Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Watu mnaojua kiingereza mnaweza kunisahihisha kama neno nililolitumia siyo sahihi. Kiranga na Nyani Ngabu msaada tutani.
Kwa mtazamo wa kijuujuu huwezi kuona kinachotengenezwa na CCM hasa viongozi wake wa juu.
CCM inatengeneza aina fulani hivi ya usultani ndani ya chama hicho na Kwa nchi kwa ujumla.
Sasa hivi kwa mfano mtu anaweza kudhani viongozi wa CCM hutoka kusikojulikana na kuwa viongozi wa chama hicho. Lakini ukweli wa mambo wenye chama chao ndiyo huamua nani ashike nafasi ipi ndani ya CCM.
Nimewaza kuwa kama John Nchimbi akifanikiwa kuwa Makamo wa Rais na baadae kuwa Rais wa Tanzania, nini kitazuia Ridhiwani Kikwete kuwa Waziri Mkuu wakati huo?
Mtoto wa Mwigulu Nchemba, huko mbele ya safari si ndiyo anatayarishwa kurithi ubunge wa baba yake?
Mifano ni mingi itoshe tu kusema kuwa ndani ya CCM kunatengenezwa kizazi Cha kisultani ambacho bila kuwa sehemu yake ama kukubaliwa na wao, itakuwa ni ngumu kwa mtu mwingine nje ya koo hizo teule ndani ya CCM, kuwa kiongozi.
Nawaza Kwa mfano bunge likiisha, Ridhiwani na Salma Kikwete watapeleka kwenye familia Yao kiinua mgongo cha shilingi ngapi?
Bila kusahau kuwa Salma Kikwete alipendekeza Bungeni kuwa wake wa waliokuwa viongozi wakuu nao pia wapewe kiinua mgongo. Akipewa atakuwa na ngapi?
Akirudi nyumbani anakutana na Mzee naye analipwa kila kitu sawa na 80% ya aliyeko madarakani.
Nenda Kwa kina Hussein Mwinyi, kina Amani Karume, kina Nyerere na wengineo.
Sijui kama kina Lucas Mwashambwa ChoiceVariable na kaka yao johnthebaptist watanielewa.
CCM
Kalamu Nguruvi3