Uchaguzi 2020 CCM wana maana gani kuandika Fomu zao za Urais ni za kuwania Uongozi katika Vyombo vya Dola?

Hivi ccm kwanini mnakuwa wapumbvu kiasi hiki.
Unakwazika na nini hapo?
Ukiwa rais ni tayari kiongozi wa dola
Mnaipaisha tu ccm bila ya kujijua kwa kuitaja taja.tuonesheni basi makabrasha yenu yameandikwaje?
 
Kwani hizi fom kila chama kinachapisha ya kwake!? Tutoane tongotongo hapa

Mimi fikira zangu nilidhani kwasababu anatafutwa Rais wa nchi bila kujali atakuwa wa chama gani hivyo na form inakuwa ya aina moja kwa vyama vyote
Aheee nadhani utatusaidia na wengine katika hili
 
Hebu jisome upya halafu uniambie kama umejielewa
Hapo nimefupisha kilichopo kwenye katiba ya CCM na ndio katiba pekee ya chama Cha siasa ambayo haijatiliwa shaka vipengele vyake mpaka sasa, kwa kukusaisldia tu itafute uisome
 
Rais ni Amiri jeshi au hamjui maana yake.

Rais anakuwa amili Jeshi baada ya kuchaguliwa Kuwa rais na Rais anachaguliwa na wanainchi na siyo Vyombo vya dola!au safarii majeshi yetu ndiyo yatakayo piga kula peke yake[emoji15]
 
Hili suala nimeliona jana, nikadhani kama ni mzaa.

Embu angalieni hii picha wandugu.. " Kugombea nafasi ya uongozi katika vyombo vya Dola maana yake nini"

Mi nahisi hapa kuna mkono wa Mungu umepita, inawezekana kuna makosa kwenye kuandika hayo maneno.

Lakini kwenye makosa hayo ya kiuandishi, Mungu ameamua kujifunua kwa watanzania kwamba Magufuli na CCM ni watu wa namna gani, na Mungu ametufunulia ya kwamba CCM bila Dola haipo.

Ccm ipo madarakani kwa nguvu ya dola na sio nguvu ya wananchi. Mungu anazidi kujionesha. Ccm wakumbuke Ulimwengu wa kiMungu haujalala, na endapo wananchi tukishindwa kuleta haki Mungu atajionesha.
 
Uwongo huo wame edit

Usiwe na akili ndogo uwe unatafuta ukweli
 
WAPO SAHIHI.

MAGUFULI NI RAIS WA VYOMBO VYA DOLA.

BILA VYOMBO VYA DOLA MAGUFULI HAWEZI KUSHINDA URAIS TANZANIA.

KILA MTU ANALIJUA HILO. POLISI NA TISS WAKIKAA PEMBENI CCM HATUSHINDI UCHAGUZI WOWOTE TANZANIA.

TUMECHOKWAAA, SASA NI UBABE TU NA PROPAGANDA NDIO ZINAENDESHA NCHI.
 
Kuna tofauti fulani naiona kwenye bag lenye form ya kuomba ridhaa ya kuingia ikuru kupitia CCM.

Ya 2015 inasomeka "form za CCM za kuomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"

Ya 2020 inasomeka "form ya maombi ya kugombea uongozi katika vyombo vya dola "

Hii ya kuomba kugombea uongozi katika vyombo vya dola imekaaje wadau. Kwangu naona inaleta ukakasi kidogo.

Sisi wananchi ndio huamua kwa kupiga kura kumchagua raisi, wabunge na madiwani.

Hii ya kuomba kuongoza vyombo vya dola?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…