Uchaguzi 2020 CCM wanakosea wapi?

Uchaguzi 2020 CCM wanakosea wapi?

edwardbm

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2016
Posts
292
Reaction score
252
Kwa kipindi ambacho nimekifahamu Chama cha Mapinduzi kwa chaguzi zilizopita. Kimekua kikifanya vizuri kwenye kufanya Kampeni za Uchaguzi.

Sisemi kwamba mbinu zote walizotumia zilikua ni sahihi za haki na za usawa"fair". La hasha. Ila nyingi ya mbinu walizotumia, mfumo wao wa Kampeni na njia zao za propaganda na namna walizotumia kutafuta kuungwa mkono zilikua zikionyesha kuungwa mkono toka kwenye mbio za Kampeni, kabla hata ya kwenda kwenye Kura.

Hata jamii za kimataifa hazikutilia shaka sana mchakato wa Kampeni Hadi Uchaguzi. Tofauti na zama hii.

Jambo moja na kumbuka hata wimbo walioutumia kwenye Kampeni za mwisho 2015. Ulibamba balaa. Hata kwa mtu aliye kua ni Chadema, wapinzani wa kuu, au wengi ambao hawakua na mapenzi na Chama walikua wakiuimba maana ulikua umepangika vizuri kimrindimo na mdundo.

Mwaka huu sijui hawaja tunga.

Mwaka huu Mengi hayajakaa kwa kuhamasisha. Zaidi ni Ile mbinu ya kuandaa usafiri na kufanikiwa kukusanya watu au kuleta wananchi kwenye Kampeni. Nyingine zoote sijaona zikifanikiwa kuhamasisha umati mkubwa au wananchi.

Zama hii kwa mtazamo wangu ni kama wame(na) tumia gharama kubwa kwa mbinu ambazo sioni Kama Ni "effective" na zinaweza kumuachia mtu hamasa ya kupiga Kura CCM, mfano wanatumia wasanii wengi kwenye kila tukio la Kampeni hasa za Uraisi. Ila sidhani hata Hawa wasanii woote wameweza kuufikia ule wimbo wa CCM ni ileileee wa 2015.

Mbaya zaidi vitu vinavyo tafsiriwa na upinzani kama conspiracy zinazofanya na Taasisi za umma(serikali) mbalimbali ambazo kimtanzamo Ni Kama kwa lengo la kumharibia mipango ya kampeni Mpinzani wao mkuu Lisu , badala yake zinaonekana kumpaisha.

Jambo la mwisho ni hili ambalo la karbuni la kwenye Kampeni hizi, Ni hii ya kuona kutafuta support ya Viongozi wa dini, namely Viongozi wa dini ya Uisilamu, (naomba kwenye hii nieleweke, wametafuta support ya VIONGOZI) nadhani lengo ni kuamini kwa kupata kuungwa mkono na Viongozi wa dini ya kiisilam Basi watapata Kura za waumini wa kiislam hata Kama sio zote, walau nyingi, ili kwenda kuongeza hesabu.

Cha ajabu hata move hii imepata Upinzani kwa watu ambao naamini ni waumini wa Uislam wenyewe ama viongozi wenza wa Uislam.

Mfano ni tukio la kiongozi wa BAKWATA Dar kuweka wakati wa Dua ya kuombea Kampeni ya Chama. Inaonekana baadhi ya waamini na baadhi ya Viongozi kutofurahishwa na hilo. Hivyo badala ya kuongeza mtaji wa kura nalo ni kama limeharibu.

Swali moja najiuliza na nimekua nikijiuliza. Hivi hujuma ya kujificha inayofanywa na hizi Taasisi dhidhi ya kampeni za Chama, yaani Taasisi au watu husika wana-design tukio la kusupport Upande wa CHADEMA ironically. Hivyo kuihujumu CCM.

Au ni nafsi na akili zinawasaliti hawa wanaotaka kui-support CCM Kwa kuandaa Mambo ambayo ni Kama figisu dhidi ya Upinzani, kwasababu akili inakua hawaamini kile ambacho wanasupport, hivyo wanafanya honest mistakes na blunders kwenye harakati zao. Kwa kutofanya matukio ya kimahesabu kufanikisha azma zao (calculated moves)

Ama ni Upinzani tu, especially CHADEMA. Wanafanya Mambo yao kwa mahesabu makali kuwazidi CCM, kwa kutake advantage ya kila hila inayofanywa dhidi yao na kuifanya iwe na manufaa kwao,( Jambo ambalo naamini ndivyo ilivyo)

Ama CCM msimu huu inagundu? Kama anavyosema Mshana Jr.😃😃

Nnavyofikiria CCM ni chama kikubwa na kikongwe, kwa Tz na Africa. Siasa ni figisu, propaganda, kuchafuana, etc. Sio kwa maneno tu hata kwa vitendo ambavyo vitafanya mwingine aonekane mbaya. Alimradi visivuke mipaka kufikia kuumiza watu physically au kugharimu Uhai.

Mwenyekiti wa CCM wa awamu hii kama sijakosea ni kama alishawahi kusema yeye sio mwanasiasa, akimaanisha yeye sio muongo muongo wa kutumia waneno matamu ili kupata Umaarufu wa kisiasa. Yeye Ni mtu wa Haina ya vitendo (kwenye hili na kubali kwa asilimia kadhaa).

Bahati mbaya kipindi hiki, ni msimu ya kampeni, ndio mda hasa wa kufanya Siasa. Ingefaa awaachie jukwaa zaidi walio wanasiasa, yaani team yake ya kuratibu Kampeni na kutengeneza umaarufa(kukubalika) kwa Chama kungeandaliwa watu wanaoiweza Siasa.

