CCM wanajuta kuingia kwenye mchakato wa katiba mpya?

mcfm40

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,452
Reaction score
3,151
Sarakasi walizofanya kwenye mabaraza na lawama na matusi yanayoelelezwa kwa Warioba kana kwamba yeye ndiye anayeamua nini kiwepo na nini kisiwepo katika katiba mpya ni mbinu za CCM kumtisha?

Kwani Tume ni warioba peke yake. CCM kemeeni hawa makada wenu la sivyo naiona tume ikijiuzulu na mchakato mzima kuvurugika.

Na huo ndo utakuwa mwanzo wa kuiingiza nchi ktk machafuko makubwa. Kikwete be careful!
 
Suala la kupata katiba mpya ni ajenda ya kikwete na wapinzani, na sio maccm, ndo maana wanampiga vita kikwete kwa kuingiza washauri wa ovyo kwenye suala hili ili wavuruge mchakato mzima wa kupata katiba mpya!!
 
Kichwa cha habari: CCM wanajuta kuingia kwenye mchakato. Habari yenyewe: CCM kemeeni makada wenu la sivyo Tume itajiuzulu. Kama mleta mada siyo mburula a.k.a kilaza a.k.a mbumbumbu a.k.a pimbimaji atakuwa nini sasa?
 
Wameiona nguvu ya umma ilivyo,wametetemeka. Walidhani kwa kukaririsha maonii yao ya nec wanachama wao itawaokoa.
 
Sarakasi walizofanya kwenye mabaraza na lawama na matusi yanayoelelezwa kwa Warioba kana kwamba yeye ndiye anayeamua nini kiwepo na nini kisiwepo katika katiba mpya ni mbinu za ccm kumtisha? Kwani Tume ni warioba peke yake. Ccm kemeeni hawa makada wenu la sivyo naiona tume ikijiuzulu na mchakato mzima kuvurugika. Na huo ndo utakuwa mwanzo wa kuiingiza nchi ktk machafuko makubwa. Kikwete be careful!

wazo zuri! ila samahani nataka kukuuliza' machafuko yapi! navipi yanaweza tukokeaje nini chanzo labda! naomba unielekeze!
 
Suala la kupata katiba mpya ni ajenda ya kikwete na wapinzani, na sio maccm, ndo maana wanampiga vita kikwete kwa kuingiza washauri wa ovyo kwenye suala hili ili wavuruge mchakato mzima wa kupata katiba mpya!!

Hahahahaaa, msijidanganye. yaani mnataka katiba mpya ikipatikana wapinzani mjinasibu kuwa ndo mmefanikisha kumbe wakati wa majadiliano ya muswada wa marekebisho ya katiba mpya wapinzani mburulaz walitoka nje ya ukumbi wa bunge na ccm pekee ndo imejadili na kupitisha kwa kushirikiana na wabunge wa upinzani wanaojitambua kama akina shibuda, cheyo na mrema
 
Kichwa cha habari: CCM wanajuta kuingia kwenye mchakato. Habari yenyewe: CCM kemeeni makada wenu la sivyo Tume itajiuzulu. Kama mleta mada siyo mburula a.k.a kilaza a.k.a mbumbumbu a.k.a pimbimaji atakuwa nini sasa?

atakua kama ulivyo wewe!
 
Tena nawasihi warioba na tume yake wasitishwe wala wasirudi nyuma. Tunatengeneza katika ya watanzania sio ya ccm, na tume wanaanda katika kwa mujibu wa maoni ya watanzania walio wengi kuliko hao maccm.
 
Wameiona nguvu ya umma ilivyo,wametetemeka. Walidhani kwa kukaririsha maonii yao ya nec wanachama wao itawaokoa.

Nguvu ya umma unayosema ni ipi? au ni ile ambayo imesababisha viongozi wenu vihiyo waungane? kwa kuwa ccm ndo ina wabunge wengi, ni wazi kuwa ndiyo inayowawakilisha wananchi wengi na kwa hali hiyo nguvu ya umma ipo ccm
 
Tena nawasihi warioba na tume yake wasitishwe wala wasirudi nyuma. Tunatengeneza katika ya watanzania sio ya ccm, na tume wanaanda katika kwa mujibu wa maoni ya watanzania walio wengi kuliko hao maccm.

Mkuuu, kwani Tume ina kazi gani kubwa imebaki katika mchakato ufuatao; Bunge la Katiba, Kura za Maoni na Kusainiwa?
 
maoni yaliotolewa na wananchi ndio yako kwenye mchakato wa katiba amabayo nyie maccm mnalalamikia. Tumesema kuhusu serikali tatu ambazo nyie hamtaki japo waliosema ni watanzania, mnataka tume iandike maoni ya ccm,iache ya watanzania walio wengi.
Kuhusu nguvu ya umma.ccm haijawahi kuwa na nguvu ya umma,siku zote ccm inaamini katika nguvu za mafisadi,wauza sembe na walanguzi wa mali za umma. Ccm haijawahi kutambua umma katika historia yake. Wabunge wake wengi waki kwa maslahi binafsi na chama chao huku nchi wakiiweka mbali kabisa.nguvu gani ya umma ndani ya ccm inayosafirisha tembo na twiga hai kila siku kwa ujangili???
 
Mleta hoja kavurugwa hana anachojua hizo vurugu anazoongea mbona wengine hatuzioni ficha umbulula wako.
 
Sarakasi walizofanya kwenye mabaraza na lawama na matusi yanayoelelezwa kwa Warioba kana kwamba yeye ndiye anayeamua nini kiwepo na nini kisiwepo katika katiba mpya ni mbinu za ccm kumtisha? Kwani Tume ni warioba peke yake. Ccm kemeeni hawa makada wenu la sivyo naiona tume ikijiuzulu na mchakato mzima kuvurugika. Na huo ndo utakuwa mwanzo wa kuiingiza nchi ktk machafuko makubwa. Kikwete be careful!
Mkuu siyo bure umerogwa umeandika pumba hasa hoja zingine sijui huwa mnazitoa wapi.
 
Swali kwa Mh.Simiyu, Hivi ni kweli toka moyoni kuwa CCM walikuwa na nia ya dhati kupata katiba mpya au kukarabati ile ya zamani??
 
Nguvu ya umma unayosema ni ipi? au ni ile ambayo imesababisha viongozi wenu vihiyo waungane? kwa kuwa ccm ndo ina wabunge wengi, ni wazi kuwa ndiyo inayowawakilisha wananchi wengi na kwa hali hiyo nguvu ya umma ipo ccm

Kwani nini mnachakachua sasa?
 
Back
Top Bottom