhusu nini?
Kasheshe,
Shida si kwamba hela ni zao. Hela hizo wametuibia. Umesahau mambo ya EPA, Meremeta etc?
 

Nyani ulishawahi kutuma neno shinda mkoko sijui kwenda namba ngapi ngapi! Ukakatwa Tshs. 550/=
 
Hili nadhani tuwaachie wanachama wa CCM, hela zao sisi zinatuhusu nini?

Kasheshe una hakika ni za CCM tu? Kumbuka 2005 EPA (KAGODA) sasa ngoja uje upate ukweli wa hizi.
 
Wewe unauliza nini,hizi ni fedha za kifisadi na huu ni utawala wa kiimla?nini cha ajabu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…