Hata hivyo bado siku ni nyingi , inawezekana kuna mipango Bora zaidi itakayowavutia Wafuasi. Pia inawezekana ni mawazo yangu tu, ila CCM Bado ina umaarufu wake na unakubaliana zaidi ya hapo muhula uliotangulia.

Kama sivyo, kuna Jambo ambalo ningeshauri ambalo litailetea umaarufu angalau wa kutosha Uchaguzi huu.

1. CCM kulaani matukio yoote ya dhuluma ama uvunjwaji wa Sheria wanayofanyiwa vyama vya Siasa vikiwemo vya Upinzani vyoote. Walaani hata yanayofanywa na vyombo vya serikali, ama Dola. Ambayo yana mlengo wa uonevu dhidi ya wagombea,
Na kwasababu bado u Chama tawala iamuru kusitishwa matendo ya namna hiyo.

2. Ikemee matendo yali(na)yo fanywa na baadhi ya Wafuasi wao dhidi ya wapinzani wao, ambayo sio ya kiungwana kama kurushia mawe misafara ya wapinzani, Kama Mambo hayo yameratibiwa na Wafuasi wao au CCM wenyewe.

3.Taasisi zenye mamlaka ziache Kampeni ziendelee kwa Uhuru. Bila kubughudhi wagombea na ikiwezekana woote walioenguliwa warudishwe. Hili litawaongezea ushindi Upinzani. Ila naamini pia litampatia Ushindi Raisi kwa Ticket ya CCM, hivyo ni sadaka ambayo inabidi waitoe ili kupata Urais.

NB. Nitatoa Utabiri wa atakaye shinda Uchaguzi huu, japo kwa Sasa bado mapema kidogo.
 
Philip mpango alishindwa kumshauri Jiwe kuhusu money circulation, mzunguko wa Pesa ili biashara zifanyike

Pili: Jenister Mhagama kumdanganya Rais na kuondoa FAO la kujitoa

Tatu: TANAPA kuuwa wavuvi Kanda ya Ziwa, Nzega, Mara, Kagera na kuwazamisha ziwani.

Kuuwa wasukuma wenzako sio Jambo zuri.

Sera za uchumi za Philip mpango zilifeli mno

Magufuli alishindwa kutatua tatizo la mafuriko Dar.
 
Shida kubwa ya CCM kuitumia polis,tume na vyombo vya dola kupambana na upinzani badala ya kusimama wenyewe. Kwa mfano wananamtumia siro kupambana na upinzani kule Mara
 
Philip mpango alishindwa kumshauri Jiwe kuhusu money circulation, mzunguko wa Pesa ili biashara zifanyike

Pili: Jenister Mhagama kumdanganya Rais na kuondoa FAO la kujitoa

Tatu: TANAPA kuuwa wavuvi Kanda ya Ziwa, Nzega, Mara, Kagera na kuwazamisha ziwani.

Kuuwa wasukuma wenzako sio Jambo zuri.

Sera za uchumi za Philip mpango zilifeli mno

Magufuli alishindwa kutatua tatizo la mafuriko Dar.
Haya yanaweza kuwa kweli hasa kwa namna wananchi wanavyoitikia kwenye kampeni hizi.

Ndio maana kipindi hiki kipo. Ili ijitathmini na kuona Ni namna gani wanaweza kupata ridhaa ya wananchi.

Yaani Sasa inabidi watumie mbinu ama ushawishi ili wawaaminishe wananchi kwamba Mambo yatakua Bora zaidi.

Ndio maana ya Siasa, na ndio maana ya Kampeni.

Ila bado naona ushawishi wao hautoshelezi.
 
Mungu ameamua kuwanyima maarifa,wake wasiotenda haki na kuwainua wapenda haki ili Kila moja aweze kuuona Utukufu was Mungu.
 
Ccm ilikuwa ni ya kina nape, Makamba, kinana, mwiguru,.. Bashiru, polepole na police tumewatuma waihujumu awamu hii, hakika wamefanya kazi nzuri Sana ya kuibomoa ccm.
 
Ccm ilikuwa ni ya kina nape, Makamba, kinana, mwiguru,.. Bashiru, polepole na police tumewatuma waihujumu awamu hii, hakika wamefanya kazi nzuri Sana ya kuibomoa ccm.
Zipo na mbeleko nyingine,tusipozitambua kwa mchango wao mzuri was kuibomoa ccm tutakuwa hatujawatendea haki.
 
Mungu ameamua kuwanyima maarifa,wake wasiotenda haki na kuwainua wapenda haki ili Kila moja aweze kuuona Utukufu was Mungu.
True Mungu alimpa ccm chatoboy ili imfie hakika imetia.
Tuliwaambia ccm katiba yenu ndio kitanzi chenu, mwenye kiti kuwa na nguvu kuliko chama ilifaa zamani,mnapopata mwenyekiti mwenda wa zimu anaejua kila kitu ni lzm li chama life, wanachama wamekuwa ni wapenzi watazamani
 
CCM hawajakosea kitu ila Waafrika na dunia hawataki DICTATORS full stop.
 
Magufuli aliweka Makufuli masikioni hakutaka kushauriwa. Sasa chama ndiyo hivyo kinamfia mikononi
Hata watumie euro badala ya dola haitowaokoa anga limeshawakataa wamekiuka zindiko la mwenge ilitakiwa ukimbizwe tu hata Kama kuna corona kutimiza agano tambiko la bagamoyo
 
Back
Top Bottom