CCM wanapenda kupush CCM vs CCM ili waendelee kubaki, msikubali kuchezewa

CCM wanapenda kupush CCM vs CCM ili waendelee kubaki, msikubali kuchezewa

Duh Aisee

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2025
Posts
1,297
Reaction score
860
Wanataka siku zote adui yao awe CCM ili waendelee kubaki kututawala.

Au wanataka mpinzani soft soft leo watu wanatekwa kesho tunakutana kwenye mechi ya Simba na Yanga tunachekeana na tag juu “ Upinzani sio Uadui”, sio uadui wakati watu wanauliwa, wanabakwa, chaguzi zinaibiwa, watu hawajazika.

Watu wote wale ambao hawakushiriki na walishiriki uchaguzi 2025 ni CCM, ndiyo hata hao akina Majaliwa, Makamba na wengineo. Michezo ya mjini na inakuwa hivyo.

Msikubali kuchezewa, watu hawajaanza kuuliwa na miili yao kupotezwa October 29, yani mtu amechekea huu ushenzi wote na akampigia kampeni nchi mzima, akamtazama akivunja katiba ya chama chao alafu ghafla leo ajifanya yuko na sisi????

Tumtafute tumjulie hali ila ni mwanaCCM na mnufaika wa haya yote kama wengine

Walimseti aende msiba uliotokea kwa familia ya Magufuli, wakamseti aende Warioba( wanajua ndiyo mtu anapendwa na raia) alafu akajifanya naye anataka katiba.

Tusiache kumtafuta na kumjulia hali, mwisho wa siku ni binadamu ila ninmnufaika wa mfumo
 
Back
Top Bottom