CCM wanafikiri kura walizopata 2020 ni mali ya kudumu

CCM wanafikiri kura walizopata 2020 ni mali ya kudumu

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Nimemsikia Membe akizungumza kwa kujiamini kama ilivyokua kawaida yake. Mimi namshangaa ni msomi wa aina gani asiyeweza kutathmini mambo kisayansi hata kidogo.

Yeye ni mwanasiasa asiyekua na mvuto wowote zaidi ya kujiamini bure. Tatizo lingine kubwa la Membe kwenye siasa sio mtu mwadilifu. Ni mtu fisadi na mbadhirifu ndio kisa kikubwa kumchukia magufuli.

Kama Samia anafuata ushauri wa wanasiass wa pwani kama kina membe, nape na januari makamba wenye kumchukia magufuli kwa kua wao wanatumiwa na wafanyabiashara fisadi na watumishi wapenda rushwa kwa hakika ccm 2025 itaangukia pua.

Ccm wanafurahia ushindi mkubwa wa 2020 huku wakisahau kwa haraka kama sio magufuli wabunge walio wengi wa ccm wasingekua bungeni. Mbunge lusinde kibabaji amekua anawaonya ccm kulitambua hilo ila wengi wanafikiri tofauti.

Bila uongozi wa asili ya ccm kuwajali wanyonge kwenye jamii na kuendesha nchi kwa maslahi ya umma ccm ndio itabidi kuwa ya kidikteta kweli maana hawataweza kushinda uchaguzi kihalali. CHADEMA wameaminisha wafuasi wao eti walibiwa kura en masse 2020. Hapana... CCM ilishinda en masse kutokana na uongozi wa Magufuli.

Licha ya samia kufuata mstari wa hao 'gang of four wa tz' juzi ilibidi kukiri makubwa ya mafanikio ya jpm kwenye miundombinu na akakiri zawadi hiyo ingebidi iwe ya JPM.

Watanzania wana kumbukumbu kuliko hao genge la kina nape wanavyofikiri. 2025 bila shaka watatoa hukumu sahihi kwa usaliti wa samia na genge lake.
 
2020 hakukuwa na UCHAGUZI bali U HAFUZI hata CCM wanalijua wanajitoa Ufahamu pamoja na MAGUFULI kuweka MABANGO ya CHAGUA MAGUFULI NZIMA bado MAGUFULI na Vyombo Vyake WALIUNAJISI Uchaguzi na MUNGU HAKUPENDEZWA KABISA NA KITENDO HICHO

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
2020 kulikuwa hakuna uchaguzi, ni ubakaji, yule dikteta aliogopa sana uchaguzi ndio maana alizima mitandao kwa miezi 3 kuficha uovu wake
 
Mungu ni mkubwa sana. Maajenti wa sheatani wanajifanya eti hawajui kilichotokea 28 Oktoba 2020. Eti wanaita uchaguzi...
 
Mungu ni mkubwa sana. Maajenti wa sheatani wanajifanya eti hawajui kilichotokea 28 Oktoba 2020. Eti wanaita uchaguzi...
Hata huko nyuma mbona hamna rekodi ya upinzani kushinda kwa viti bungeni? .. kila siku eti wameibiwa kura. Mbona tusione basi hata rufaa moja kwa uchaguzi 2020 kama wizi ulikua wa kiwango hicho?
 
Okay, Shetani. ulishinda uchafuzi. Mungu kaamua ugomvi. Kwa nini tuendelee kuzozana?
Hata huko nyuma mbona hamna rekodi ya upinzani kushinda kwa viti bungeni? .. kila siku eti wameibiwa kura. Mbona tusione basi hata rufaa moja kwa uchaguzi 2020 kama wizi ulikua wa kiwango hicho?
 
Tatizo ni kwa sababu chama kimetekwa tena na walewale waliokuwa wamekizamisha kuelekea kifo kabla ya JPM kukiokoa 2015.

Muda ni mchache na mambo yanaenda kwa kasi sana.

Kinahitajika chama kipya mbadala wa CCM na tofauti na hawa wapinzani tumbo politics wa sasa.

Muda utaongea soon!
 
Okay, Shetani. ulishinda uchafuzi. Mungu kaamua ugomvi. Kwa nini tuendelee kuzozana?
Kwani kufa magufuli ndio mtashinda uchaguzi? Nyie ni wa kushindwa tu. Lawama mtupieni baba wa taifa mwalimu nyerere. Yeye alipanda mbegu kwa watanzania kutambua wadhalimu na vibaraka wa ubeberu. Watanzania wanajua nani anaweza kuwaongoza na nani ni dalali wa kuwapiga mnada.
 
🙌
Kwani kufa magufuli ndio mtashinda uchaguzi? Nyie ni wa kushindwa tu. Lawama mtupieni baba wa taifa mwalimu nyerere. Yeye alipanda mbegu kwa watanzania kutambua wadhalimu na vibaraka wa ubeberu. Watanzania wanajua nani anaweza kuwaongoza na nani ni dalali wa kuwapiga mnada.

🙌
 
Tatizo ni kwa sababu chama kimetekwa tena na walewale waliokuwa wamekizamisha kuelekea kifo kabla ya JPM kukiokoa 2015.

Muda ni mchache na mambo yanaenda kwa kasi sana.

Kinahitajika chama kipya mbadala wa CCM na tofauti na hawa wapinzani tumbo politics wa sasa.

Muda utaongea soon!
Kikitokea Chama kipya chenye watu wanaojielewa mbona CCM watafurahi wenyewe.. Sio hawa wachumia tumbo wanaojiita wapinzani.. Watu wamechoka.. Mustakabali wa maisha haueleweki.. Wao wamekazana na matozo yao tu.. Halafu kesho watakuja kuomba tuwachague tena, kisha litatokea bwege moja litahamasisha watu wasiende kupiga kura..
.
 
Back
Top Bottom